Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Tunajitahidi sana kumwamsha usiku ili akojoe lakini bado ni ngoma nzito, niliwahi kutishia kwa FIMBO lakini hakuna matokeo mazur
Msimchape sio kosa lake. Nenda nae taratibu. Unatakiwa umwamshe kila siku hata mara tatu. Ni kazi kama hauwezi mnunulie pempers zipo zenye kama chupi ila hata akikojoa haozeshi godoro.
 
Hilo ni tatizo walilonao baadhi ya watoto.

Ingawa nimesoma wengi humu wanasema ni kudekeza mtoto ambapo siyo kweli.

Wengi wanaobwabwaja hapa bila kutoa suluhisho wakidhani kuadhibu mtoto ndiyo suluhisho, ujue hao hawajakumbana na vikojozi na hawawezi kufanya lolote.

Kwanza tatizo hilo huwaandama watoto involuntarily kuanzia wakiwa wachanga hadi umri wa balekhe wa miaka 15 na kisha tatizo hilo hukoma na kuondoka lenyewe.

Akiendelea baada ya umri huo nenda hospitali kawaone wataalamu.
Asante mkuu, hata leo nawaza nikawaone madokta wapo nane 8 niseme nao.
 
Sometimes ni kama ugonjwa.

Kaka yangu aliacha kukojoa akiwa form4 na hiyo ni baada ya kutumia dawa.

Wazazi walimtandika baadaye wakagundua jibu si kutandika.

Ila ilimsaidia sana kuwa msafi,yaani ni msafi Sana kuanzia sehemu anapolala, mavazi yake na mwili wake.

Dawa gani hiyo ndugu?
 
Pia usimkaripie,maana huwa wanaona kama wako chooni wanakojoa,kumbe wapo kitandani.Ni ndoto unaota umebanwa mkojo tena unaenda chooni kuja kushtuka kumbe yupo kashusha mzigo kitandani.
Ni kisaikolojia zaidi. Ataacha tu.
Asante
 
Hanywi mengi ni glasi moja tu
Akinywa maji iwe hata masaa mawili kabla hajakwenda kulala. Then before kulala akojoe. Then unamwamsha hata mara tatu usiku. Uwe consistent katika kumwamsha. Pia ongea nae vyema usimchape. Muulize nini kinamtokea hadi anajikuta kakojoa kitandani? Huyo ni mwanao. Kwani unafikiri yeye anapenda kukojoa kitandani?
 
Kumwamsha usiku sio tiba, hii inamjengea mazoea ya kukojoa kila ikifika muda huo ikiwa hatoamshwa, ahimizwe kunywa maji mengi asubuhi na kukojoa kila mara mchana kutwa hadi ubongo utazoea.

Mkojo ni matokeo ya kunywa, muhimu ni kumdhibiti kunywa maji kuanzia mida ya jioni, au anywe kiasi kiduchu sana baada ya chakula.

Nimekuwa na mtoto wa hivyo, nilijaribu mbinu nyingi ikiwemo vitisho na vipigo kabla sijagundua hii, alikuja kukoma akiwa na miaka 13 kwa njia hii.
Nini kilisaidie sasa akaacha?
 
Hilo ni tatizo walilonao baadhi ya watoto.

Ingawa nimesoma wengi humu wanasema ni kudekeza mtoto ambapo siyo kweli.

Wengi wanaobwabwaja hapa bila kutoa suluhisho wakidhani kuadhibu mtoto ndiyo suluhisho, ujue hao hawajakumbana na vikojozi na hawawezi kufanya lolote.

Kwanza tatizo hilo huwaandama watoto involuntarily kuanzia wakiwa wachanga hadi umri wa balekhe wa miaka 15 na kisha tatizo hilo hukoma na kuondoka lenyewe.

Akiendelea baada ya umri huo nenda hospitali kawaone wataalamu.
Ok naongelea tokana na uzoefu, nina mtoto wa ndugu yangu ninaishi nae ana miaka 11 bado alikua anajikojolea, nikamuuliza mama yake mtoto wako anashida gani mimi siwezi ishi nae, akasema kuna dawa anampa amekua akijikojolea kwa muda mrefu, nikamwambia haiwezekani akaniambia hata kaka yake alifika miaka 12 anakojoa akawa anatumia dawa.

nikasema huu ni upumbavu nikaweka mpango kuna siku nikamtegea amekojoa tu nilimchapa sana, na kumpa mkakati akikojoa utalala chini na usiku weka alarm usituke ukakojoe, navyokuambia sasa ana miezi miwili hajajikojolea.
 
