Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Dawa ya Kumtibu Mtoto kukojowa Kitandani Vifaa vyake upate hivi:

Upate Kwato La N'gombe tiya ndani yake Kaa La Moto kisha yule mgonjwa wa kukojowa Kitandani alinuse lile kwato la

N'gombe lilio na Kaa la Moto ndani yake, kisha Avue nguo zake awe uchi Apande juu ya mti kisha juu ya huo mti akojoe

mkojo ushuke chini akisha maliza kukojoa juu ya mti ashuke chini, afanye hiyo Dawa kwa Muda wa siku 7 kila siku Asubuhi mapema sana atapona kabisa.

Mkuu.@
LEE VAN CLEEF TTTumia hii dawa kisha uje hapa unipe Feedback
Mkuu mzizi mkavu nimekuelewa nitafanya hivyo na nitawapa feed back mungu akipenda.
 
Habari wana Jamii Forum,

Mimi ni kijana nimeoa na tuna mtoto mmoja.Tulihangaika na mke wangu kutafuta House girl baada wa yule wa kwanza kuondoka.Tukaja mpata House girl anapiga kazi kweli kweli, ila tatizo anakojoa kitandani usiku.Naomba msaada wenu nini dawa ya kuacha kukojoa kitandani usiku?Na tumemkubali kwa jinsi anavyopiga kazi.

Wenu Kimanga
 
Osha mchele, yale maji ulooshea mchele (ya kwanza ) mpe anywe kila siku, na umwamshe saa kumi na nusu usiku kila siku ataacha, nilikuwa na mjukuu wangu ana matatizo hayo AlhamduliLLAH yameisha kwa dawa hiyo try it.
 
osha mchele, yale maji ulooshea mchele (ya kwanza ) mpe anywe kila siku, na umwamshe saa kumi na nusu usiku kila siku ataacha, nilikuwa na mjukuu wangu ana matatizo hayo AlhamduliLLAH yameisha kwa dawa hiyo try it.

Ushauri mwingine kama nguvu za giza vilee,. Samahani lakini
 
DIABETES INSIPIDUS:Ni ugonjwa unaosababishwa na muongezeko wa mkojo ulochujuka(lita kadhaa kwa siku) ambao husababisha kupatwa na kiu kilichopindukia.​

Ugonjwa huu umegawanyika katika makundi mawili

Nevrogenic diabetes insipidus inatokana na kupungukiwa na antidiuretic hormone(ADH) ambayo huzalishwa/tengenezwa katika ubongo.The main function of the ADH hormone is to maintain the liquid amount in the body by regulating the amount of liquid eliminated from the body.

Ugonjwa huu unaweza kurithiwa.

Nephrogenic diabetes insipidus:Unakuwa na ADH homoni ya kutosha ila mafigo hayareacti ya hio homoni kwahio there wont be regulation of liquid as normal.

Utajuaje kama una ugonjwa huu

Daktari wa mafigo anaweza kufanya vipimo vya mkojo wako ili kuchunguza kama una production ya mkojo ya kawaida.

Dalili za ugonjwa huu:

1.Kuwa na kiu cha kupindukia ambacho kinasababisha ongezeko la kunywa maji/vinywaji ambayo hupelekea kuongezeka kwa hitaji la kupata haja ndogo

Jinsi ya kutibu

1.Kuepuka kunywa maji kabla kulala

2.Kuna dawa inaitwa DESMOPRESSIN ambayo ina hio ADH homoni ili kufidia mapungukio ya hio homoni.

NB:ukishapata mapungufu ya hii ADH homoni utakuwa ni mtegemezi wa dawa maisha.

 
Tatizo hili la kujikojolea bila sababu yoyote ya msingi ni tatizo linaloathiri watu wengi sana na ambalo huleta usumbufu na aibu kubwa kama litampata mtu. Tatizo hili huwakumba sana wanawake kuliko wanaume na inakisiwa kuwa asilimia 35 ya watu walio na umri zaidi ya miaka 60 wana tatizo hili, kati ya hawa wanawake ni mara mbili ya wanaume wanaopata tatizo hili.

