Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

WanaJF naomba msaada wenu. Binti yangu ana miaka 12 yupo darasa la 6. Anatatizo la kukojoa kitandani. Tumejaribu kila namna lakini bado anaendelea. Tumekuwa tunamuamsha usiku, tumemzuia kunywa maji au kiminika usiku, tumejaribu ndevu za mahindi, maji ya mchele lakini bado. Naombeni msaada wenu kama kuna mbinu au dawa iwe ya kienyeji au kizungu nimsaidie mtoto huyo. Mungu awabariki

Pole sana.

Nafikiri aliyekupa maarifa ya kutumia ndevu za mahindi alilenga kurekebisha mfumo wa utumaji taarifa kupitia uti wa mgongo. Ikiwa ulifuata vyema dozi ya ndevu za mahindi na bado tatizo lipo, na mmejaribu kumzuia kutumia vimiminaka usiku bila mafanikio, basi kuna moja kati ya haya mawili:

1. Ana kibofu kidogo. Hii issue sijawahi kuisikia kwa wataalam wetu hapa Tanzania lkn somehow ni tatizo. Fanya ulinganifu kwa mtoto mwingine wa umri wake juu ya mara ngapi anakwenda haja ndogo vs binti yako. Ukilibaini hilo, unaweza kujaribu kusolve kwa kufanya hivi:

- Mpe vinywaji vingi sana wakati wa mchana na ajizuie kwenda haja kwa muda mrefu kadiri inavyowezekana. Hii itasaidia kumtanua kibofu endapo itafanyika mara kwa mara kwa miezi kadhaa mfululizo.

NB: Jambo lingine ambalo ningekushauri kufanya, acheni kumsuka nywele huyo mtoto. Mfumo wa fahamu unaathiriwa na kuvutwa nywele. Na hii ni mbaya ikiwa mlianza kumsuka angali mdogo sana

2. Pepo wachafu.
Kuna katabia kako mitaani ka kufanyiana sayansi za ajabu ajabu. Unapokojoa kitandani ktk umri mkubwa, huwa unakosa amani na unaathirika kisaikolojia. Moja kati ya mbinu za Ibilisi kuwakwamisha watoto masomoni ni kuweka mambo mazito akilini mwao, washindwe aidha kulala kwa amani au kusoma.

-Solution kwa hili la pili linategemea imani yako. Ikiwa uko radhi mtoto wako afanyiwe maombi, ni PM nikuelekeze jambo la kufanya na haya matatizo yatakwisha katika jina la Yesu.
 
Pole sana. Lakini kabla sijashauri nataka kujua ni kila siku? Je, anakojoa tena baada ya kumwamsha. Je, ni muda ule ule au unabadilika?
 
Mkuu pole kwa tatizo la kijana kwa umri wake angekuwa kaacha au mara chache
Jaribu mara kwa mara kumuamsha hatimaye
atakuja acha.

Nimejaribu kwa mtoto wa miaka 4 unapomusha
mara kwa mara anakuwa hakojoi kabisa lakini
ukimuacha huwa anakojoa.

Endelea kumuamsha usiku bila kuchoka Mkuu.

Nashukuru mkuu, hilo ndio jambo ambalo tunafanya kwa sasa angalau kumuamsha mara 3 kwa usiku
 
Pole sana...lakini kabla sijashauri nataka kujua ni kila siku? Je, anakojoa tena baada ya kumwamsha... je ni muda ule ule au unabadilika?

Ni kila siku anakojoa, wakati mwingine inatokea hata baada ya kumwamsha, ila muda unabadilika lakini mara nyingi ni kati ya saa 8 usiku na 11 alfajiri.
 
Nakushukuru Mwana Mtoka Pabaya, inawezekana hatukuwa na dozi ya hiyo dawa ya ndevu za mahindi, kama unaifahamu naomba unijulishe nijaribu tena. Pia nitajaribu kufanya hayo uliyonielekeza hilo la kusuka na kupima ukubwa na uhimili wa kibofu chake. Imani kwangu ni jambo jingine. Ninachotaka hili tatizo liishe. Nipo tayari afanyiwe maombi. Tuwasiliane kwa hilo
 
Mkuu.@chamlungu DAWA YA MTOTO KUACHA KUKOJOA KITANDANI:

Dawa ya Kumtibu Mtoto kukojowa Kitandani Vifaa vyake upate hivi:

Upate Kwato La N'gombe tiya ndani yake Kaa La Moto kisha yule mgonjwa wa kukojowa Kitandani alinuse lile kwato la N'gombe lilio na Kaa la Moto ndani yake, kisha Avue nguo zake awe uchi Apande juu ya mti kisha juu ya huo mti akojoe mkojo ushuke chini akisha maliza kukojoa ashuke juu huo mti. Afanye hiyo Dawa kwa Muda wa siku 7 atapona kabisa.

Hakuna dawa Mahospitalini kutibu mtoto kukojowa kitandani. Atumie dawa kisha baada ya siku 7 njoo unipe Feedback.
chanzo. MziziMkavu.
 
