Sekta binafsi inakufa kwa kasi kutokana na utegemezi wa mfumo wa kiuchumi ambao hauendani na sera za taifa.
Nchi yetu kimsingi imejijenga kwa mifumo ya kijamaa but tunataka kuoperate kibepari katika sekta za uchumi. Uchumi wa kijamaa mifumo yake ya sheria inategemea sana maamuzi ya serikali katika kuamua matumizi ya rasilimali vile itaona inapendeza.
Mfano, inawezakana kabisa sekta ya mawasiliano ikawa inafanya vizuri na inaajiri watu vema ila viongozi kwa utashi wao wakaona waipige kodi nyingi hadi inakufa halafu akili zao zikawaelekeza kuwa wawekeze kwenye ujenzi wa barabara kwa kodi zile wamekamua. Vijana wakakosa ajira baada sekta ya mawasiliano kufa halafu wao katika vyombo vya habari wakajisifu na kujinadi kuwa serikali inajenga barabara kwa wingi na hayo ni maendeleo kwa wananchi.
Kimsingi magufuri anasimamia sheria na mfumo uliopo katika taifa letu ambao bungeni hawakuwahi kupoteza muda kuuchambua na kuufanyia marekebisho kuendana na uhalisia.
Taifa likiwa na watu/raia wachache mfumo wa ubepari huwa haufai na unakuwa hauna effects. Katika mazingira hayo ya watu wachache ni rahisi sana kwa mfumo wa ujamaa kufanikiwa sababu serikali inaweza ikauza madini, mafuta, au kutumia pesa za utalii kujenga shule, hospitali, mabarabara hata kuwawekea watu pesa kwenye account kama loyalty ya kuwa raia wa nchi husika.
Ila idadi ya watu inaoongezeka tu, rasilimali pamoja na mapato ya serikali ni chache sana kuweza kuwahudumia hao watu wote na kuwapa mahitaji yao ya msingi. Hivyo inabidi natural process ya balance ifanyike kama kuacha soko liwe huria ili watu wajitengenezee ajira na kuajiri watu, serikali inatabakia kuwa msimamizi wa sheria na usalama wa raia,kucontrol supply ya pesa kwenye mzunguko na kuzuia uhujumu uchumi.
Shida ni moja, wengi wa viongozi wetu hawana elimu nzuri ya sociology, uchumi na history. Hizi principles huwa zinawapa uelewa wa namna jamii ina evolve na kubadilika na kuweza kuprededict the next move.
Kwa bahati mbaya, mh. Dkt J.J.P.M yeye ni mtaalamu wa maswala ya kisayansi na principles zake alizosomea ni issue za vipimo ndio maana unamuona katika utendaji wake anakwenda sana na quantity na qualities. Anachagua watu kwenye ranks zake kwa misingi ya ufaulu darasani na miaka ya kazi na kadhalika. Kwa hali ya kiuchumi tuliyonayo sasa hatuhitaji watu kwa misingi hiyo, tunahitaji uwezo na ubunifu.
Sisi hatuhitaji kuwa na kiongozi mwenye mrundikano wa mavyeti ya GPA za 4.5 na aliyesoma Harvard. Tunataka kiongozi ambaye anajua tuna rasilimali watu wa aina gani, na anaye jua kuhesabu tuna list gani ya rasilimali tunazoweza tumia kwa wakati huu kuleta maendeleo na hapo akaweza kuja na sera nzuri za kutuambia watanzania.
But hizi mbwembwe za kupiga pushapu hazitatutoa hapa tulipo. Na ile hali nguvu kazi ya taifa (vijana) wanazidi kuteketea na kupotea..........
Tukitaka kutoka hapa tulipo, inabidi tuapply mixed economy formation ya uchumi, yaani tukubali kuwa serikali na taasisi binafsi zinatakiwa kufanya kazi kwapamoja. Tuweke sheria kali sana kwa viongozi na wafanyabiashara watakaokuwa wakihujumu serikali kwa faida binafsi, familia na jamaa zao.
Tupunguze muda wa kukaa mashuleni sio vijana wanasoma miaka 21 at least mtu akae shule miaka 12 kutoka vidudu hadi chuo kikuu except for baadhi ya taaluma kama udaktari.
Sera za kifedha za benki kuu zibadilishwe na tubadilishe pia sera na masharti ya kibenki ili kuweka clear and direct flow ya pesa kutoka serikalini hadi kwa raia kurudi serikalini tena.