Hakuna uhusiano wowote wa tatizo hili na vitendo vya kujaamiiana kinyume cha maumbile au ngono kwa njia ya haja kubwa (anal sex) au ushoga (homosexuality).

Miongoni mwa sababu zinazochangia kutokea kwa tatizo hili ni

  1. Jinsia Hutokea zaidi kwa wanawake kuliko wanaume (stress incontinence), kutokana na ujauzito, kujifungua, wanawake ambao wameacha kupata hedhi (menopausal women) na maumbile ya kawaida ya mwanamke (normal female anatomy), hata hivyo, urinary incontinence huwa zaidi kwa wanaume wenye matatizo ya kwenye tezi dume (prostate) kama saratani ya tezi dume, uvimbe katika tezi dume (BPH) nk.
  2. Umri Kutokana na kuongeza umri, muscle za kwenye kibofu cha mkojo na kwenye mrija wa kupitisha mkojo yaani urethra, zinaanza kuwa legevu (weak) na hivyo kusababisha mtu kushindwa kuzuia mkojo au kujikojolea. Hii haimanishi ya kwamba kila mtu ambaye ana umri mkubwa atapata tatizo hili, la hasha, linaweza kuonekana kwa baadhi tu ya watu wenye umri mkubwa. Mara nyingi huonekana kwa watoto wadogo au wachanga kutokana na kutokukomaa kwa viungo vyao (kibofu cha mkojo na mrija wa kupitisha mkojo)
  3. Uzito uliopitiliza Kuwa na uzito uliopitiliza (obesity) ni moja ya chanzo kinachochangia kutokea kwa tatizo hili kwani uzito huu huongeza presha katika kibofu cha mkojo na kufanya muscle zinazozunguka kibofu hiki kuwa legevu na matokeo yake ni mtu kujikojolea pindi anapopiga chafya au kukohoa.
  4. Uvutaji sigara Kikohozi sugu kinachotokana na uvutaji sigara (chronic cough) pia huchangia kutokea kwa tatizo hili au kuongeza tatizo hili la kujikojolea kama lipo tayari. Kukohoa mara kwa mara, huongeza presha kwenye milango (sphincters) ya mirija ya kupitisha mkojo na hivyo kusababisha tatizo la kujikojolea (stress incontinence). Na hii ndiyo sababu ambayo pia inafanya kuonekana tatizo la kujikojolea kwa wagonjwa wa kifua kikuu, saratani ya mapafu na nk. Uvutaji sigara pia huchochea kwa kibofu cha mkojo kuwa kusisimka kupita kiasi (overactive bladder) kutokana na contractions zinazotokea kwenye kibofu cha mkojo.
  5. Magonjwa mbalimbali kama magonjwa ya figo, kisukari, uvimbe katika tezi dume (BPH), saratani ya tezi dume (prostate cancer) na nk.
Nini chanzo cha tatizo hili?
  • Kukojoa mara kwa mara (polyuria) - Kutokana na magonjwa kama kisukari, kunywa vinywaji kwa wingi (primary polydipsia), diabetes insipidus (central na nephrogenic). Hali ya kukojoa mara kwa mara huongeza hisia ya kutaka kukojoa (urgency) na vipindi vya kukojoa kila wakati (frequency) lakini haileti tatizo la kushindwa kuzuia kujikojolea.
  • Vinywaji vyenye caffeine na cola - Huchochea kibofu kutoa mkojo. (Kibofu ni kiungo cha kuhifadhi mkojo kwa muda tu ndani ya mwili kabla haujatolewa nje).Vinywaji kama soda, chai,kahawa, vinywaji vya kuongeza nishati mwilini (kama redbull nk), hata vinywaji vyenye viungo vingi (spicy) , sukari, na tindikali (acid) nyingi kama citrus na vya nyanya au tungule (tomatoes) pia huchochea kibofu cha mkojo kutoa mkojo.
  • Unywaji pombe Pombe pia huchochea kibofu cha mkojo kutoa mkojo. Unywaji wa pombe kupitiliza huleta mtu kushindwa kuzuia kujikojolea lakini hii inakuwa kwa muda tu, pombe ikiisha mwilini mtu anarudi katika hali yake ya kawaida. Kwa wale ambao wamekuwa addicted na pombe, baada ya kunywa kwa kipindi kirefu ndio huweza kupata tatizo hili.
  • Uvimbe katika tezi dume kwa wanaume wenye umri zaidi ya miaka 40, husababisha tatizo hili la kujikojolea kama BPH, saratani ya tezi dume, nk.
  • Dawa Baadhi ya dawa kama dawa za magonjwa ya moyo, dawa za shinikizo la damu (hypertensive medication), muscle relaxants, sedatives nk husababisha tatizo hili.
  • Tiba ya mionzi Tiba za mionzi za saratani mbalimbali pia husababisha kutokea kwa tatizo la kushindwa kuzuia kujikojolea.
  • Magonjwa mbalimbali kama multiple sclerosis, kiharusi,maambukizi katika mfumo wa mkojo (UTI), kupata choo kigumu (constipation), spina bifida, parkinsons disease na hata maumivu katika uti wa mgongo (spinal cord injury), saratani ya kibofu cha mkojo, ni moja ya chanzo cha tatizo hili.
  • Ujauzito - Baadhi ya wanawake wajawazito na ambao wamejifungua hupatwa na tatizo la stress incontinence kutokana na mabadiliko ya viwango vya vichocheo mwilini (hormonal imbalance) pamoja na kuongezeka uzito kwa mfuko wa kizazi (enlargement of uterus). Stress wakati wa kujifungua kwa njia ya kawaida huleta ulegevu wa muscle zinazohusika kusaidia kibofu cha mkojo katika kazi yake ya kuhifadhi na kutoa mkojo.
  • Tiba za upasuaji - Kama tiba ya kuondoa mfuko wa kizazi (hysterectomy)kutokana na magonjwa mbalimbali pia husababisha tatizo hili kutokana na kibofu cha mkojo na mfuko wa kizazi kuwa karibu ndani ya mwili wa mwanamke, hivyo, muscle na ligament ambazo zinazosaidia mfuko wa kizazi kuuweka katika sehemu yake ndizo pia husaidia kuweka kibofu cha mkojo katika sehemu yake sahihi mwilini.
Aina za tatizo la kushindwa kujizuia kujikojolea (Urinary incontinence)