Akinywa maji iwe hata masaa mawili kabla hajakwenda kulala. Then before kulala akojoe. Then unamwamsha hata mara tatu usiku. Uwe consistent katika kumwamsha. Pia ongea nae vyema usimchape. Muulize nini kinamtokea hadi anajikuta kakojoa kitandani? Huyo ni mwanao. Kwani unafikiri yeye anapenda kukojoa kitandani ?
Hapendi na ukimuuliza hata kwa upole anaonyesha kusononeka kabisa.
 
Hayajakukuta.
Una watoto wenye umri gani??
Umeshawahi kulea Mtoto anayekojoa??
Au umeamua tu kuchangia ili umponde mtoa mada!?!
Soma post zote utakutana na nilioelezea, hatu coment for funy, kama wewe u do for funny sawa, namsaidia ili aamke amelala sasa, we ni mdogo sana huwezi elewa, so tulia, wengine humu ni watu wazima, nina comment navyotaka mimi ili imuelimishe na sio unavyotaka wewe na wengine, mimi ndiyo nampa ushauri mzuri, sio nyie na miti shamba, hiyo miti shamba inaenda kuziba mirija wakati wa usiku ili asikojoe ni mind set tu na imani yako, watoto hukua na tabia tokana na malezi ya wazazi. Garbage in garbage out
 
Hatumuhukumu, ndiyo tunamkumbusha kuvuta shuka asubuhi, mtoto akifikia hatua anakojoa mpaka miaka 10 kweli kuna kauzembe sana,
Bro acha kusema hivyo huo ni ugonjwa ase na wat weng inawakuta hiyo hasa wadada
 
Alitumia mitishamba
Sijui ni ipi,ni muda mrefu sasa umepita.
Nitajaribu kumuuliza.
Mitishamba gani, haya mambo ni mind set tu, wewe una watoto? Yaliyokutokea ni yapi yanayokupa uzoefu
 
Wewe acha ujinga, naongelea tokana na uzoefu, nina mtoto wa ndugu yangu ninaishi nae ana miaka 11 bado alikua anajikojolea, nikamuuliza mama yake mtoto wako anashida gani mimi siwezi ishi nae, akasema kuna dawa anampa amekua akijikojolea kwa muda mrefu, nikamwambia haiwezekani akaniambia hata kaka yake alifika miaka 12 anakojoa akawa anatumia dawa, ,

nikasema huu ni upumbavu nikaweka mpango kuna siku nikamtegea amekojoa tu nilimchapa sana, na kumpa mkakati akikojoa utalala chini na usiku weka alarm usituke ukakojoe, navyokuambia sasa ana miezi miwili hajajikojolea,
Mkuu nikujibu kistaarabu ingawa umentusi!
Niseme tu kwamba una bahati na ukikojozi wa huyo kijana pia umri wake ulikuwa unaelekea kwenye balekhe ndiyo unajisifu kukomesha kwa kupiga.

Tatizo hilo linatokana na usingizi wa kitoto, akishaangusha kaangusha,haamki na si makusudi, anajistukia tu kaharibu.

Ipo siku utakutana na mtoto kikojozi masalia, utapiga uue lakini kojo lipo pale pale.
Ninadhani kupiga ni kama huduma ya kwanza, lakini si tiba kamili.
 
Hilo ni tatizo walilonao baadhi ya watoto.

Ingawa nimesoma wengi humu wanasema ni kudekeza mtoto ambapo siyo kweli.

Wengi wanaobwabwaja hapa bila kutoa suluhisho wakidhani kuadhibu mtoto ndiyo suluhisho, ujue hao hawajakumbana na vikojozi na hawawezi kufanya lolote.

Kwanza tatizo hilo huwaandama watoto involuntarily kuanzia wakiwa wachanga hadi umri wa balekhe wa miaka 15 na kisha tatizo hilo hukoma na kuondoka lenyewe.

Akiendelea baada ya umri huo nenda hospitali kawaone wataalamu.
Ukweli mtupu!!! Mm binafsi nakumbuka nilikuwa naumwaga mwingi tu, nikiwa na umri huo.

Tena unakuwa katika ndoto ukiwa unacheza na wenzako Kisha unabanwa haja na kuchepuka ukimaliza tu kukojoa unastuka umeharibu.

Ni utoto tu. Hivi sasa ndoto hizo zinakuja lkn nastuka na kubaini Niko ndotoni naamka na kuingia toilet.

Kikubwa sasa mkuu ni kuvaa hali yake kabla ya ww kwenda kulala muamshe akakojoe , kisha baada ya masaa 2 au 3 mwamshe tena lkn pia usichoke kuomba ushauri.
 
Back
Top Bottom