Tatizo la LUKU limerudi tena

Tatizo la LUKU limerudi tena

Ni kweli kuna Tatizo kubwa sana kwenye mfumo wa Luku.

Makamba, bodi Mpya ya Tanesco na Management mpya ya Tanesco wanatakiwa kujua kuwa kuna vita kubwa sana dhidi yao! Wanatakiwa kujipanga na kuwa makini sana!

Mifumo ya Kielectronic iliyoundwa kipindi cha Jiwe inatakiwa isimamiwe na watu wapya na sio watu walewale walioiunda kipindi kile. Au ibadirishwe na kuwekewa mifumo mingine ya usimamizi
 
Ni siku ya pili sasa kuna tatizo kubwa ya Luku. either kwa kununua kwa njia ya mitandao ama kwa wakala wao.... Waziri mpya tulijua umeingia kuongeza kasi kumbe mambo ni yale yale...
 
Huyu waziri ndo hakuna kitu kabisa

991D62AA-6034-4302-9500-4318AF6748C1.jpeg
 
Ni siku ya pili sasa kuna tatizo kubwa ya Luku. either kwa kununua kwa njia ya mitandao ama kwa wakala wao.... Waziri mpya tulijua umeingia kuongeza siku ya pili sasa kuna tatizo kubwa ya Luku. either kwa kununua kwa njia ya mitandao ama kwa wakala wao.... Waziri mpya tulijua umeingia kuongeza kasi kumbe mambo ni yale yale...
Nishida, japo nitatizo la mifumo
 
Wewe upo mkoa gani? Mbona hakuna tatizo la luku mkuu,

Anyway si mkubali Makamba tangu akiwa waziri wa teknolojia na habari enzi za mkwere.
Mkuu kuna tatizo. Niko Moshi nimejaribu kununua Luku toka saa 1 asubuhi imeshindikana.

Nimempigia Tanesco wanasema kuna tatizo linashughulikiwa na makao makuu. Haijulikani itachukua muda gani kurekebisha.
 
Nami niko Arusha,najaribu kununua umeme tangu asubuhi ya leo. Nimejaribu kwa m pesa na kupitia benki imeshindikana.
 
Ni kweli kuna Tatizo kubwa sana kwenye mfumo wa Luku.

Makamba, bodi Mpya ya Tanesco na Management mpya ya Tanesco wanatakiwa kujua kuwa kuna vita kubwa sana dhidi yao! Wanatakiwa kujipanga na kuwa makini sana!

Mifumo ya Kielectronic iliyoundwa kipindi cha Jiwe inatakiwa isimamiwe na watu wapya na sio watu walewale walioiunda kipindi kile. Au ibadirishwe na kuwekewa mifumo mingine ya usimamizi
Incompetence yenu mnasingizia watu walioshika ofisi kabla. Mmetoa management yote haya sasa toeni hadi wafagizi msipate kisingizio.
 
Jana Geita hakukuwa na umeme! Hasa karumwa na nyang'hwale yote!
Mkuu wasalimie karumwa hapo ingia na kijiji cha Gamashi waambie nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Nyang'hwale
 
ivi kipindi kile wanunuzi walirudishiwa fedha/tokeni kwa manunuzi walofanya?
 
Ni kweli kuna Tatizo kubwa sana kwenye mfumo wa Luku.

Makamba, bodi Mpya ya Tanesco na Management mpya ya Tanesco wanatakiwa kujua kuwa kuna vita kubwa sana dhidi yao! Wanatakiwa kujipanga na kuwa makini sana!

Mifumo ya Kielectronic iliyoundwa kipindi cha Jiwe inatakiwa isimamiwe na watu wapya na sio watu walewale walioiunda kipindi kile. Au ibadirishwe na kuwekewa mifumo mingine ya usimamizi
Msipende kuharalisha kila uzembe ni hujuma, yaani kila kiongozi akiingia abadirishe mfumo kisa kukwepa hujuma?tatizo la tanesco ni kubwa mno, zaidi ya utendaji, na ndio maana unaona sasa kila sehemu ni kilio tu kwa wateja wapya wa umeme, kisa vifaa hakuna, hapo waziri anafanya nini?sasa wewe mtumishi wa kawaida uanze kufanye hujuma kwa serikali hii kisa ulikuwa mfuasi wa marehemu, hiyo ni akili?ukifukuzwa kazi hayati atakusaidia??na matatizo ya tanesco ni mengi mno ya miaka na miaka usitegemee kuyamaliza kwa wakati mmoja, na kama awamu ya tano ndio waliyazidisha kabisa kwani walikuwa wanatumia tu matamko ya kisiasa bila uhalisia!!na hakuna kitu kinawaumiza vichwa kama huu utaratibu wa sasa wa kuunganisha umeme kwa 27, 000!!kwani hiyo tofauti serikali hawapeleki!!
 
Nakumbuka mara ya mwisho tatizo la kununua umeme wa luku kwenye simu waziri kalemani aliwaamuru tanesco waachane na kampuni ya kigeni inayosimamia mfumo wa luku.

Leo kumezuka tena shida sijui sehemu zingine. Kwetu tangu asubuhi mfumo wa simu wanasema wamesimama kwa muda tatizo eti liko tanesco.

Isiwe ni mipango haramu ya kuihujumu tanesco kuhalalisha njama za wapigaji wa mali ya umma kutaka shirika libinafsishwe.
 
Jumatano wamekata umeme bila taarifa kwa masaa 12, Alhamis hivyo hivyo bila taarifa, Jumapili wakatoa taarifa.

Jumatatu siruhusiwi kununua Luku hadi saa 9 alasiri. Hivi watanipa hela ya kula mwisho wa mwezi? Hawajui kuwa Kuna watu umeme ndio maisha yetu!?
 
Nakumbuka mara ya mwisho tatizo la kununua umeme wa luku kwenye simu waziri kalemani aliwaamuru tanesco waachane na kampuni ya kigeni inayosimamia mfumo wa luku...
Ngoja tuone wakisimamisha chumi zao kwanza
 
Back
Top Bottom