Tatizo la kupoteza uwezo wa kunusa (Kutosikia harufu): Fahamu chanzo na namna ya kutibu tatizo hili

Tatizo la kupoteza uwezo wa kunusa (Kutosikia harufu): Fahamu chanzo na namna ya kutibu tatizo hili

mi naenda mwezi sasa....sijui harufu ya kitu...hata nikienda kukata gogo ....najihisi kama pua zimetengeneza filter hivi...napata oxygen harufu nyingine hola.

nilipigwa kamafua ka 5G nikadhani ni hali yangu ya kawaida ,bcoz nina alerg nikapambana kama siku tano mwendo wa piriton,codril na panadol..hali ikaa sawa kidogo baada ya hapo inmepoteza uwezo wa kunusa completely though kwa sasa siumwi wala nini...ila napata mashaka hali yangu ya uwezo wa kunusa itarud lini....kama ni hizi ni moja ya dalili za corona basi wana DSM wengi tuna corona...we have to embrace for impact...
Duuh!! Inatisha hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili gonjwa lipo na linauwa sana ila kwa baadhi linapita tu
Baadhi ya wenye mgogoro wa afya ndio linapita nao mazima
Kufa ni wajib hakuna namna


Sent from my iPhone using Tapatalk
Kabisa mkuu na wenye maradhi like pressure, sukar na hiv aliwaachi salama kabisa na tena aliwap ata dalili hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ulipiga nyungu then hiyo hali ikaanza jua mixer yako ya nyungu ndio iliyokuponza sababu kuna watu wanachanganya madude kwenye kuandaa nyungu hata Korea kaskazini kwa Kiduku mixer yao ya yale madude irudi laboratory. Mseme yote.
 
Mimi nina takribani siku 6 sasa, sijui harufu ya kitu chochote wala sisikii taste ya chochote.

Siumwi homa, wala mafua.
Hii ilitokea gafla tu baada ya kumeza Alu (mseto).
Kuna wenzangu humu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hali hiyo isikupe pressure, relax. Mimi pia takriban wiki mbili zilizopita hali hiyo ilinitokea nikashangaa kwa sababu sijawahi kuexperience tatizo hilo nilikuwa sisikii kabisa harufu hata wife akijipulizia perfume sisikii chochote nikila chakula hata kama kimewekewa viungo sisikii harufu wala taste.Nilijaribu kuuliza rafiki zangu baadhi yao wakawa wananitania oooh! ndio symptoms za COVID-19, wala sikupanic nikawa napiga chai ya tangawizi kaliii na malimao kila siku jioni kwa muda wa wiki moja na result ni nzuri sasa hivi nasikia harufu ya kila kitu hata kikiwa umbali fulani, pia harufu ya dona na samaki naisikia vizuri na nnapokula nafeel ile taste.Kwa hiyo mkuu ondoa shaka ni tatizo la muda tu.Kila jioni pata kikombe cha chai ya tangawizi kali mix na malimao utanipa feedback.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nina takribani siku 6 sasa, sijui harufu ya kitu chochote wala sisikii taste ya chochote.

Siumwi homa, wala mafua.
Hii ilitokea gafla tu baada ya kumeza Alu (mseto).
Kuna wenzangu humu?

Sent using Jamii Forums mobile app


Yani mimi chanzo nilimeza amoxcillin na panadol lkn nilimeza hizi dawa baada ya kuona mwili unaumwa, hasa ktk viungo nikaenda AAR Hospital, wanaona sina ugonjwa wowote, kurudi nyumbani nikawa kuchoka mara kwa mara pua zinakauka lkn sina mafua saiv sina sensing yeyote sasa kuanzia jana na leo ndio angalau at least 45% nina afafhali
 
Yani mimi chanzo nilimeza amoxcillin na panadol lkn nilimeza hizi dawa baada ya kuona mwili unaumwa, hasa ktk viungo nikaenda AAR Hospital, wanaona sina ugonjwa wowote, kurudi nyumbani nikawa kuchoka mara kwa mara pua zinakauka lkn sina mafua saiv sina sensing yeyote sasa kuanzia jana na leo ndio angalau at least 45% nina afafhali
Pole mkuu.
Piga tangawizi mixer na limao na vitunguu swaumu vibrend na ongeza asali kidogo kwenye huo mchanganyiko kunywa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilianza kujisikia vibaya tarehe moja nikawa nahisi kama nina homa kali na kichwa kinauma balaa, nikaenda kupima nikaambiwa niko fresh lakini nikapewa diclopar ili kutuliza maumivu ya kichwa lakini mpaka leo pua zimepoteza uwezo wa kunusa na kutambua kama hapa kuna harufu nzuri au mbaya siku ya tisa leo na chakula sijwahi pata ladha yake toka Siku hiyo mpaka leo yaani nakula tu il nisife

Sent using Jamii Forums mobile app

Ulienda kupima Covid-19 au malaria, typhoid na UTI kama sisi wengine tuliokumbwa na dalili hizo?


Alexander The Great
 
Back
Top Bottom