Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Kama upo Dar nenda pale kkoo sokoni maduka ya dawa asili nunua kungu manga robo shs elf 10 tu msagie alafu utampa kijiko kimoja asubuhi kimoja jioni kijiki kisijae sana maana ukila nyingi unalewa.
 
Kama upo serious njoo DM nkupe maelezo ya dawa ya kufanya ndani ya week 3 utaleta mrejesho ni buree
Fanya hapa mkuu tufaidike sote, majanga haya leo unasikia kwa mwenzako kesho linakukuta wewe unaanza kuhangaika, wengi ni wazazi humu tusaidiane.
 
Nina bint wa miaka 9 ila ana tatizo la kukojoa kitandani, yaani anaweza kukojoa hata mara mbili kwa usiku mmoja. Pia hata mchana akilala anaweza akakojoa pia.

Msaada please.
Chukua ndevu za mahindi zikaushe au zichemshe na maji yake MPE anywe kila siku asubuhi na jioni ndani ya wiki atakuwa ameacha
 
Dawa zipo hospital tena bei rahis kabisa zinakaza mirija ya mikojo..mie pia mwanangu alikua na shida hiyo nimehangaika dawa zote za kienyeji lakin wap baadae ndo nikaenda duka la dawa nikapewa na sasa kapona ila zinahitaji uvumilivu maana anaeza tumia miezi zaid ya mitatu ndo uone matokeo mazuri
 
Wapi hilo duka tuelekeze kama ni Dar.
 
Dawa ni ndogo s
Nina bint wa miaka 9 ila ana tatizo la kukojoa kitandani, yaani anaweza kukojoa hata mara mbili kwa usiku mmoja. Pia hata mchana akilala anaweza akakojoa pia.

Msaada please.
Dawa ndogo sana!
1.KIPIGO ASUBUHI KILA ANAPOJIKOJOLEA
2.KILA MWANAFAMILIA ASHIRIKI KUMSUTA NA KUMZOMEA KILA SIKU.
3.HAKIKISHA WEWE KAMA MZAZI AU MLEZI UNAMUAMSHA MTOTO MARA USIKU MARA TATU KWENDA KUJISAIDIA.
 
Asinywe vimiminika baada ya saa kumi na pia hakikisha kabla ya kulala anaenda kukojoa na usiku muwe mnamuamsha akakojoe
 
Niseme asante kwa michango na ushauri wenu wakuu, nami kwa uzoefu nimepitia hiyo hali na bado naendelea kupambana nayo.... naona matumaini ila bado sijafikia hitimisho.

Nina kijana wangu (ME) umri miaka 12 ni mhanga wa kukojoa kitandani, tumekuwa tukijaribu hasa tiba asili zikiwemo hizo ‘ndevu za mahindi’ na ‘maji ya mchele’ na hata kumyima vimiminika mida ya usiku lakini hola haikufaa kitu.... ila pia nikiri hatukulifanya ‘siriazi’ kivile ilikuwa ni kujaribu tu ila sio kwa umakini mkubwa na mwendelezo.

Tatizo lake hasa sio usingizi mzito kwanza hakojoi kila siku (wastani mara mbili au tatu kwa wiki) na anao uwezo wa kujiamsha mwenyewe ila wakati huo anakuta shughuli imeisha, anachokifanya ni kubadili nguo tu alizovaa na kumsogeza mdogo wake (dogo hakojoi) mahali penye unyevu huku yeye akihamia sehemu salama kuuchapa usingizi.... lengo ni kuficha aibu kwa sababu ya ubishi ikitokea alikunywa juisi au maji usiku au aliamshwa akagoma kwa kujidai kuwa hana mkojo.

Majuzi hapa hata mwezi haujapita ilitokea namna ambayo ilinilazimu kulala naye kitandani kwangu, saa 4 usiku wako macho sebleni nawaaga niende kupokea mgeni stendi natoa maelekezo nani alale wapi na kabla ya kulala kuhakikisha wamekojoa..... ile tu saa 6 narudi home nakuta dogo keshafanya yake kitandani kwangu.

Nikachukulia bahati mbaya na kuhisi labda walisinzia sebleni kisha wakazama ndani bila kukojoa, siku iliyofuata tumezingatia hatua zote kabla ya kulala lakini alikojoa tena mapema tu kabla ya muda niliopanga kumwamsha. Nilisikia uchungu ambao ulinifanya kulichukulia hili suala kwa umakini wa kipekee.

Tangu siku hiyo nikaanza kuwa namwamsha mara tatu kila usiku bila kujali ana mkojo au laah, ni wiki ya tatu sasa nimekuwa nikifanya hivyo kwa mafanikio makubwa na nimeona iko haja ya kuendelea hadi ubongo wake uzoee kumwamsha. Naona kabisa hata kisaikolojia ni faida kwake na anaelewa vile nafanya kirafiki na kwa nia njema nimeamua kubeba tatizo lake kuliko vichapo na vitisho ambavyo tulishapitia bila mafanikio.