Hakikisha usiku hanywi vinywaji kiasi kikubwa aua mkataze kabisa na inapofika saa 6 usiku mwamshe tena akakojoe
 
Nashukuru MziziMkavu kwa dawa uliyoniambia. Anatakiwa afanye mara ngapi kwa siku au aifanye muda gani? Ubarikiwe mkuu
 
Hakikisha usiku hanywi vinywaji kiasi kikubwa aua mkataze kabisa na inapofika saa 6 usiku mwamshe tena akakojoe

Asante Binti Kadogoo, hilo la kumuamsha ndio tufanyalo. Lakini la vinywaji tunajaribu kumdhibiti ingawa nahisi unatuzidi ujanja hasa pale tunapochelewa kurudi kwenye mihangaiko
 
Kigogo wewe nahisi ndio mmoja wa wale wanaojibu sijui kwenye kipima joto bila shaka, kama kitu hujui kaa kimya kuliko kumpa mtu ushauri wa kumkejeli, ingekuwa ndio wewe unauguliwa na binti yako ukapewa ushauri kama huo ungefeel aje? Na yatakukuta tu, kwani kejeli malipo yake ni hapa hapa duniani, jiangalie sana.. Unaboa!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mpeleke CCBRT,anaweza kuwa na tatizo ndani ya mwili la mfumo wa mkojo kwa sabau kuna dada namfaham aliku ana tatizo kama hilo mpaka ukubwani.Alienda pale waka mpima na kumfanyia op aka pona kabisa. Wataalam wakisema hana tatizo lolote la kimaumbile basi usisahau kumfanyia maombi kwa sana ina weza kua kapigwa kipapai (sayansi za Kiafrika).
 
Pole sana.

Nafikiri aliyekupa maarifa ya kutumia ndevu za mahindi alilenga kurekebisha mfumo wa utumaji taarifa kupitia uti wa mgongo. Ikiwa ulifuata vyema dozi ya ndevu za mahindi na bado tatizo lipo, na mmejaribu kumzuia kutumia vimiminaka usiku bila mafanikio, basi kuna moja kati ya haya mawili:

1. Ana kibofu kidogo. Hii issue sijawahi kuisikia kwa wataalam wetu hapa Tanzania lkn somehow ni tatizo. Fanya ulinganifu kwa mtoto mwingine wa umri wake juu ya mara ngapi anakwenda haja ndogo vs binti yako. Ukilibaini hilo, unaweza kujaribu kusolve kwa kufanya hivi:

- Mpe vinywaji vingi sana wakati wa mchana na ajizuie kwenda haja kwa muda mrefu kadiri inavyowezekana. Hii itasaidia kumtanua kibofu endapo itafanyika mara kwa mara kwa miezi kadhaa mfululizo.

NB: Jambo lingine ambalo ningekushauri kufanya, acheni kumsuka nywele huyo mtoto. Mfumo wa fahamu unaathiriwa na kuvutwa nywele. Na hii ni mbaya ikiwa mlianza kumsuka angali mdogo sana

2. Pepo wachafu.
Kuna katabia kako mitaani ka kufanyiana sayansi za ajabu ajabu. Unapokojoa kitandani ktk umri mkubwa, huwa unakosa amani na unaathirika kisaikolojia. Moja kati ya mbinu za Ibilisi kuwakwamisha watoto masomoni ni kuweka mambo mazito akilini mwao, washindwe aidha kulala kwa amani au kusoma.

-Solution kwa hili la pili linategemea imani yako. Ikiwa uko radhi mtoto wako afanyiwe maombi, ni PM nikuelekeze jambo la kufanya na haya matatizo yatakwisha katika jina la Yesu.

Ushauri namba moja ni hatari kiafya, atapata UTI kwa sababu ya urinary retention.
 
mpeleke CCBRT,anaweza kuwa na tatizo ndani ya mwili la mfumo wa mkojo kwa sabau kuna dada namfaham aliku ana tatizo kama hilo mpaka ukubwani.Alienda pale waka mpima na kumfanyia op aka pona kabisa.Wataalam wakisema hana tatizo lolote la kimaumbile basi usisahau kumfanyia maombi kwa sana ina weza kua kapigwa kipapai(sayansi za kiafrika).

Asante sana, nitayafanyia kazi yote uliyonielekeza. Nashukuru kwa msaada wako
 
Habari?nina umri wa miaka 20, bado nasumbuliwa na tatizo la kukojoa kitandani,pia nakojoa mara kwa mara,naomba ushauri.
 
Bedwetting ni tatizo kubwa sana na mara nyingi ni kama "pepo" fulani hivi. Nimeshashuhudia kupitia TB Joshua, wa Emmanuel TV wengi wakitoa ushuhuda wa kuteswa na hali hiyo kwa miaka mingi sana ya utu uzima, wengine hadi miaka 40 naaa...na baada ya kupata huduma ya maombezi "walifunguliwa".

Tafadhali jaribu nawe kwenda ombewa(siyo lazima iwe kwa TB Joshua)nenda popote pale, imani yako yaweza kuponya kwani kawaida hali hiyo huwakuta watoto wadogo tu tena si-wote.
 
Pole sana aise,ebu jaribu kwanza kumtafuta mw/saikologia anaehusika na mental illiness atakusaidia. Ni tatizo katika brain.
 
Back
Top Bottom