Mwana Mtoka Pabaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 15,118
- 16,485
WanaJF naomba msaada wenu. Binti yangu ana miaka 12 yupo darasa la 6. Anatatizo la kukojoa kitandani. Tumejaribu kila namna lakini bado anaendelea. Tumekuwa tunamuamsha usiku, tumemzuia kunywa maji au kiminika usiku, tumejaribu ndevu za mahindi, maji ya mchele lakini bado. Naombeni msaada wenu kama kuna mbinu au dawa iwe ya kienyeji au kizungu nimsaidie mtoto huyo. Mungu awabariki
Pole sana.
Nafikiri aliyekupa maarifa ya kutumia ndevu za mahindi alilenga kurekebisha mfumo wa utumaji taarifa kupitia uti wa mgongo. Ikiwa ulifuata vyema dozi ya ndevu za mahindi na bado tatizo lipo, na mmejaribu kumzuia kutumia vimiminaka usiku bila mafanikio, basi kuna moja kati ya haya mawili:
1. Ana kibofu kidogo. Hii issue sijawahi kuisikia kwa wataalam wetu hapa Tanzania lkn somehow ni tatizo. Fanya ulinganifu kwa mtoto mwingine wa umri wake juu ya mara ngapi anakwenda haja ndogo vs binti yako. Ukilibaini hilo, unaweza kujaribu kusolve kwa kufanya hivi:
- Mpe vinywaji vingi sana wakati wa mchana na ajizuie kwenda haja kwa muda mrefu kadiri inavyowezekana. Hii itasaidia kumtanua kibofu endapo itafanyika mara kwa mara kwa miezi kadhaa mfululizo.
NB: Jambo lingine ambalo ningekushauri kufanya, acheni kumsuka nywele huyo mtoto. Mfumo wa fahamu unaathiriwa na kuvutwa nywele. Na hii ni mbaya ikiwa mlianza kumsuka angali mdogo sana
2. Pepo wachafu.
Kuna katabia kako mitaani ka kufanyiana sayansi za ajabu ajabu. Unapokojoa kitandani ktk umri mkubwa, huwa unakosa amani na unaathirika kisaikolojia. Moja kati ya mbinu za Ibilisi kuwakwamisha watoto masomoni ni kuweka mambo mazito akilini mwao, washindwe aidha kulala kwa amani au kusoma.
-Solution kwa hili la pili linategemea imani yako. Ikiwa uko radhi mtoto wako afanyiwe maombi, ni PM nikuelekeze jambo la kufanya na haya matatizo yatakwisha katika jina la Yesu.