Kuna aina nyingi za tatizo hili kama zifuatavyo;
  1. Stress incontinence Aina hii ya kujikojolea, hutokea baada ya mtu kukohoa, kucheka, kupiga chafya, kufanya mazoezi au kunyanyua vitu vizito. Stress incontinence hutokea baada ya milango ya kibofu cha mkojo kuwa legevu (sphincter muscles). Huonekana wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua, na wakati mwanamke ameacha kupata hedhi kutokana na umri kuwa mkubwa (menopause). Kwa wanaume, inaweza kutokea baada ya kuondoa tezi dume (prostate).
  2. Urge incontinence Hali inayotokea ghafla ya kuhisi unahitaji kukojoa. Hali hii husababishwa na maambukizi katika mfumo wa mkojo (UTI), kiharusi, alzheimers disease, parkinsons disease, multiple sclerosis, bowel irritants na nk.
  3. Overflow incontinence Hali ya kushindwa kuzuia mkojo kutoka mara kwa mara, mtu kila akijisaidia haja ndogo bado anahisi ya kwamba hajamaliza haja yake hiyo, kwa hiyo kila mara mtu anapata haja ndogo au mkojo unatoka.Hii hutokana na madhara kwenye kibofu cha mkojo (damaged bladder), madhara ya neva kutokana na ugonjwa wa kisukari, multiple sclerosis, maumivu katika uti wa mgongo.Kwa wanaume aina hii, huusishwa na matatizo katika tezi dume kama BPH, saratani ya tezi dume.
  4. Mixed incontinence Katika aina hii, mtu anakuwa na aina zaidi ya moja za urinary incontinence.
  5. Functional incontinence - Hii hutokea pale ambapo mtu anashindwa kwenda chooni kujisaidia haja ndogo kutokana na umri kuwa mkubwa au matatizo mengine ya afya kama kiharusi, ugonjwa wa mifupa aina ya arthritis na nk.
  6. Total incontinence Mtu anaweza kuwa na hali ya mkojo kumtoka bila kuweza kuuzuia kwa wingi muda wote yaani mchana na usiku bila sababu yoyote.
  7. Transient incontinence Aina hii ya mkojo kutoka bila kuweza kuuzuia hutokea kwa muda tu (temporary) na husababishwa na baadhi ya dawa, adrenal insufficiency, mental impairement, au hali ya kushindwa kupata choo kutokana na choo kuwa kigumu sana (stool impaction due to severe constipation).
  8. Giggle incontinence Huwapata sana watoto wadogo wakati wanacheka na mkojo huwatoka ghafla. Mara nyingi mkojo unaotoka hapa unakuwa kidogo sana, na ni hali ya muda tu sio endelevu (temporary). Baadhi ya watoto hujikojolea wakati wapo usingizini na hujulikana kama bedwetting.
  9. Coital Incontinence Ni aina ya kupata haja ndogo wakati wa kujamiana au wakati wa kufikia kilele (orgasm) na inaweza kutokea wakati wa kujamiana kwa mwanamke na mpenzi wake au wakati wa kujichua (masturbation). Huonekana kwa wanawake.
Vipimo vya Uchunguzi

