Tatizo la gari za Nissan kushtukashtuka(misfire) kati ya speed 40Km/h mpaka 60Km/h

Shida hii ipo karibu kwenye kila gari ila kwenye Nissan Hali ni mbaya mno. mfano wa gari zenye hiyo shida ni Dualis, Xtrail T31, Note, Juke na Tiida.

Gari inawaka vizuri, Ila ukianza kuitafuta 40kph ndio unaona hiyo shida hasa kama hujaikanyagia sana na hasa maeneo ya vilima, hata kama ni kilima kidogo.

Shida huwa ni spark plugs.

Sasa watu wengi wamepata mkanganyiko sababu baada ya kubadili plug gari inaweza kutulia hata kwa siku moja au mbili halafu ikarudia tena hali ile ile ya mwanzo. Ikijitahidi kukaa muda mrefu ni mwezi mmoja au ukipiga safari ndefu hutatoboa hata 2000km.

Sababu ya shida hiyo kujirudia baada ya kubadili plug huwa ni plug feki na ndio nyingi zilizojaa madukani.

Shida hii imepelekea watu kubadili plug hata mara 8 kwa mwaka na wengine kuyakatia tamaa magari yao au hata kuyauza.

Solutions ni kupata Spark Plug original.

Mambo ya kuzingatia

1. Plug iwe original na compatible na hiyo engine

2. Usiruhusu fundi kusafisha plug zako(wengi mmejitia kiherehere kusafisha plug na mwisho wa siku mmeingia kwenye hiyo shida)

3. Kama unafanya gapping kwenye plug usiguse electrodes zake vinginevyo plug haitofaa tena.

5. Funga plug ambazo ni PFE design(mostly ni double iridium) au PSPE(ruthenium). Ni plug hizi mbili tu ambazo zinaingia kwenye kundi la plugs zenye uwezo mkubwa wa kuunguza mafuta.

Kwa wenye dualis na Xtrail zenye MR20DE kama umekosa plug original karibu ninazo High performance NCE spark plugs ambazo zitasolve tatizo lako kwa 80,000Km zijazo.

Shida hiyo pia ipo kwenye engines kama EJ20 ya turbo na FB20 za subaru unapokuwa speed 60km/h mpaka 80km/h

1NR FE toyota

TSI engines za VW

Na gari nyingine nyingi na sababu ni hizohizo za spark plugs.
Mkuu plug za dualis bei gani? Maana nshaweka plug nimebadili mara tatu shida ni hiyo ni kama vile inakuwa inashindwa kujua niko gear gani. Mara ya mwisho hadi fundi fulani akasema aah hii itakuwa gearbox badili gear box mkuu unaona inashindwa kutambua iko gear gani. plug nilizoweka nilianza na used za ilala ambazo zimetolewa kwa nissa dualis nyingine, wapi. nikabadili coil wapi, nikawekewa zile zinauzwa 20000 mpya wapi, nikanunua tena nyingine wapi. nishabadili sijui ndo chase ya gearbox wapi. hapa nilikuwa nina mpango wa kubadili gear box yote mwezi ujao.
yani gari ikiwa speed ndogo ndipo kama inaslip slip fulani hivi. ikitembea beyond 60 nimekanyagia hilo tatizo hakuna na wala haiwashi taa ya check engine.
wakati nabadilisha plug iliwasha taa ya check engine, nia mashine ikasoma kuwa plug namba mbili haichomi ndio maana nilizibadili lakini ilikuwa ishaanza kuslip pia.
 
Pia ningeshauri watu wenye magari wanunue kifaa cha kufanya diagnosis ndogo ambayo itakupa codes zenye hitilafu katika engine ya gari lako.

Kila gari ina socket ya kuchomeka kifaa hicho ambacho bei yake si kubwa sana.

View attachment 3136730
Ukitumia kifaa hiki huna haja ya kwenda kwenye garage za mafundi kwani waweza kubadilisha mwenyewe siku za weekend ukiwa home na waoata bia na nyamachoma. Katika package kuna kijitabu kidogo chenye codes zote za hitilafu.

Pia tatizo jingine la engine kusitasita au kuwa na speed ndogo ni catalyst converter kuwa ina shredhold ilojaa uchafu ambayo itabidi ibadilishwe au pia kuisafisha kwa kutumia maji maalum yaitwayo Cataclean.

