Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Ni kweli hili tatizo watu wengi wanalo. Hata nyumbani kuna binti wa miaka 14 ana tatizo kama hilo. Na linamtesa kwa kweli kwa sababu kila siku inabidi atoe godoro kuanika. Awe wazi ili liwasaidie wengi.
Dawa pekee na sahihi, ambayo kweli inafanyakazi ni kuanza kupunguza maji ,juice na soda anazokunywa hasa ifikapo kuanzia mida ya jioni.
Kwamfano ; mzuie kutumia vimiminika kuanzia SAA kumi jioni mpaka mida ya kwenda kulala asitumie kimiminika chochote....ninauhakika hatokojoa endelea hivo hivo kwamuda was wiki mbili, afu mbadilishie , yaani atumie vimiminika hafi SAA kuminamoja jioni.... Pia hapo hatokojoa endelea na zoezi hivo hivo kwa at least wiki mbili tena. Afu baadae muhamishie SAA kumi na mbili hapa akae kwa muda mrefu kama mwezi na nusu au miezi miwili.

Hii kitu inafabyakazi iwe ni kwa mtoto au mtu mzima. Fanya hivo na nipe mrejesho ndani ya siku mbili au siku moja tu.
 
Mkuu Gentamycine, sio busara kutoa jibu la namna hiyo. Hili ni tatizo la kiafya ambalo lipo katika jamii zetu, hatutakiwi kulifanyia mzaha bali ni kulitafutia ufumbuzi.
Huwezi jua leo analo huyu jamaa, huenda kesho likakuanguakia wewe au mtu wako wa karibu na pia utataka ushauri kama huyu ndugu yetu. Ni vizuri ukamshauri japo kumuelekeza njia ilipo hospitali, hapo utakuwa utakuwa umefanya jambo la kiungwana.
ID yako inaonesha wewe ni mtu wa aina fulani ambayo pia ni ya kiheshima, lakini umenivunja moyo kwa ushauri ulioutoa.

Naomba uniwie radhi kama nimekukwaza.

Haina noma Mkuu na barida.
 
Dawa pekee na sahihi, ambayo kweli inafanyakazi ni kuanza kupunguza maji ,juice na soda anazokunywa hasa ifikapo kuanzia mida ya jioni.
Kwamfano ; mzuie kutumia vimiminika kuanzia SAA kumi jioni mpaka mida ya kwenda kulala asitumie kimiminika chochote....ninauhakika hatokojoa endelea hivo hivo kwamuda was wiki mbili, afu mbadilishie , yaani atumie vimiminika hafi SAA kuminamoja jioni.... Pia hapo hatokojoa endelea na zoezi hivo hivo kwa at least wiki mbili tena. Afu baadae muhamishie SAA kumi na mbili hapa akae kwa muda mrefu kama mwezi na nusu au miezi miwili.

Hii kitu inafabyakazi iwe ni kwa mtoto au mtu mzima. Fanya hivo na nipe mrejesho ndani ya siku mbili au siku moja tu.
Asante mkuu nitalifanyia kazi
 
Nenda nae mental mkuu mana hilo tatizo lipo kwenye ubongo unakosa mawasiliano na other parts akiwa amelala, atapata antipsychotics zinaweza kumsaidia. Ñna ndg yangu anatumia hizo dawa wanachoma Sindano kichwani Kuna kamshipa fulani sasa inaweza kumsaidia na yy. Huyu ndg yangu ameshaoa sa iv na amepata mtt hakojoi kitandn tena.
 
Nenda nae mental mkuu mana hilo tatizo lipo kwenye ubongo unakosa mawasiliano na other parts akiwa amelala, atapata antipsychotics zinaweza kumsaidia. Ñna ndg yangu anatumia hizo dawa wanachoma Sindano kichwani Kuna kamshipa fulani sasa inaweza kumsaidia na yy. Huyu ndg yangu ameshaoa sa iv na amepata mtt hakojoi kitandn tena.
asante sana sana je wapi twaweza enda hyo mental department tukafanikiwa???
 
Tafuta ule mpira wa maji mrefu na hakikisha kila siku usiku anapoenda kulala basi unauchukua na kumchomeka nao huyo Kijana katika Lidudu lake kisha ule mpira unaukunjua ili uwe mrefu na unauelekezea nje au bustanini kabisa ili usiku pale anapokuwa anajikojolea ule mkojo usipotee tu bure na badala yake moja kwa moja uende kumwagilia ama Maua ya hapo Kwenu au Shamba. Lichukulieni hilo tatizo lake kama Fursa kuelekea katika Kilimo biashara na hapo hata gharama ya kununua Mbolea ( Samadi ) mtakuwa mmeikoa.
BOYA LINAELEA JUU YA MAJI HALINA MWELEKEO WOWOTE.
 
