Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Msimuhukumu mleta Uzi. Mpeni msaada, labda ugonjwa
Hatumuhukumu, ndiyo tunamkumbusha kuvuta shuka asubuhi, mtoto akifikia hatua anakojoa mpaka miaka 10 kweli kuna kauzembe sana.
 
Mzazi atueleze vizuri,je mtoto amemhimiza vya kutosha kuhusu swala la kutokujoa kitandani,au ukili udhaifu huo km hukufanya hivyo. Pili km umejitahidi imeshinfikana pia sema make kukojoa kwingine siyo uzembe,malezi au kutowajibika vzr kwa mzazi,pia kuna UGONJWA sema/ fafanua vzr usaidiwe
Tunajitahidi sana kumwamsha usiku ili akojoe lakini bado ni ngoma nzito, niliwahi kutishia kwa FIMBO lakini hakuna matokeo mazuri.
 
Rejea mada tajwa hapo juu.

Nina mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 10 sasa lakini bado anakojoa kitandani, nafikiria kwa umri huu ni mkubwa mtu kukojoa kitandani.

Tafadhali wakuu naomba mnisaidie nini chakufanya, kuna tiba ya tatizo hilo?
Halafu usifikiri lakini ni kweli kosa how miaka kumi? Mtoto wa miaka 3 tu anaweza asijikojolee, akawa anamka anakojoa kwenye poti yake regularly, ni namna unavyomzoesha mtoto, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
 
Chemsha ndevu za mahindi kisha awe anakunywa maji yake yakiwa ya mepoa asubuhi na usiku kwa muda wa siku saba.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Usiku kabla ya kulala anakunywa maji sana?Kabla ya kwenda kulala akakojoe na usiku midnight mwamshe akakojoe.
Kuna wangu mmoja ameacha kukojoa akiwa na miaka 8.Ila kusema ukweli nilichoka kumuamsha usiku ikabidi usiku akawa anavaa pempers. Sasa ana miaka tisa hakojoi tena kitandani,akibanwa anaamka mwenyewe kwenda chooni usiku.
 
Rejea mada tajwa hapo juu.

Nina mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 10 sasa lakini bado anakojoa kitandani, nafikiria kwa umri huu ni mkubwa mtu kukojoa kitandani.

Tafadhali wakuu naomba mnisaidie nini chakufanya, kuna tiba ya tatizo hilo?
Hilo ni tatizo walilonao baadhi ya watoto.

Ingawa nimesoma wengi humu wanasema ni kudekeza mtoto ambapo siyo kweli.

Wengi wanaobwabwaja hapa bila kutoa suluhisho wakidhani kuadhibu mtoto ndiyo suluhisho, ujue hao hawajakumbana na vikojozi na hawawezi kufanya lolote.

Kwanza tatizo hilo huwaandama watoto involuntarily kuanzia wakiwa wachanga hadi umri wa balekhe wa miaka 15 na kisha tatizo hilo hukoma na kuondoka lenyewe.

Akiendelea baada ya umri huo nenda hospitali kawaone wataalamu.
 
Sometimes ni kama ugonjwa .
Kaka yangu aliacha kukojoa akiwa form4 na hiyo ni baada ya kutumia dawa.
Wazazi walimtandika baadaye wakagundua jibu si kutandika.

Ila ilimsaidia sana kuwa msafi,yaani ni msafi Sana kuanzia sehemu anapolala, mavazi yake na mwili wake.
 
Pia usimkaripie,maana huwa wanaona kama wako chooni wanakojoa,kumbe wapo kitandani.Ni ndoto unaota umebanwa mkojo tena unaenda chooni kuja kushtuka kumbe yupo kashusha mzigo kitandani.
Ni kisaikolojia zaidi. Ataacha tu.
 
Anza kwa kumuamsha usiku akakojoa hata kama hana mkojo yani aamke 2 times usiku.

Kumwamsha usiku sio tiba, hii inamjengea mazoea ya kukojoa kila ikifika muda huo ikiwa hatoamshwa, ahimizwe kunywa maji mengi asubuhi na kukojoa kila mara mchana kutwa hadi ubongo utazoea.

Mkojo ni matokeo ya kunywa, muhimu ni kumdhibiti kunywa maji kuanzia mida ya jioni, au anywe kiasi kiduchu sana baada ya chakula.

Nimekuwa na mtoto wa hivyo, nilijaribu mbinu nyingi ikiwemo vitisho na vipigo kabla sijagundua hii. Alikuja kukoma akiwa na miaka 13 kwa njia hii.
 
Usiku kabla ya kulala anakunywa maji sana?Kabla ya kwenda kulala akakojoe na usiku midnight mwamshe akakojoe.

Kuna wangu mmoja ameacha kukojoa akiwa na miaka 8.Ila kusema ukweli nilichoka kumuamsha usiku ikabidi usiku akawa anavaa pempers. Sasa ana miaka tisa hakojoi tena kitandani,akibanwa anaamka mwenyewe kwenda chooni usiku.

Hanywi mengi ni glasi moja tu.
 
Rejea mada tajwa hapo juu.

Nina mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 10 sasa lakini bado anakojoa kitandani, nafikiria kwa umri huu ni mkubwa mtu kukojoa kitandani.

Tafadhali wakuu naomba mnisaidie nini chakufanya, kuna tiba ya tatizo hilo?
Kaka Baba yake mwenyewe unaakili ya ki-ccm, wewe mwache akojoe tu. Akifikisha umri kama wa Wassira aka Tyson ataacha kukojoa.
 
Back
Top Bottom