Habari wakuu,
Nina mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 12 sasa anaingia class 7. Anakojoa kitandani kila siku. Kwa mwezi anaweza asikojoe mara moja au mbili tu. Lakini siku zote hizo anakojoa sana.
Katumia dawa za kienyeji, za kimasai pia lakini imeshindikana. Nikampeleka hospital kuna vidonge alipewa. Walisema akinywa ndani ya siku 30 tatizo litaisha. Hakuna unafuu. Nikampeleka Muhimbili kuna Dr niliambiwa anasaidia lakini ilishindikana. Dr alisema hali itaisha yenyewe.
Yeye binti pia haipendi hii hali. Maana huwa anakuja na njia nyingi za kupona tatizo lake kama kunywa maji ya mchele, kunywa maji ya nazi, kuchemsha yale manyoya ya mahindi mabichi nk.
Sasa anakaribia kukua na soon ataenda form one boarding.
Naomba msaada wenu kwa yeyote anayejua dawa au Dr anaweza msaidia please. Tupo Dar