Ugunduzi wa tatizo hili utahusisha daktari kuchukua historia ya mgonjwa ambayo italenga kutambua aina ya dawa anazotumia au ambazo alishawahi kutumia, tiba ya upasuaji yoyote ambayo alifanyiwa hapo awali, ugonjwa wowote alionao mgonjwa, na kama ana historia ya kupata maumivu wakati wa kukojoa au kama anajikamua wakati anakojoa. Pia daktari atamfanyia uchunguzi mgonjwa ili aangalie kama kuna dalili na viashiria vyovyote vya ugonjwa wowote.
Vipimo vya uchunguzi vitahusisha;
  • Vipimo vya damu (Complete Blood Count or FBP) Kuangalia wingi wa damu na chembechembe mbalimbali za damu.
  • Urinalysis Vipimo vya mkojo kuangalia kama kuna mawe katika figo, maambukizi katika njia ya mkojo (UTI) na nk.
  • Ultrasound ya kuangalia figo, kibofu cha mkojo, ureters na urethra.
  • Stress test Hapa daktari anamuhimiza mgonjwa kukohoa wakati huohuo akitazama kama kuna mkojo unaotoka wakati mgonjwa anakohoa.
  • Kipimo cha Cystoscopy Mpira ulio na kamera ndogo kwa mbele huingizwa katika mirija ya kutoa mkojo (urethra) kwa mgonjwa ili kutazama kama kuna matatizo yoyote ndani ya urethra na kwenye kibofu cha mkojo.
  • Urodynamics Vipimo mbalimbali vya kupima presha ndani ya kibofu cha mkojo na presha ya mkojo wenyewe.
  • Postvoid residual measurement (PVR) Mgonjwa anakojoa katika chombo cha kupima wingi wa mkojo, na baada ya hapo daktari hupima kiwango cha mkojo uliobakia ndani kwa kuingiza mpira au catheter katika mrija wa kupitishia mkojo na kuupima baada ya kutoka au anaweza kutumia kipimo cha ultrasound kuangalia kiwango kilichobakia.
  • Cystogram Baada ya kuingiziwa mpira au catheter katika mrija wa kupitisha mkojo mpaka kwenye kibofu cha mkojo, rangi maalum (contrast dye) huingizwa katika mpira huu na mgonjwa hupigwa picha za muda tofauti tofauti za x-ray ili kuangalia kama kuna tatizo lolote katika mfumo wa mkojo.
Tiba ya Urinary Incontinence

