Ndikwega kabla ya kujaribu baking powder naomba unisikilize.
Nijibu kwanza. Ulishawahi kumwona DR. Bingwa wa sikio, pua na Koo ? Wanaitwa Dr. Wa E.N.T kama bado ni vizuri uanzie kwa daktari. Akishindwa ndo uje upate second opinion hapa.
Nasisitiza mtafute Dr. Bingwa wa E.N.T ila sikushauri uende magomeni kwa yule Dr. Mmasai. Yupo kibiashara zaidi.
Kuna vitu vingi ambavyo huchangia kinywa kutoa harufu mbaya. Aidha uzembe katika kusafisha meno, au bacteria kwenye kinywa au koo au ndani ya pua. Na pengine hiyo harufu inatokea tumboni.
Watu wengi ambao wanasafisha meno vizuri na bado harufu mbaya inatoka wengi hiyo harufu hutoka kwenye koo. Kuna vifuko kwenye koo ambavyo hutunza masalia ya vipande vya chakula na wakati mwingine ukikohoa huwa vinatoka na ukinusa vinatoa harufu Kali sana kama choo.
Chakufanya-. Dr. Anaweza kukupa antibiotic ili kujua tatizo liko wapi na kama tatizo halitoki basi anacheck kwenye hivo vifuko na ikiwezekana utafanyiwa operation ya kuondoa tonsils na huo utakuwa mwisho wa kutoa harufu mbaya.
Dr. Lazima ajiridishe kwamba hiyo harufu mbaya haitoki kwenye meno au pua.
Naandika kwenye simu kama nitakuwa sijaeleweka nisamehe.