Tatizo la engine kumisi ukikanyaga accelerator kwenye baadhi ya gari za Toyota

Tatizo la engine kumisi ukikanyaga accelerator kwenye baadhi ya gari za Toyota

Mkuu umemuokoa jamaa yangu saana.... ulichokielezea ndio exactly kilichokuwa kinaendelea kwene IST ya jamaa yangu.

Nilochofanya ni nilichukua coil spark za kwenye gari yangu nikahamishia kwenye yake na hapo hapo hili tatizo kwenye gari yake likaisha

Kesho anaamkia kwa wachinjaji wa spea za japan achukue coil spark zake maana tumepin-point tatizo kupitia huu uzi.

Tutakutumia chochote tukipata namba yako, kwa sasa tunasema AHSANTE SANA..

Mkuu

Ninashukuru na ninafurahi pia kama mmeweza kupata solution kupitia huu uzi.

Namba yangu ni 0621 221 606
 
Kumbe na TOYOTA nazo huaribika?...kuna watu ukiwaambia kuwa toyota nazo huchoka na kuharibika, wanatamani kukumeza.
BTW, umesaidia mafundi wengi sana na hii solution.
Keep it up!

Kila gari inaharibika mkuu.

The worst ni kupata tatizo ambalo linaweza kukutesa muda mrefu.

Moja wa watu wa mwanzo ambao niliwakuta wakiwa na hili tatizo alikuwa ameshabadili gearbox.

Maana alichowaza ni kwamba gari inachelewa kuchanganya hivyo fundi wake alilitreat kama tatizo la gearbox.

Hamna kilichobadilika na by the time alishaanza kuwa Hopeless.
 
Kumbe na TOYOTA nazo huaribika?...kuna watu ukiwaambia kuwa toyota nazo huchoka na kuharibika, wanatamani kukumeza.
BTW, umesaidia mafundi wengi sana na hii solution.
Keep it up!
Japo hapa umewachokoza Wajapani wa JF😃😃😃 nadhani watakuwa kwenye kikao sasa hivi kabla waje wakupige vita moja safi.
 
Mkuu asante kwa madini yako, me naomba kuuliza hiv; gari yangu mshale wa speedmeter sometimes hautembei tatizo linaweza kuwa nini mkuu
Speedometer kutokusoma kuna mambo kadhaa.

1. Speedometer yenyewe kuwa kimeo

2. Vehicle Speed sensor hii inakuwa kwenye gearbox.

3. Wiring za kimojawapo au vyote hapo juu.
 
Back
Top Bottom