Tiba ya Urinary incontinence ni kama ifuatavyo;
  • Kubadilisha tabia ya kujisaidia haja ndogo (kukojoa) kwa
    1. Kufanya mazoezi ya kibofu cha mkojo - Wakati mtu anahisi haja ya kukojoa basi anashauriwa ajizuie kwa angalau dakika 10 halafu ndio aende kukojoa, lengo ni kurefusha zaidi muda huu wa kusubiri kukojoa hapo mbeleni. Au kama mtu akiwa na hisia ya kutaka kukojoa basi anaweza kukojoa kidogo tu halafu asubiri kidogo kabla ya kuendelea tena kukojoa.
    2. Kupanga muda maalum wa kwenda chooni kukojoa na usisubiri mpaka huhisi kutaka kukojoa
    3. Kubadilisha aina ya vinjwaji mgonjwa anavyotumia, kuacha kutumia vinywaji venye caffeine, cola, vinywaji venye viungo vingi (spicy), sukari na tindikali nyingi (acid) kama citrus, carbonated drinks na nk.
    4. Kufanya mazoezi ya pelvic muscles (kegel exercise) kwa kufanya kama unazuia mkojo wakati unahisi haja ndogo na kuhesabu kutoka moja hadi tano, baada ya tano pumzika na halafu rudia. Mazoezi haya huongeza ukakamavu katika sehemu za nyonga pamoja na muscles za nyonga na hivyo kusaidia kuweza kuzuia mkojo.
    5. Electrical stimulation Kwa kutumia electrodes ambazo huingizwa kwenye njia ya haja kubwa kupitia kwenye puru (rectum) au kwenye tupu ya mwanamke (vagina) ili kuchochea na kuleta ukakamavu wa muscles za pelvic au nyonga. Tiba hii huchukua muda mrefu na si tiba ya siku moja na hutumiwa kwa wale wenye stress na urge incontinence.
  • Vifaa maalum vya kusaidia kufyonza mkojo kama absorbent pad, condom catheter (mipira wanaovaa wanaume kama kondomu), chupi maalum (protective underwear), diapers, male urinary incontinence clamp, na nk. Hizi husaidia kufyonza mkojo au kuzuia mtu kujichafua kutokana na kujikojolea (haja ndogo) na hivyo kumuepusha na aibu au usumbufu anaopata mgonjwa.
  • Pessary Ringi maalum ambayo mwanamke huivaa ndani ya tupu yake na hivyo kukisukuma kibofu cha mkojo ambacho kipo karibu na tupu yake juu zaidi na hivyo kuzuia mtu kujikojolea. Ringi hii huvaliwa kwa muda wa siku nzima, na mgonjwa atahitaji mara kwa mara kuitoa na kuisafisha au kama si hivyo basi atakuwa kwenye hatari ya kupata madhara kama maambukizi katika njia ya mkojo, PID (Pelvic Inflammatory Disease) na nk. Ringi hii huwasaidia sana wanawake walio na matatizo ya kuanguka kwa kibofu cha mkojo (prolapse urinary bladder) au mfuko wa uzazi (prolapse uterus).
  • Tiba ya dawa Dawa aina za anticholenergic kama oxybutynin (Ditropan), tolterodine (Detrol) na nk, husaidia kwa wale wenye urge incontinence. Dawa za kupaka aina ya topical oestrogen (cream) husaidia kupunguza dalili za tatizo hili. Imipramine hutumiwa kutibu mixed incontinence. Dawa aina ya Duloxetine inayotumiwa kutibu msongo wa mawazo (antidepressant) pia huweza kutumika kutibu stress incontinence. Ni vizuri kupata ushauri wa daktari pamoja na yeye kukupima kabla ya kuanza kutumia dawa hizi. Mara nyingi ni vigumu kutambua ni aina ipi ya kushindwa kujizuia kujikojolea (urinary incontinence) mgonjwa aliyonayo isipokuwa daktari tu. Tiba za kuchoma sindano kama bulking material injections, Botulin toxin type A injections na nerve stimulators pia hutumika.
  • Tiba ya Upasuaji - Kuna aina mbalimbali za tiba ya upasuaji kama;
    1. Sling procedures Hii hutumia tishu za sehemu nyengine ya mwili wa mgonjwa, synthetic material or mesh ambazo hufungwa kwenye shingo ya kibofu cha mkojo na urethra, na husaidia kufunga urethra wakati mgonjwa anakohoa ama kupiga chafya.
    2. Bladder neck suspensions Hufanywa kutoa msaada kwa urethra na shingo ya kibofu cha mkojo.
    3. Artificial urinary sphincter - Sphincter ya kutengeneza ambayo huvikwa kwenye shingo ya kibofu cha mkojo kwa wanaume walio na sphincter legevu kutokana na tiba ya saratani ya tezi dume au tiba ya uvimbe wa tezi dume (BPH).chanzo.Tatizo la Kushindwa Kujizuia Kujikojolea (Urinary Incontinence)
 
