Nina mdogo wangu ana miaka 6 sasa ila bado anakojoa kitandani kwa anayejua dawa tafadhali naomba anijuze
Mmh, hapa mgeni. Mie mzazi m'babe. Hapo no tv, no eating out, no sodas. Atanyooka tu! Nimesahau no kucheza.
Kwahiyo mimi na wewe tulikuwa vikojozi mi mpaka form 1,nilikuwa naota naogelea bwana.ila vikojozi ni watu wenye vizazi mno,wanazaa kinoma,mimi nimeowa juzi na bado niko honeymoon napiga 7-1 daily,tena nahisi nishaingiza kitu.Na wewe naamini utakuwa na watoto kikojozi mwezangu mstaafu!
dah madokta mbona mnamletea utani huyo jamaa,yan mm naona replies zimeongezeka lkn nikifungua naona utumbo mtupu!!
Ina maana wewe ulikuwa hujikojolei enzi zile uko under 6 yrs?Mmh, hapa mgeni. Mie mzazi m'babe. Hapo no tv, no eating out, no sodas. Atanyooka tu! Nimesahau no kucheza.
Bed wetting au kukojoa kitandani ni hali ambayo inawatokea watoto umri kuanzia miaka 4 hadi 12 na kwa extreem cases inawatokea watu wazima kabisa. Huwa ni hali ambayo muhusika bila yeye mwenyewe kujua anaota kama vile anaenda chooni au yupo chooni au kichakani then anakojoa..akishtuka tayari kitanda kisha lowa.
Ni tatizo la kisaikolojia yaani ugonjwa ambao kitalaam unajulikana kama nocturnal enuresis na unatibika kama muhusika atapelekwa kwa wataalam wa maswala ya akili.
Kilichonisukuma kuandika uzi huu ni matukio ambayo nayasoma kila leo kwenye vyombo vya habari kama last week mtoto Munir wa umri wa miaka sita alipigwa na mama yake kwa kosa la kukojoa kitandani..alipata majeraha makubwa kichwani yaliopelekea kufariki dunia. Pengine mtoto huyu alikua na hii sleeping disorder iliokua inamfanya aote akiwa chooni na kukojoa kitandani.. sasa wazazi wengi wasioelewa ugonjwa huu wao wanapiga au kuwazomea watoto wao bila kujua muhusika ni mgonjwa na wanamdhalilisha. Yapo pia matukio mengine yalioripotiwa watoto hadi wa miaka tisa kuchomwa na moto sehemu mbali mbali za mwili na walezi wao kisa wanakojoa kitandani katika umri huo.
Ifikie mahali serikali ianzishe kampeni ya kuelimisha kina wazazi au walezi magonjwa kama haya hata kwa kugawa vipeperushi hospitali au mashuleni kuelezea ugonjwa huu pengine jamii itaelewa na kupunguza ukatili kwa watoto wagonjwa wasio na hatia.
Kama wewe ni mtu mzima na unakojoa kitandani usiogope wala kuona aibu nenda katibiwe ni ugonjwa ambao una tibika kabisa.
Natoa pole kwa watoto wote na wazazi wanaoteseka na ugonjwa huu wasijue la kufanya.
Ajenge mazoea ya kukojoa kabla ya kulala halafu muamshe kwa mazoea usiku wa manane akojoe hii itamjengea tabia ya kushtuka kill unapofoka ule muda unapomwamsha kila cku.kila la kheri!
mtembeze mitaani achekwe na watoto kwa ule wimbo wa kikojozi huku amevalishwa gunia. Ataacha.