G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Waziri wa mambo ya nchi za nje kuwa muongo na mlaghai kama alivyo Prof. Kabudi ni hatari kwa afya. Waziri ambaye hawazi mbali kuhusu majukumu yake inafikirisha sana.
Nakumbuka aliyoongea kwenye sakata la madini siyo tunayoona sasa.Aidha alitoa uongo wa awamu tatu. Wa majadiliano ya tume, wa tulichotegemea kupata na mwingine wa yanayoendelea sasa. Ilikuwa ni maigizo matupu. Haya leo hayanihusu!
Juzi wakati wa msiba wa mzee Mkapa, tulisema wazi kuwa upo mgogoro wa kidiplomasia ambao ulipelekea ndege ya Kenya kugeuza angani na kuwarudisha wajumbe wa kutoka Kenya waliokuja kuhudhuria mazishi yale. Mbiombio Kabudi akaja na taarifa eti ndege hiyo ilikumbwa na hitilafu, tena alizungumza palepale msibani. Mbiombio akaagiza ubalozi wa Tanzania nchini Kenya kutoa taarifa kama yake. Ila Kenya hawakutoa taarifa yoyote kuhusu tukio lile. Tukasema huku kuwa lipo tatizo ila kama kawaida ya wafuasi wasioelewa wakaendelea kushupaza shingo!
Siku mbili baadaye ukweli umedhihirika! Ukweli umewekwa hadharani kuwa upo mgogoro mkali wa kidiplomasia kati ya Kenya na Tanzania.
Kiukweli siyo uungwana hata kidogo kwa kilichofanyika juzi! Hizo ni siasa za kitoto na sijui nani anazianzisha, kwa malengo gani?
Kwanza mimi nashangaa sana, lini ndege ya Tanzania imewahi kutangaza hata kivutio kimoja tu cha utalii kilichopo Kenya? Mbona ndege za Kenya zimeandika hadi hifadhi ya Ngorongoro? Tumewahi hata kuwapa wakenya asante ya mdomo hadharani kwa kututangazia vivutio vyetu vya utalii huko duniani?
Enzi ya utawala wa JK na Mkapa Kenya na Tanzania walikuwa ndugu. Nakumbuka enzi ya Mkapa kila shughuli ya kitaifa marais wote watatu wa nchi za EAC lazima wawepo. Leo kuna nini? Lazima tukiri kuwa lipo tatizo la kimfumo. Rais Magufuli ana hulka ambayo waziri wake wa mambo ya nje anahitaji kujiongeza sana na kuzuia yale maboko ambayo yakitoka kwake yanaleta madhara.
Mbaya zaidi zipo taarifa kuwa mgogoro kati ya Kenya na Tanzania umetanuka hadi kwa mataifa ya Uganda na Rwanda. Pia na wao wameshaacha kushirikiana na Tanzania kwenye mambo mengi.
Ni lazima tuelewe kuwa Rais wa Tanzania ana tatizo kubwa sana la ubaguzi ambalo alianza kuwaita watu weupe "Mabeberu ( Sifa mbaya sana kwa mkuu wa nchi) . Hivyo anahitaji kuwa na waziri anayejua sana kujiongeza na kumshauri ila siyo huyu Kabudi ambaye anacheza kila ngoma ya Magufuli na kutuletea uongo na ulaghai.
Kama nchi ni lazima tukiri kuwa tunatumia njia ya aina yake kuishi na Corona ambayo ni vigumu sana kuaminika usoni pa mataifa mengi. Lazima tuje na mikakati ambayo tutawaeleza wenzetu watuelewe na siyo eti tunapiga Nyungu au miujiza. Ni lazima tujue tupo ndani ya dunia ya aina gani.