Kwa uelewa wangu mdogo chanzo kikubwa ni ugonjwa wa Kisukari. Muathirika apime sukari mwilini. Ikithibitika an kisukari ani PM nitampatia dawa na atapona tu:smile-big:.
 
Nimepata mengi jamii forums tangu nimeanza kuwa mwanachama. lAKINI LEO NINAOMBA MSAADA WA KIAFYA.Binti wa rafiki yangu anakojoa kitandani na ametumia dawa za Hospital nyingi sana bila mafanikio. Sasa hivi anaingia Form two.Jamani kweli imenitia uchungu shangazi mtu kunielezea na Binti tumeonana leo ni mzuri ambaye amakata tamaa ya kuendelea kusoma kwa maesengenyo ya ndugu zake anaolala nao.Ninaomba nisaideni kama mtu anajua dawa ya kienyeji au tufanye nini binti huyu aache kukojoa usiku akilala akumbuke aamke na aende chooni. ASANTENI KWA MICHANGO YENU
 
Alale na mtu...awe anamuamsha mara kwa mara! Na wakati wa kulala ukikaribia apunguze kunywa vitu vya majimaji.
Hakuna dawa.....ni kuamka tu na kutoa haja ndogo!
Nimewahi kushuhudia hali kama hiyo!
 
Pole sana mpendwa kwa tatizo hili linalomsumbua binti wa rafiki yako kwa ufupi ningependa kukushauri kama ifuatavyo\

1) Kwanza kama alivyoshauri bi JABER JOB kwamba ipo haja ya yeye binti kuepuka kunywa vitu vya majimaji masaa mawili mpaka matatu kabla ya kwenda kulala (hii ni pamoja na juisi maji maziwa matikiti n.k)
2) Kila anapopata fulsa ya kuamka usiku ni lazima aende msalani akakojoe(Kwa kifupi ni kwamba usiku apokuwa amelala ni lazima aamke kukojoa mala mbili kwa usiku mzima)
3)Jaribu kucheza na saikolojia yake ya akili kwa kumdanganya kwa kumfanyia dawa ya miti shamba ambayo itakuwa kama ya kutisha tisha hivi (mfano mtoe nje ya nyumba mtafute mjusi then mzungushie shingoni na kiunoni huku akiimba kwa sauti ya chini "sitaki kukojoa kitandani " baada ya hapo mpeleke chooni mwambie akojoe huku akiwa amefumba macho yaani kama amelala vile ) NAOMBA NIELEWEKE HAPA KWAMBA HII SIO DAWA ILA TU UNAJARIBU KUCHEZA NA AKILI YAKE KWA KUMWAMINISHA KWAMBA HIYO NI DAWA
si vibaya ukiongeza vikolombezo vingine vya kiuganga ganga endapo utaona vinafaa
MWISHO MKUMBUSHE MASHARTI HAYO HAPO JUU MAWILI KWA MSISITIZO SANA KWAMBA ASIYAPUUZE
naamini kwa kufanya hivyo itamsaidia
Alishawahi kufanyiwa hivyo mtoto wa kaka yangu na akapona
 
DAWA YA KUACHA KUKOJOWA KITANDANI

MAANDALIZI


Tafuta Papai bichi moja au mawili au hata matatu,yamenye na uyaanike maganda yake mpaka yakauke siolazima

yakauke kwa sikwa siku moja we yaanike mpaka uhakikishe yanakauka baada ya hapo yakusanye pamoja na

uyaweke katika chombo ambacho unadhani hakita ungua kwa moto kwa muda mfupi mfano bati lolote lile au

hata sehemu iliotengenezwa kwa cement,kisha ya chome mpaka ya badilike na kuwa jivu, baada ya hapo

yakusanye na uyaweke katika chombo safi.