Hitimisho: Hata watu wazima kwenye zile ndoto zetu huwa tunakojoa, sema mkojo unakuwa tofauti na haupenyi kwa godoro ila madoa kwa shuka wala hakuna adhabu tunapata. Kwa hiyo tusiwaadhibu watoto kwa maana ya ndotoni au usingizini sio utashi wao bali tuwasaidie.
 
Nina bint wa miaka 9 ila ana tatizo la kukojoa kitandani, yaani anaweza kukojoa hata mara mbili kwa usiku mmoja. Pia hata mchana akilala anaweza akakojoa pia.

Msaada please.
Mwambie akiwa anaota either anaenda chooni au yuko chooni/kichakani anataka kukojoa basi mwambie aamke haraka sana kabla hajakojoa.

Akiwa ndotoni anaota anakojoa basi jua in real world pia atakua anakojoa.
 
Mpeleke hospitali, hapa kwa wafanyabiashara huambui kitu. Linatibika vizuri kabisa wala usihofu.
Nina bint wa miaka 9 ila ana tatizo la kukojoa kitandani, yaani anaweza kukojoa hata mara mbili kwa usiku mmoja. Pia hata mchana akilala anaweza akakojoa pia.

Msaada please.
 
Kukojoa kusikieni jamani tulikuwa tunakaa na jamaa above 18 hostel alikuwa anakojo kila siku yaan haipiti siku hata moja

Yeye wakati wengine tunaamka kwenda kupiga msuli asubuhi inabidi yeye awahi ziwani kwenda kufua mashuka kila siku jamaa alikuwa inferior sana yani sana alikuwa hawezi kugombana na mtu maana alikuwa anajua weakness yake ilipo.
Kuna kipindi alikuwa ana gombania msichana na jamaa sasa demu akamuelewa mshikaj ,opponent wake baada ya kuona hivyo akaenda kumwamba demu eti unaringa na huku unadate na kikojoz demu akamtema jamaa siku ile ile.

Nakumbuka baada ya mikojo kuzidi tukapanga tununue viroba tunywe sisi marafiki zake tumwabie ukweli maana kwa aibu ile hakuna aliyekuwa na kifua cha kumwabia , wengine wakaamua kuwa ikifika saa 7 mtu ajitolee kumshitua.

Kuna siku ya kufunga ikafika watu tukawa kila mti anatoa godoro anaamisha kukusanya kwenye chumba maalumu lakini yeye akagoma hatoi bado ataendelea kuwepo kufika usiku akapaki vitu vyake akasepa akaacha godoro sasa ile mwalimu kupita akasema mbona huyu jamaa kaaga kumbe hajarudisha godoro ebu chukua ulilete huku daa kulinyanyua mkojo uliokuwepo sio wa dunia hii mpaka mwalimu akashanga.

Chini kwenye chaga alikuwa ametafuta karatasi ngumu za nailoni kubwa ameweka yaani zimejaa mkojo kama lita tano lakini mkojo umetuama tu haupiti chini.
Hii inshu usiombe ikukute
 
Habari wakuu,

Nina mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 12 sasa anaingia class 7. Anakojoa kitandani kila siku. Kwa mwezi anaweza asikojoe mara moja au mbili tu. Lakini siku zote hizo anakojoa sana.

Katumia dawa za kienyeji, za kimasai pia lakini imeshindikana. Nikampeleka hospital kuna vidonge alipewa. Walisema akinywa ndani ya siku 30 tatizo litaisha. Hakuna unafuu. Nikampeleka Muhimbili kuna Dr niliambiwa anasaidia lakini ilishindikana. Dr alisema hali itaisha yenyewe.

Yeye binti pia haipendi hii hali. Maana huwa anakuja na njia nyingi za kupona tatizo lake kama kunywa maji ya mchele, kunywa maji ya nazi, kuchemsha yale manyoya ya mahindi mabichi nk.

Sasa anakaribia kukua na soon ataenda form one boarding.

Naomba msaada wenu kwa yeyote anayejua dawa au Dr anaweza msaidia please. Tupo Dar
 
Hii inaitwa enuresis. Daktari wa mfumo wa akili hasa wa watoto atakusaidia.Tatizo liko kwenye mfumo wa fahamu. Ubongo wa binadamu unafanya kazi masaa 24. Kibofu kikijaa ujumbe unafika kwenye ubongo na usingizi unapata.

Mtoto wa miaka miwili bado mishipa ya fahamu pamoja na sphincter zinajijenga lakini miaka mitatu watoto wengi huwa wanaamka. Wengine hufika miaka 5 lakini 12 ni tatizo.

Weka alarm ya kukuamsha umpeleke choo ni kila baada ya masaa manne.
 
Asante sn mkuu. Hii ya alarm nmeifanya sana. Unaweza enda muamsha unakuta ashakojoa. Au naweza mwamsha akakojoa chooni lkn akirudi kulala baada ya muda anakojoa tena. Mpk nmepeleka kwenye maombi jamani
 
Me nafikiri hii sijui ni kurithi maana nakumbuka binafsi nilifikisha mpaka nyundo <20 nlkua bado nakiwasha tu [emoji23][emoji41] ila ikatoweka tu celew niaje bila dawa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom