Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

MziziMkavu, asante sana, ngoja niianze leo jioni, ila nlishawahi kupaka kitungu saumu maeneo hayo ila niliona mabadliko kidogo ila badae hali ikarudi vilevile.
 
Last edited by a moderator:

mara ngapi kwa siku aisee mheshimiwa Dr
 

Jaribu na kuogea testimol soup made in india.

Tafuta kipande cha ndimu upake...
Kila siku.unapoenda kulala.
 
mara ngapi kwa siku aisee mheshimiwa Dr
mkuu paty Kila siku Asubuhi kabla ya kula kitu tumie hiyo Dawa kisha ukae kama saa moja ndio waweza kunywa chai na chakula kwa siku mara moja inatosha Mkuu. Kama una maradhi makubwa tumia kwa muda wa wiki moja tu inshallah matatizo yako yatakwisha Akipenda Mwenyeezi Mungu.
 
MziziMkavu, dozi ntumie kwa mda gan sabb hili tatzo ni la miaka mitatu sasa.
Mkuu Bray hii dawa ni ya Kienyeji kwa sababu umeumwa miaka mingi na umetumia dawa nyingi hujapona ninakushauri utumie Dawa mpaka upone ninafikiri kwa nguvu ya kitunguu samu huwezi hata kufikisha siku 15 utakuwa umeshapona jaribu kisha uje hapa kueleza je umepona au bado? Give Me feedback.

Faida za Kiafya za Kitunguu Swaumu (Garlic) Featured



Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.


Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen'genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.


Historia inaonesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika China mwaka 510 K.K na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Roma. Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana.


Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza kutumika kama dawa ya kusafishia vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza na pili ya dunia. Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa kwa kutumia jamii hii ya vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo (mouth wash) ingawa watumaiji wake wengi huilalamikia dawa hiyo kwa sababu ya harufu mbaya ya dawa hiyo inayowasababishia kunuka kwa mdomo.


Faida za vitunguu swaumu


Katika tafiti mbalimbali vitunguu swaumu vimeonekana kuwa na uwezo wa kutibu maambukizi ya bakteria, fangasi na virusi vya aina mbalimbali. Aidha husaidia kuzuia magonjwa ya moyo ikiwemo kuondoa lijamu katika mishipa ya damu na hivyo kusaidia katika kurekebisha shinikizo la damu. Faida nyingine za vitunguu swaumu ni pamoja na
  • Kutibu saratani ikiwemo saratani ya tumbo na utumbo mkubwa. Tafiti zinaonesha idadi ndogo ya wagonjwa wa saratani katika nchi ambazo wakazi wake wana utamaduni wa kutumia vitunguu swaumu kwa wingi.
  • Vitunguu swaumu husaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu. Hata hivyo inashauriwa kwamba wagonjwa wa kisukari wanaotumia sindano za insulin wasitumie kitunguu swaumu kwa wingi mpaka watakaposhauriwa na daktari.
  • Huzuia kusanyiko la chembe sahani zinazosaidia kuganda kwa damu (platelet aggregation)
  • Husaidia ufyozwaji wa thiamin, hivyo kusaidia kuepusha mwili na ugonjwa wa beriberi
  • Ina kiasi kikubwa cha vitamini C ambayo husaidia kuzuia ugonjwa wa kiseyeye
  • Hutumika kutibu magonjwa nyemelezi kama toxoplasmosis, hasa kwa watu wenye upungufu wa kinga mwilini.

Ushahidi wa Kitafiti


Katika utafiti uliofanyika nchini Czech ilionekana kuwa matumizi ya vitunguu swaumu yalisaidia sana katika kupunguza kusanyiko la lijamu (cholesterol) pamoja na mafuta yasiyofaa mwilini (low density

lipoproteins)
katika mishipa ya damu. Aidha, mwaka 2007 BBC iliripoti matumizi ya vitunguu swaumu katika kusaidia kumkinga mtumiaji dhidi ya aina fulani ya mafua iliyosababishwa na virusi. Mwaka 2010,

ulifanyika utafiti mwingine ambao ulijumuisha wagonjwa 50 wenye shinikizo la damu sugu ambalo lilikuwa ni vigumu kudhibitiwa hata kwa matibabu yaliyozoeleka ya dawa na njia nyingine. Kama njia ya

kuchunguza ufanisi wa vitunguu swaumu katika kutibu shinikizo la damu, baadhi ya wagonjwa hao walipewa vitunguu swaumu wakati wengine walipewa dawa isiyohusika na matibabu ya shinikizo la damu

(au placebo). Ilionekana kuwa wale waliopewa vitunguu swaumu kama dawa ya shinikizo la damu walionesha maendeleo mazuri kwa vitunguu swaumu kuweza kushusha vizuri kiwango cha shinikizo la damu, hususani systolic pressure, tofauti na wale waliopewa placebo.


Nini siri ya kitunguu swaumu?






Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;
  • Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
  • Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
  • Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
  • Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo inayotolewa baada ya kuvila.
 
Last edited by a moderator:
Asante sana mzizimkavu, na vipi kuhusu kupaka mchanganyiko wa kitungu saumu na limao, naweza kupaka au niache tu.
 
natamani kuitumia dawa hii lkn nilipopima presha ilikuwa imeshuka ngoja kesho nikapime tena
 
BAOSITA nimepima pressure imekuwa 94/63
je, naweza kutumia dawa hii?
 
Nafuu uliyopata inaitwa "placebo effect."

Asilimia 99 ya Watanzania hawajawahi kusikia kitu kinachoitwa "placebo effect."

Nchi ya watu ma-primitive tulionyimwa elimu, masikini weee, yani inaniuma kweli kweli nchi yangu.

Sijui ukiwa atheist unakuwa kama umelogwa vile,unabaki kukariri tuuuuuuu. kwa sababu huamini katika kitu chochote kisicho cha kiwandani, wewe mpaka uone tembe kwenye ganda la brister ndiyo unaona ni dawa inayoponya,nje ya hapo uponyaji ni wa ki placebo effect,mwenyewe unajiona mjanja kwamba umekariri neno placebo effect...
 
nashukuru kk nitaitumia kwa kutuelimisha. kwanza dawa ni rahisi kupatikana, pili ni pesa kidogo ambapo kila mmoja anweza kuimudu, tatu haina kemikali ambazo ni hatari kwa miili yetu. Thank u very much!!!!
 
nilisumbuliwa na Fangasi na nikatumia Hii Dawa
Sasa mambo yamejipa, sina tena mabaka ya fangasi

Ila Wazee Mwenzenu Nakula Sana na Ninachukua Chakula Kingi Sana Mpaka Kushiba, sasa sijui tatizo nini hapo
Ahsanten!
 
nilisumbuliwa na Fangasi na nikatumia Hii Dawa
Sasa mambo yamejipa, sina tena mabaka ya fangasi

Ila Wazee Mwenzenu Nakula Sana na Ninachukua Chakula Kingi Sana Mpaka Kushiba, sasa sijui tatizo nini hapo
Ahsanten!
labda ulikuwa na minyoo nayo imekufa coz dawa inatibu na minyoo
 
Heshima kwanza Dk..!
Nina mpwa wangu ana tatizo la fangasi ktk vidole vya miguu yake, yaani kila akitumia dawa fangasi zinaisha lakini baada ya muda kidogo zinarudia tena je tiba yake halisi hapa ni dawa gani? Kwani ni mda mrefu sasa bado hili tatizo haliishi akiacha kuvaa viatu fangasi zinapotea akivaa zinarudi tena, na sasaivi tena ndio anaishi Uarabuni na uanajua tena kulivyo na joto ndio haziponi kabisaa. Naomba msaada tafadhali.
 

hii ndio tiba,kabla ya kuvaa viatu awe anapaka miguu mafuta pamoja na vidole,apake mafuta tu ya kawaida,hizo fungus atakuwa anazisikia tu kwa watu,usipopaka mafuta lile joto na msuguano ndio uleta fungus,fanya kama nilivyokueleza harafu uje kutoa ushuhuda nina uhakika asilimia zote atapona
 
je mafuta hupunguza joto? nenda pharmacy kanunue antifangal!!
 
BAOSTA
Shukrani kwa elimu nzuri..What a useful thread !!
GOD BLESS YOU and I mean it.
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru mkuu..!!
Nitajaribu kufuata huo ushauri wako aksante sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…