chief chakicha
Member
- Nov 3, 2018
- 61
- 67
Great [emoji106]
Mkuu pole sana ,kwanza nikupongeze kwa kulivalia njuga swala la binti yako umeliwahi ,ukiliacha likaenda ukubwani laweza mletea fedheha kubwa kwenye mahusiano na ndoa yake swala hili linatatulika kwa njia mbili
1. Kidaktari
Kaka nenda hospitali kubwa kutana na daktari bingwa wa masuala ya kibofu ,sisemi dawa za kienyeji hazisaidii ila mara
nyingi ni kubahatisha kuua kindege juu ya screen ya tv waweza ua kindege ukapasua tv ,sababu za hali hiyo ni nyingi
-aweza kuwa ana kisukali cha kuzaliwa (usiogope 80% hutibika)
-Matumizi ya kupitiliza ya carboneted drinks (soda,sparkling waters etc)
-etc
UGONJWA HUU UNATIBIKA KABISA
2. Kiroho
Huu ni moja ya ugonjwa pendwa na walozi au roho chafu kama wewe ni mkristo usimpeleke kwa wauza mafuta ya upako au sijui maji ya uzima ,peleka kwenye makanisa yasiyo binafsi kama mlokole peleka TAG kwenye maombi usisahau kutoa na sadaka kumsihi mungu akuhurumie ,kama wewe ni muislamu usiende kwa hawa wanaojitangaza mara wanamajini,mara nyota huo sio uislamu nenda msikiti unaosali kaongee na imamu atakupa dua stahiki ziombe huku ukifunga ,wa dini za asili usisafiri mbali nenda kaone wazee kijijini kwenu
NB: Wasio wakristo au waislamu wafuate viongozi wao husika sio hawa matapeli wa mitandaoni
Karibu