Mkuu kuna magari ni hatari sana kuendesha kama huna uzoefu nayo
Mi nimezoea kuendesha haya magari yetu ya kimasikini kama Rav 4, IST nk nk ambayo ukifika speed 120 comfortability inapotea unaanza kuona kama gari inapaa na inakosa balance
Siku moja nikaendesha Land cruser Vx kutokata Tanga kuja Dar
Aisee kuna muda unakuta barabara imetuliaa inakuita tu, kwa njisi gari lilivyotulia unadhani upo kwenye speed za kawaida za 100-120.......kuja kuchungulia speed meter nakuta inasoma 180, nili shtuka sana nika achia pedal
Kuanzia hapo nikawana natembea na speed meter tu sivuki 120
Kuna magari unaweza ukawa 200 lakini gari imetuliaa lakini sasa ukibugi kidogo tu hiyo ajali yake nimbaya sana