Tatizo la gari za Nissan kushtukashtuka(misfire) kati ya speed 40Km/h mpaka 60Km/h

Mkuu plug za dualis bei gani? Maana nshaweka plug nimebadili mara tatu shida ni hiyo ni kama vile inakuwa inashindwa kujua niko gear gani. Mara ya mwisho hadi fundi fulani akasema aah hii itakuwa gearbox badili gear box mkuu unaona inashindwa kutambua iko gear gani. plug nilizoweka nilianza na used za ilala ambazo zimetolewa kwa nissa dualis nyingine, wapi. nikabadili coil wapi, nikawekewa zile zinauzwa 20000 mpya wapi, nikanunua tena nyingine wapi. nishabadili sijui ndo chase ya gearbox wapi. hapa nilikuwa nina mpango wa kubadili gear box yote mwezi ujao.
yani gari ikiwa speed ndogo ndipo kama inaslip slip fulani hivi. ikitembea beyond 60 nimekanyagia hilo tatizo hakuna na wala haiwashi taa ya check engine.
wakati nabadilisha plug iliwasha taa ya check engine, nia mashine ikasoma kuwa plug namba mbili haichomi ndio maana nilizibadili lakini ilikuwa ishaanza kuslip pia.
 
Mkuu, gari likiwa na tatizo hilo la kushtuka shtuka hata ukiweka mashine, haidetect kuwa kuna kosa, yenyewe itasema kila kitu kipo sawa ingawa wewe muendeshaji unaona kabisa gari halipo sawa.

Ahsante kwa kunipa elimu ya hayo maji, je hapa bongo yanauzwa??
 
Plug ni Tsh. 370,000/= warranty nakupa mimi 30,000Km

Hayo mambo mengine yote umehangaika Bure.
 
jaribu kuulizia kwa wale dealers wakubwa watakuwa nayo.
 
Pamoja sana mkuu, shukrani...

Una recommend duka gani kwa Dar?
Nenda mtaa wa Msimbazi kwenye dula la Toyota. Lipo mkono wa kushoto kama umetokea Fire. Mara ya mwisho nilinunua plugs za injini ya 1ZZ-FE. Plug moja ilikuwa sh 45,000/-. Nenda na chassis number ya gari husika au engine code.
 
vipi Kwa dealers wa mikoani wa Toyota tunaweza pata plug original kwel
 
Nenda mtaa wa Msimbazi kwenye dula la Toyota. Lipo mkono wa kushoto kama umetokea Fire. Mara ya mwisho nilinunua plugs za injini ya 1ZZ-FE. Plug moja ilikuwa sh 45,000/-. Nenda na chassis number ya gari husika au engine code.
vipi plug za brevis fse
 
Nenda mtaa wa Msimbazi kwenye dula la Toyota. Lipo mkono wa kushoto kama umetokea Fire. Mara ya mwisho nilinunua plugs za injini ya 1ZZ-FE. Plug moja ilikuwa sh 45,000/-. Nenda na chassis number ya gari husika au engine code.

Shukrani sana mdau, maana kuna plug nimeuziwa naona gari inatetemeka sana na mwanzo haikuwa hivyo...
 
Maduka yao yapo wapi mkuu?
Jana nmemtembelea bw jitu, kaniwekea plug hizo hadi sasa hivi toka aliponiwekea nshatembea kama kilomita 80 sijapata hko tatzo ngoja niendelee kuipima maana yani nilikuwa nshaaminishwa ni gearbox na nilikuwa ninakwenda kuibadili mwez ujao yani kwenye tarehe 5
 
tukikutana na mafundi wa kukariri tunaishia kutishwa sana, Mimi niliambiwa engene imekufa kisa gari kuchemsha kumbe shida ilikuwa rejeta imetoboka na kuziba baadhi ya matundu
 
Superdoll pale mwembechai wanauza spare na oil og pia?
Itakuwa wameweka na pale nilipita kwenye banda Lao kwenye maonyesho ya Automotive Expo pale Diamond Jubilee. Nikakutana na product za gari ndogo zote za Japan na Europe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…