Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Nina mdogo wangu ana miaka 6 sasa ila bado anakojoa kitandani kwa anayejua dawa tafadhali naomba anijuze

Mwache akojowe kwa raha zake, hakikisha unamvalisha diapers asichafue mashuka na godoro. Ataacha.
 
Dah madokta mbona mnamletea utani huyo jamaa, yan mm naona replies zimeongezeka lkn nikifungua naona utumbo mtupu!!
 
Uwe unamuamsha masaa mawili baada ya kulala akakojoe. Simu za Mchina zina alamu nzuri ya kufanya hiyo kazi.
 
Kwahiyo mimi na wewe tulikuwa vikojozi mi mpaka form 1,nilikuwa naota naogelea bwana.ila vikojozi ni watu wenye vizazi mno,wanazaa kinoma,mimi nimeowa juzi na bado niko honeymoon napiga 7-1 daily,tena nahisi nishaingiza kitu.Na wewe naamini utakuwa na watoto kikojozi mwezangu mstaafu!

Hahaha!!, Mimi nilikuwa naota nipo chooni kabisaaa na nimevua hadi kichupi changu nakojoa,nikishtuka ndo namalizia asubuh nabebeshwa godoro wakanitangaze,mimi ni kulia tu nikilala tu tena! Nilichapwa, nikakosa raha, nikanyimwa soda maji usiku lakini wapi, midawa yote nilitumia lakini wapi, ilikata yenyewe.
 
dah madokta mbona mnamletea utani huyo jamaa,yan mm naona replies zimeongezeka lkn nikifungua naona utumbo mtupu!!

Umezoea kula utumbo kwahiyo hilo ni tatizo la kukufanya wewe kila kitu ukione ni utumbo.
 
Hakuna dawa ya mtu kuacha kukojoa zaidi ya kulishwa mavi na mikojo na waganga wa kienyeji. Dawa ni psychological training ambayo itamfanya aache kukojoa. Unaanza kumuamsha mara mbili usiku akakojoe akizoea atajikuta anaamka mwenyewe. Ni zoezi gumu lakini itakubidi ujitahidi kufanya hivyo. I trained my nephew alikuwa 4 years sasa hivi anaamka mwenyewe. Harsh treatment wakati mwingine zinasaidia japo watu wa haki za watoto watakujia juu! Hii inahusisha fimbo, kumnyima vitu anavyopendelea kama mtoto nk. Angalia usimnyime chakula tu.
 
Bed wetting au kukojoa kitandani ni hali ambayo inawatokea watoto umri kuanzia miaka 4 hadi 12 na kwa extreem cases inawatokea watu wazima kabisa. Huwa ni hali ambayo muhusika bila yeye mwenyewe kujua anaota kama vile anaenda chooni au yupo chooni au kichakani then anakojoa..akishtuka tayari kitanda kisha lowa.

Ni tatizo la kisaikolojia yaani ugonjwa ambao kitalaam unajulikana kama nocturnal enuresis na unatibika kama muhusika atapelekwa kwa wataalam wa maswala ya akili.

Kilichonisukuma kuandika uzi huu ni matukio ambayo nayasoma kila leo kwenye vyombo vya habari kama last week mtoto Munir wa umri wa miaka sita alipigwa na mama yake kwa kosa la kukojoa kitandani..alipata majeraha makubwa kichwani yaliopelekea kufariki dunia. Pengine mtoto huyu alikua na hii sleeping disorder iliokua inamfanya aote akiwa chooni na kukojoa kitandani.. sasa wazazi wengi wasioelewa ugonjwa huu wao wanapiga au kuwazomea watoto wao bila kujua muhusika ni mgonjwa na wanamdhalilisha. Yapo pia matukio mengine yalioripotiwa watoto hadi wa miaka tisa kuchomwa na moto sehemu mbali mbali za mwili na walezi wao kisa wanakojoa kitandani katika umri huo.

Ifikie mahali serikali ianzishe kampeni ya kuelimisha kina wazazi au walezi magonjwa kama haya hata kwa kugawa vipeperushi hospitali au mashuleni kuelezea ugonjwa huu pengine jamii itaelewa na kupunguza ukatili kwa watoto wagonjwa wasio na hatia.

Kama wewe ni mtu mzima na unakojoa kitandani usiogope wala kuona aibu nenda katibiwe ni ugonjwa ambao una tibika kabisa.

Natoa pole kwa watoto wote na wazazi wanaoteseka na ugonjwa huu wasijue la kufanya.
 
Ahsante kwa elimu mkuu.
 
Jamani naomba msaada wenu, mwanangu Ana miaka nane sasa still anakojoa kitandani kila Siku. Nifanyeje aache? Please naombeni ushauri wenu wana JF.
 
Ajenge mazoea ya kukojoa kabla ya kulala halafu muamshe kwa mazoea usiku wa manane akojoe hii itamjengea tabia ya kushtuka kill unapofoka ule muda unapomwamsha kila cku. Kila la kheri!
 
Dawa ni kumpunguzia au kutomruhusu kunywa maji inapofika mida ya usiku.Pia kikubwa ni kutoa sana kwenda kukojoa. Ila pia hii kitu ni watu na watu, mi nna mdogo wangu wa kike alikuwa anakojoa kitandani mpk anaanza secondary lkn sasa nna watoto wangu wawili wa kiume mmoja 5 mwingine 3 hawakojoi ila nna kibarua cha kumtoa usiku huyu mdogo.
 
Mpe maji ya kunywa ya kutosha na hata anapoenda kulala mpe tena glasi moja ya maji. Mtu anaweza akashangaa lakini ndiyo dawa yake, kukojoa kitandani hutokea wakati kibofu cha mkojo kinazarisha haidrojeni na naitrojeni na kuunda ammonia ambayo huzuia uwezo wa kuhisi kuja kwa mkojo ukiwa usingizini.

Mpe maji mengi tu na apunguze kula vyakula vinavyolimwa kwa kutumia mbolea za dukani ikiwemo kuacha soda na juisi za viwandani.
 
Ajenge mazoea ya kukojoa kabla ya kulala halafu muamshe kwa mazoea usiku wa manane akojoe hii itamjengea tabia ya kushtuka kill unapofoka ule muda unapomwamsha kila cku.kila la kheri!

Mtembeze mitaani achekwe na watoto kwa ule wimbo wa kikojozi huku amevalishwa gunia. Ataacha.
 
mtembeze mitaani achekwe na watoto kwa ule wimbo wa kikojozi huku amevalishwa gunia. Ataacha.

Utakuwa unamtesa kisaikologia Pasi na sababu mbinu nyingine zishapitwa na wakati..
 
Kunywa maji usiku hakuna problem. Labda chai au vitu venye nicotine ndio umpunguzie kumpa mida za usiku.
 
Back
Top Bottom