View attachment 3136742

Hayo maji husafisha catalyst converter, fuel injector na maji hayo humwagwa kwenye tank ya mafuta ambayo yamebakia kidogo.
Mkuu, gari likiwa na tatizo hilo la kushtuka shtuka hata ukiweka mashine, haidetect kuwa kuna kosa, yenyewe itasema kila kitu kipo sawa ingawa wewe muendeshaji unaona kabisa gari halipo sawa.

Ahsante kwa kunipa elimu ya hayo maji, je hapa bongo yanauzwa??
 
Mkuu plug za dualis bei gani? Maana nshaweka plug nimebadili mara tatu shida ni hiyo ni kama vile inakuwa inashindwa kujua niko gear gani. Mara ya mwisho hadi fundi fulani akasema aah hii itakuwa gearbox badili gear box mkuu unaona inashindwa kutambua iko gear gani. plug nilizoweka nilianza na used za ilala ambazo zimetolewa kwa nissa dualis nyingine, wapi. nikabadili coil wapi, nikawekewa zile zinauzwa 20000 mpya wapi, nikanunua tena nyingine wapi. nishabadili sijui ndo chase ya gearbox wapi. hapa nilikuwa nina mpango wa kubadili gear box yote mwezi ujao.
yani gari ikiwa speed ndogo ndipo kama inaslip slip fulani hivi. ikitembea beyond 60 nimekanyagia hilo tatizo hakuna na wala haiwashi taa ya check engine.
wakati nabadilisha plug iliwasha taa ya check engine, nia mashine ikasoma kuwa plug namba mbili haichomi ndio maana nilizibadili lakini ilikuwa ishaanza kuslip pia.
Plug ni Tsh. 370,000/= warranty nakupa mimi 30,000Km

Hayo mambo mengine yote umehangaika Bure.
 
Mkuu, gari likiwa na tatizo hilo la kushtuka shtuka hata ukiweka mashine, haidetect kuwa kuna kosa, yenyewe itasema kila kitu kipo sawa ingawa wewe muendeshaji unaona kabisa gari halipo sawa.

Ahsante kwa kunipa elimu ya hayo maji, je hapa bongo yanauzwa??
jaribu kuulizia kwa wale dealers wakubwa watakuwa nayo.
 
Pamoja sana mkuu, shukrani...

Una recommend duka gani kwa Dar?
Nenda mtaa wa Msimbazi kwenye dula la Toyota. Lipo mkono wa kushoto kama umetokea Fire. Mara ya mwisho nilinunua plugs za injini ya 1ZZ-FE. Plug moja ilikuwa sh 45,000/-. Nenda na chassis number ya gari husika au engine code.
 
vipi Kwa dealers wa mikoani wa Toyota tunaweza pata plug original kwel
 
Nenda mtaa wa Msimbazi kwenye dula la Toyota. Lipo mkono wa kushoto kama umetokea Fire. Mara ya mwisho nilinunua plugs za injini ya 1ZZ-FE. Plug moja ilikuwa sh 45,000/-. Nenda na chassis number ya gari husika au engine code.
vipi plug za brevis fse
 
Nenda mtaa wa Msimbazi kwenye dula la Toyota. Lipo mkono wa kushoto kama umetokea Fire. Mara ya mwisho nilinunua plugs za injini ya 1ZZ-FE. Plug moja ilikuwa sh 45,000/-. Nenda na chassis number ya gari husika au engine code.

Shukrani sana mdau, maana kuna plug nimeuziwa naona gari inatetemeka sana na mwanzo haikuwa hivyo...
 
Maduka yao yapo wapi mkuu?
Jana nmemtembelea bw jitu, kaniwekea plug hizo hadi sasa hivi toka aliponiwekea nshatembea kama kilomita 80 sijapata hko tatzo ngoja niendelee kuipima maana yani nilikuwa nshaaminishwa ni gearbox na nilikuwa ninakwenda kuibadili mwez ujao yani kwenye tarehe 5
 
tukikutana na mafundi wa kukariri tunaishia kutishwa sana, Mimi niliambiwa engene imekufa kisa gari kuchemsha kumbe shida ilikuwa rejeta imetoboka na kuziba baadhi ya matundu
 
Back
Top Bottom