MATUMIZI

Unamrambisha mtoto mdomoni kisha utampa na maji kidogo ili kuondoa radha ya jivu kwa mtoto na kama

anaweza kulamba bila kutumia maji basi itakuwa ni vizuri zaidi, fanya ivyo kwa muda wa wiki moja halafu mchunguze

kama anaendelea kukojoa, kama anaendelea kukojoa nawe endelea kumpa hata kwa wiki mbili hadi tatu na

mtu mzima utafanya hivyo hivyo ila usinywe maji baada ya kutumia dawa bali utakunywa maji baada ya saa 1

kupita Kwa uwezo wa Mwenyeezi Mungu hilo tatizo litaisha. Tumia kisha uje hapa unipe Feedback.@Mbwambo
 
Mwenzetu Dr. MziziMkavu hapo amemaliza kila kitu. Lakini sayansi ya kiarabu inasema kuwa maganda ya papai yana dawa inayosafisha kibofu cha mkojo. Kwa hiyo mtu anayekojoa inaonesha kuwa njia za kibofu cha mkojo haziko sawa.
 
Kingine akienda shule kama ya bweni. Mara nyingi huwa wanarudi wameacha. Kwa maana huwa wanaona aibu kuchekwa na mara nyingine watu wanaojikojolea hutengwa na wenzao.

Nyumbani anachukulia kawaida, maana mmechukulia kama tatizo...aamshwe ni dawa pekee.

Huyu ninayemsemea mimi alikunywa dawa karibu zote ambazo mmeorodhesha. Hazikusaidia,aliacha bila dawa baada ya kwenda bweni kidato cha tano. Ila tangu utoto watu walijua ni tatizo ambalo hawezi pona.
Sasa ni mwaka wa 5 imebaki story!
 
Wadau nina kijana wangu 4 years anakojoa sana kitandani usiku hata mara 3 per usiku mmoja, hata akilala mchana anaweza kuachia kojo, hii si kawaida nini tatizo? nini yaweza kua tiba ?
 
Nimepata mengi jamii forums tangu nimeanza kuwa mwanachama. lAKINI LEO NINAOMBA MSAADA WA KIAFYA.Binti wa rafiki yangu anakojoa kitandani na ametumia dawa za Hospital nyingi sana bila mafanikio. Sasa hivi anaingia Form two.Jamani kweli imenitia uchungu shangazi mtu kunielezea na Binti tumeonana leo ni mzuri ambaye amakata tamaa ya kuendelea kusoma kwa maesengenyo ya ndugu zake anaolala nao.Ninaomba nisaideni kama mtu anajua dawa ya kienyeji au tufanye nini binti huyu aache kukojoa usiku akilala akumbuke aamke na aende chooni. ASANTENI KWA MICHANGO YENU
Hilo tatizo dogo kwangu dawa ya kumponya ipo inaponya hata awe mzee ni pm nikusaidie.
 
Pole mwaya.

Kuna mtoto wa ndugu yangu naye alikuwa anakojoa mpaka high school!ni binti mrembo sana! Yani ilimkosesha confidence akawa anajiona hafai ilimuathiri sana!! Sasa kumbe yeye watu hawakugundua kila jioni hajaenda lala lazima anywe chai na maji,hata asipokunywa chai anakunywa maji mengi. Na kingine alikuwa na tabia ya kubana mkojo mchana! Sasa usiku akishalala anajisahau ndo anamwaga kuanzia la asubuhi!

It was terrible!
Walijitahidi kwa madaktari wakamaliza hela bure! Siku kama Mungu tuu, rafiki wa family yao akaenda kuwatembelea likizo ndo akajua! Akawa anamsaidia mchana ajisaidie ikifika 6pm hakuna kunywa kitu,na ikifika usiku anamwamshaakojoe alifanya kama week the next one akawa amezoea! Fromthere akawa anajisahau once in a while ila after kama week3 aliacha kabisa!
 
Tafuta simu au saa yenye alarm iwe inamuamsha hata mara mbili kwa siku.
 
Back
Top Bottom