Mmeamkaje ndugu zangu, naomba mrejesho kwa yeyote alietumia mbinu ya kuacha kukojoa kitandani kama nilivyoelezea.
 
chukua yale mawelewele ya mahindi (a.k.a ndevu) then chumsha anywe asubuhi jioni kwa wiki tu atakuwa amepona. usisahau kuleta hela ya bia
hata me naijua hiyo hiyo ila akichemsha asirudie
 
Nenda pharmacy kanunue dawa inaitwa IMIPRAMINE ni vidonge 50-60 kwa tsh.5000/= tu afu awe anatumia vidonge viwili tu kwa siku tena usiku kila anapotaka kulala mungu atamsaidia atapona. Kwani Mimi binafsi mpaka nilipokua na miaka 17 namalza form four nilkua kikojozi kabsa ila nilitibiwa na hii dawa IMIPRAMINE.
 
Hilo mbona jambo jepesi cha kufanya kama unaishi nae kila siku kabla ya kulala mwambie aende akakojoe baada ya hapo wewe weka alamu kwenye simu yako kila baada ya masaa matatu nenda kamwamshe aende kukojo usione uvivu ukamwambia yeye ndio ajiwekee alamu watu wa namna hiyo huwa wanakuwa wavivu kuamka wewe jitahidi fanya hilo zoezi baada ya majuma machache atazoea na kuacha kabisa kukojoa kitandani.
Sishangai kuona unajibu hivi mkuu, ila kaa ukijua hili ni tatizo kbsa tena ni ugonjwa wa aibu me nmetumia mbinu nyingi Sana hata hii lakini hakunisaidia hata theluthi na ninakumbuka nilikwisha kuwahi kubadili mpaka masaa ya kulala nikawa nalala saa 11 ya alfajiri lakini nikiamka tu kitu imooooooo, ndo nkagundua kua naumwa seriously!!!
 
Habari zenu Wandugu wa JF doctors nina mtoto wangu wa miaka mitatu sasa amekua akisumbuliwa sana na tatizo la kukojoa kitandani, akishalala tu kabla lisaa1 halijaisha inabidi kumuamsha ili akakojoe ukichelewa kidogo tu basi utakuta ashalimwaga.

Hili limekua ni tatizo sugu kwan ata akilala mchana usipomuamsha tu atakojoa apo alipolala kwakweli sijui hali hii inasababishwa na nin kwan nimejaribu kumkataza asinywe maji jioni lakin bado anakojoa.

Nimeona nije kwa Wataalamu hapa nitapata msaada juu ya Tiba sahihi ya kuacha kukojoa
Ahsanteni
 
Tatizo dogo sana hilo, nenda kwenye maduka ya dawa za kisunna utatatuliwa tatizo lako.
 
Kwa hisani ya Fadhili paulo

Dawa za asili 8 zinazotibu tatizo la kukojoa kitandani

1. Maji ya Kunywa

Ikiwa mtoto au hata mtu mzima mwenye tatizo hili atakunywa maji kabla ya kwenda kulala (ndiyo namaanisha kabla ya kwenda kulala usidhani nimekosea) basi hataweza kukojoa kitandani tena akiwa usingizini.

Kile unatakiwa kufanya ni kunywa maji mengi zaidi kila siku kutwa nzima kidogo kidogo.

Kukojoa kitandani hutokea wakati kibofu cha mkojo kinazalisha hydrogen na nitrogen kwa pamoja na kuunda amonia. Amonia ni sumu katika mwili wa binadamu. Wakati ubongo unapopata ujumbe kutoka kwenye kibofu cha mkojo, ubongo humfanya mtoto aote kwamba yupo chooni na hatimaye hukojoa akiwa usingizini.

Huku yupo usingizi bado ataona wazi yupo chooni sababu ya hiyo ammonia.

Kwahiyo sababu ya mtu kukojoa kitandani ni matokeo ya kuundwa kwa amonia kwenye kibofu cha mkojo na amonia hii inaondolewa kirahisi mwilini kwa kunywa maji mengi kila siku.

Watu wengi hawanywi maji ya kutosha kila siku, wengi kama siyo wote wanasubiri KIU ndipo wanywe maji jambo ambalo ni kosa. Kiu ni ISHARA ya mwili iliyoCHELEWA ya kuhitaji maji.

2. Mdalasini

Mdalasini ni dawa rahisi zaidi kwa mtoto anayekojoa kitandani. Inaaminika kwamba kiungo hiki huufanya mwili kuwa wa moto moto.

Chukua mdalasini ya unga kama kijiko kidogo kimoja hivi cha chai changanya na asali kijiko kidogo tena na upake kwenye kipande cha mkate na umpe mtoto ale kila siku wakati wa chai ya asubuhi

3. ZabibuBata (Indian Gooseberry)

ZabibuBata ambazo pia hujulikana kama amla ni dawa nyingine ya kihindi nzuri kwa ajili ya tatizo hili la kukojoa kitandani.

Chukua zabibubata 2 kisha ondoa ganda lake la nje na uziponde kidogo, halafu changanya pamoja na kijiko kidogo cha chai cha asali na kiasi kidogo cha binzari ya unga. Mpe mtoto kijiko kidogo cha chai cha mchanganyiko huu kila siku asubuhi mpaka atakapopona.

