Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Ahsante sana Doctor kwa kutuelewesha vitu kama hivi, ujue kumlaumulaumu sana mtoto na kumsemasema in a negative way kila mara kunampunguzia confidence, anakuwa hajiamini vya kutosha mbele za watu, moto afundishwe na aelimishwe, apewe maneno positive na kuwa uencouraged katika kufanya mambo mazuri katika maisha yake ili ajiamini, sio kumuita mpumbavu, mshenzi, toka utotoni mpaka kuwa mtu mzima, lazima akose confidence na wengine wanakuwa watukutu
 
Tuondoe nidamu ya uoga kwa watoto wetu, tuwafanye wawe na nidhamu ya kweli na wawe karibu na sisi, tuwe na urafiki nao wa karibu ili waweze kutueleza matatizo yao, wajiamini, wasimhofie mtu, wakitueleza matatizo yao na mambo yanayowatatiza tuwasaidie kwa ukaribu mkubwa, tusiwapuuze, ili matatizo yanayowakabili yasiwaharibie maisha yao, yaweza kuwa uonevu shuleni, yaweza kuwa kudhalilishwa kijinsia na Mwalimu wake au mlinzi wa hapo nyumbani.

Wazazi wote wawe karibu na watoto, hata kama Baba anamnyemelea mwanae wa kike, amwambia Mama yake, na Mama asipuuze na kuona ni uongo, alifuatilie na amsaidie mwanae ili asimfanye ajione ambaye hana mtetezi mwingine apart ya Mungu, wakati yeye pia au polisi wapo kwa ajili yake pia
 
Lakini kuna swala la kuweza kurekebisha hali kwa kuongezea tu.

kwa watoto wenye miaka 6> basi waeuke kula vitu aina ya vimiminika baada ya saa kumi na mbili jion. hali hii itamfanya mtoto awe ameshakojoa japo mara 3 kabla ya muda wake wa kulala saa mbili usiku. hii inapunguza kiwango cha mkojo utakao tengenezwa usiku na pia kama mzazi akifanikiwa kumwamsha saa 7 usiku ili akoje basi over time tabia hii itastop.

Ni kweli ulichoelezea kuhusu kuamsha watoto usiku inasaidia sana, binafsi huwa namfanyia hivyo mwanangu wa miaka 3, muda wowote nikishtuka usiku namtoa au ile alfajiri kwa kuwa naamka saa kumi na nusu huwa namtoa maana mara nyingine kumekucha lakini kwa kuwa yu usingizini basi hukojoa nisipomuwahi.
 
Nina binti yangu kwa sasa ana umri wa miaka 14 na anatatizo la kukojoa kitandani wakati akiwa amelala.

Tafadhali ninaomba mnisaidie dawa ya kuzuia tatizo hilo jamani.
 
Hahaha,

Dah!
Mkuu kama una mtoto wako au mtoto wa jamaa yako anakojoa kitandani jaribu dawa yangu itamsaidia inshallah.@Invisible

Invisible nakusubiri leo na kwato lako la ng'ombe......hahahahhahahahahhhhhhhh huyo ndio mzizimkavu aka babu wa loliondo...hahahhahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa mama mbavu zangu zinachomoka....:nerd::spy::yawn:
MziziMkavu Ph.D. Babu wa Jamii Forums hahahahahahah karibuni sana Kwato la Ng'ombe linatibu maradhi mengi tu sio Maradhi ya kikojozi. Kwato la Ng'ombe nikianza kusema faida yake ninafikiri naweza kujaza hii Server ya Jamii forums Jestina
 
Last edited by a moderator:
Kuna mimea inaota maeneo ya mkoa wa kagera, akikojoa usiku unampaka, zinawasha, hapo hatarudia tena make akipatwa na mkojo kisoikologia anakumbuka kuwashwa na hivo anaamka mwenyewe. mmea huo unaitwa'engenyi'

Mkuu engeyi utaua mtoto ni kama *****
 
Naomba kuwauliza wataalamu wa mambo haya, nini kinasababisha mtu mzima mwenye umri mkubwa kuwa na tabia ya kwenda haja ndogo kitandani usiku? Je kuna dawa yoyote ya kumsaidia mtu huyu?
 
Ni kwa nini baadhi ya watu wana umri wa utu uzima lakini wana tabia ya kujisahau wanapolala na wanakwenda haja ndogo kitandani? Ni dawa ipi inaweza kuwasaidia watu hao?
 
Naomba kuuliza hasa madoctor au yeyote mwenye ufahamu,hiv inaweza ikatokea mtu mzima siku moja akakojoa kitandani?nikiwa na maana ya kuwa huwa akojoi kabisa alishaacha tangu utotoni lakni siku moja gafla akakojoa kitandani usku inawezekana au kama ikitokea tatizo huwa nini au ni dalili ya nini? mwenye kujua naomba anisaidie tafadhari.
 
Vp Mkuu umeamka na kujikuta umelimwaga nini kwa bed?
 
Kuna jamaa nilimskia akisema hutokea ukiwa na uchovu (ubongo kuchoka) unapo pumzika ndipo hutokea hyo
 
Huwa inatokea,ila sababu sijui ngoja wataalam waje
 
Wakati mwingine husababishwa na ulevi, pombe ikiingia kwenye mwili huchosha mfumo wa fahamu na kuongeza muda wa kufikiri (REACTION TIME) kwa hiyo ni rahisi zaidi kufanya kitendo chochote ambacho hukutegemea. kama mtu huyo hajalewa sijui kwa nini limetokea hilo! tusubiri ufafanuzi wa wataalamu wengine. Pole
 
Hiyo ni sijawahi kusikia. Hata mtu alewe vipi ataamka asubuhi aone amebanwa na mkojo na sio kukojoa. Hilo litakua ni tatizo
 
WanaJF naomba msaada wenu.

Binti yangu ana miaka 12 yupo darasa la 6. Ana tatizo la kukojoa kitandani. Tumejaribu kila namna lakini bado anaendelea. Tumekuwa tunamuamsha usiku, tumemzuia kunywa maji au kiminika usiku, tumejaribu ndevu za mahindi, maji ya mchele lakini bado. Naombeni msaada wenu kama kuna mbinu au dawa iwe ya kienyeji au kizungu nimsaidie mtoto huyo.

Mungu awabariki
 
Mkuu pole kwa tatizo la kijana kwa umri wake angekuwa kaacha au mara chache. Jaribu mara kwa mara kumuamsha hatimaye atakuja acha.

Nimejaribu kwa mtoto wa miaka 4 unapomusha mara kwa mara anakuwa hakojoi kabisa lakini ukimuacha huwa anakojoa.

Endelea kumuamsha usiku bila kuchoka Mkuu.
 
Back
Top Bottom