Amina Thomas
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 272
- 130
Jamani naomba nitoe tahadhari na hii dawa. Kitunguu saumu ni dawa sana ya Kushusha presha. Unaweza kushusha presha kwa kutumia punje za kitunguu saumu. Na kama presha yako iko chini halafu ukala kitunguu saumu kibichi ujue utaishusha zaidi. Hii ilimtokea mama yangu. Alishauriwa anywe maji yaliyolala na punje 8. Yeye akaponda ili ifanye kazi haraka. Du! Tusingepata akili ya kumpa kahawa ingekua hatari maana presha ilishuka sana. Kwa hiyo nashauri mtu kabla hajatumia, acheki kwanza presha yake.