4. Masaji

Masaji pia inatibu tatizo la kukojoa kitandani na kwa matokeo mazuri zaidi tumia mafuta ya zeituni (olive oil).

Yapashe moto kidogo mafuta ya zeituni ili yawe ya uvuguvugu kwa mbali na upake ya kutosha sehemu ya chini ya tumbo la mtoto na ufanye masaji eneo hilo polepole kwa dakika kadhaa.

Fanya zoezi hili kila siku mpaka umeridhika na mtokeo yake.

5. Jozi (Walnuts) na ZabibuKavu (Raisins)

Jozi na Zabibu kavu vinaweza pia kutumika kupunguza tatizo la kukojoa kitandani. Watoto wengi watafurahia pia kutumia kwani hivi ni vitu vya asusa (snack).

Mpe mtoto jozi 2 na zabibu kavu 5 kabla ya kwenda kulala kila siku kwa wiki kadhaa mpaka umeanza kuona mabadiliko.

6. Asali mbichi

Dawa nyingine maarufu kutibu tatizo la kukojoa kitandani ni asali mbichi. Watoto wengi wanapenda radha tamu ya asali na hivyo ni rahisi kutumika kwao kama dawa.

Mpe mtoto kijiko kidogo kimoja cha chai cha asali mbichi kila anapoenda kulala kila siku mpaka atakapopona. Unaweza pia kuchanganya na maziwa fresh wakati wa chai ya asubuhi.

7. Siki ya tufaa (Apple Cider Vinegar)

Siki ya tufaa husaidia kuweka sawa usawa wa asidi na alkaline mwilini (body’s Ph) na hivyo kupunguza asidi iliyozidi katika mwili kitu ambacho kinaweza kuwa ni moja ya sababu za tatizo la kukojoa kitandani.

Siki ya tufaa pia husaidia kuondoa sumu mbalimbali mwilini pia hutibu tatizo la kufunga choo vitu vingine ambavyo husababisha tatizo la kukojoa kitandani.

Mimina vijiko viwili vya chai vya siki ya tufaa ndani ya glasi moja (robo lita) ya maji ya kunywa na umpe mtoto anywe kutwa mara 1 kila siku, unaweza pia kuongeza asali kidogo ndani yake kupata radha. Vizuri akinywa wakati wakula chakula cha mchana au cha jioni.

8. Mbegu za Mharadali (Mustard Seeds)

Dawa nyingine nzuri kwa tatizo la kukojoa kitandani ni mbegu za mharadali. Ni dawa nzuri pia kwa wale wenye tatizo la U.T.I (yutiai).

Weka nusu kijiko kidogo cha chai cha mbegu za mharadali au unga wa mbegu hizi ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha maziwa fresh asubuhi na umpe mtoto anywe kinywaji hiki lisaa limoja kabla ya kwenda kulala kila siku mpaka amepona.



Mambo ya mhimu kuzingatia ili ufanikiwe na dawa hizi:

• Wasiwasi na mfadhaiko (stress) huweza kuongeza ukubwa wa tatizo. Hivyo badala ya kumkalipia au kumdhalilisha kila siku mtoto muonyeshe upendo na uwe tayari kumsaidia polepole mpaka anapona tofauti na hapo tegemea tatizo kutokuisha kwa haraka.

• Mhimize mtoto kwenda kukojoa kabla ya kwenda kulala kila siku

• Hakikisha kuna taa au mwanga wa kutosha njia ya kuelekea chooni, wakati mwingine mtoto akiona giza anaogopa kwenda chooni hasa kama choo kipo mbali na anapolala hasa kwenye nyumba zetu hizi za uswahilini.

• Mpe zawadi yoyote ndogo kila siku anapofanikiwa kuamka salama bila kukojoa kitandani, hii itamuongezea nguvu na moyo zaidi wa kujidhibiti zaidi na tatizo lake.

• Dhibiti matumizi ya juisi hasa juisi zenye sukari nyingi na za dukani nyakati za jioni.

• Epuka vinywaji vyenye kaffeina kama vile chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi, malta, energy drinks zote na vingine vyote vyenye kaffeina ikiwemo chokoleti

• Tibu tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara.

• Tumia karatasi linalozuia maji kupenya kwenye godoro moja kwa moja ili
kupunguza harufu mbaya chumbani na usumbufu usio wa lazima.

• Weka alamu muda ule unaona mara nyingi mtoto ndiyo hujikojolea, weka saa yenye kengele (alarm) muda huo ili aweze kushtuka kabla na aende chooni.

Tatizo la kukojoa kitandani si tatizo linaloweza kutibika kwa haraka haraka ndani ya siku 2 au 3. Kuwa mvumilivu na mpole, walau jaribu tiba kwa mwezi mmoja mpaka miwili mfululizo na usikate tama haraka.
Asante sn JOVEREST I never thought that u can deliver such a useful materials like these
 
Back
Top Bottom