Tatizo la lishe duni bado ni kubwa nchini Tanzania.. wananchi wahimizwe kula chakula cha kutosha na sio kutishwa kuhusu vyakula.

Matongee

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2023
Posts
1,056
Reaction score
2,729
Kwa mujibu wa taasisi ya kimarekani ya National Health and Nutrition Examination Survey (NHANES) hadi kufikia mwaka 2016 nchi ya Tanzania ilikuwa ina kiwango cha unene uliopitiliza (Obesity Rate) kwa 8.4% ya idadi ya watu wake. Huku USA ikiwa na 42.1% ya idadi ya watu wake. Hii ni kumaanisha kuwa hadi 2016 kulikuwa na watu 8 kati ya 100 wenye tatizo la unene Tanzania. Huku wamarekani wanne kati ya 10 wakiwa na tatizo la unene.

Pia kwa mujibu wa ripoti za benki ya dunia kwa mwaka 2021 asilimia 23.5 ya idadi ya watu nchini Tanzania walikuwa na tatizo la ukosefu wa chakula cha kutosha (undernourishment). Inamaanisha kulikuwa na watu 24 kati ya 100 waliokuwa wanapata lishe duni. Na hadi 2020 asilimia 34 ya watoto wa chini ya umri wa miaka 5 walikuwa na tatizo la chronic malnutrition nchini Tanzania kwa mujibu wa USAID.

Hizo ni ripoti ambazo ziko mtandaoni na yeyote anaweza kujisomea. Nimeandika huu uzi nikiwa na masikitiko kuona kumeibuka kampeni kubwa ya kuwaaminisha wananchi kuwa kwa sasa hatuna tatizo lolote linalosababishwa na lishe duni ila tuna matatizo yanayosababishwa na matumizi mabaya ya lishe tele iliyopo. Kila mwanaharakati wa afya akiibuka ni kusema kitu fulani msile ni kibaya kwa afya wakati hata hicho anachotaja watu wanakipata kwa kubahatisha.

Ukienda mitaa ya uswazi tatizo kubwa linalowasumbua ni vidonda vya tumbo kutokana na kutopata chakula cha kutosha kwa wakati. Udumavu wa watoto ni mkubwa. Watu wengi tuna maumbo madogo kwa sababu ya kutopata lishe sahihi. Jana waziri wa mifugo kahimiza watu wale na nyama na maziwa ila akaibuka mfuasi wa Mbowe (nyumbu) ndugu Lema na kumpinga kwa kudai angewaona kwanza madaktari kabla ya kuhimiza.

Dr Janabi na wanaharakati wengine ingependeza kama mngeweka nguvu kuhakikisha watanzania wanapata chakula bora. Pongezi za dhati kwa mbunge Neema Lugangira kwa jitihada zake kuhusu lishe.
 
kuna matatizo kama ya nguvu za kijinsia, yamefanya watu kufakamia kila wanachoambiwa ni dawa ya kuongeza nguvu za kijinsia 🐒

vitu vingine ni vichungu na havina hata ladha lakini jamii inashindilia tu, na kuacha kula vyakula bora kwa ajili ya kujenga mwili na kuimarisha afya zao kama ambavyo umeshari kulingana na taarifa ya shirika hilo la kimarekani kuhusu utapia mlo nchini 🐒
 
Kuna tatizo kubwa sana. Wanaharakati ni kero kwa sasa
 
Hao 23% ni maskini, hilo linakuwa ni suala mtambuka

Tunaondoaje umaskini tz?
 
Changanua data zako kwa usahihi. Obesity sio kipimo cha lishe bora.Ni janga
 
Kuna tatizo kubwa sana. Wanaharakati ni kero kwa sasa
ushauri na vitisho kuhusu lishe vya akina Prof.na wengineo lazima kwakweli viangaliwe kwa namna ya tofauti kuhusu kula....🐒

kuna kundi la watu wengi wanasita kula vyakula muhimu kwa afya zao kwa maangalizo na ushauri wenye kutia hofu matokeo yake watu wamedhoofika sana, wengine yupo amesimama tu kituoni kusubiri dalada anaanguka kwa kukosa vitamin na virutubisho muhimu ambavyo aliacha kula kwasabb ya hofu aloipata baada ya kutishwa na wanaharakti.....🐒
 
Back
Top Bottom