Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

ebane ni dawa hata kama miguu ilikuwa inatema zinde chafu ukinywa tuu hata demu wako ataweza kuku kiss miguuni
 
Habari zenu wadau.Nimeona nitoe elimu hii hapa kwa sababu ni watu wengi sana wanaosumbuliwa na minyoo na fungus sugu kila maeneo kuanzia miguuni mpaka sehemu nyeti!Hii imekuwa kero sana.Haijalishi umezunguka hospitali ngapi bila kupata nafuu.Cha kufanya ni:-

Nunua kitunguu swaumu.Menya chote kama vile uandaavyo kwa ajili ya kupikia.Twanga ama saga,vikishasagika changanya na maji ya uvuguvugu kidogo kipimo cha kijiko cha chai ili vilainike.Chota msagiko wote wa vitunguu na uvimeze.
Tahadhari,jitahidi uwe na mfuko ama sehemu ya maliwatoni maana kama hauna tumbo zuri unaweza tapika.(Mara chache sana hutokea kutapika)

Ukishakaa kama dk 15 hali yako itarudi kawaida.Baada ya SIKU 1,utaona minyoo hakuna tena na fungus wote wamekauka!Kwisha kabisa!!!!

Pia kama una presha ya kushuka usitumie hii dawa maana huwa inashusha sana presha,labda unywe na kahawa baada ya kuinywa dawa hii ili kuipandisha tena presha!

Msisite kuja kutoa ushuhuda wenu hapa wakuu.Ni hayo tu.

Wakuu,

Kama unajijua wewe ni weak usjaribu kuitumia hii dawa, itakuondoa. Nilifanya kama tulivyoelekezwa hapa, lakini baada ya kunywa ukweli nilijisikia kufa kufa, nilikosa nguvu na kujisikia kutapika lakini sikutapika. Niliamua kuitumia kwa ajili ya kuua minyoo. Nashindwa kutoa ushuhuda hapa kwani sina uhakika kama kweli minyoo imekufa!!!!!

Tiba
 
Baosita naomba nikupe cheo cha Dr. Asante sana na hii dawa ni kweli asiyekubali na akae kimya. Kitunguu saumu kinatibu mambo mengi sana ikiwemo minyoo sugu na fangasi! Turejee natural therapies na side effect za madawa zitateupuka.
 
BAOSITA hebu rudi jamvini kwanza, hii dawa nimetumia inafanya kazi kwakweli, ila sasa nilikuwa na tatizo la appetite kwa sababu mimi si mlaji sana ila tangu nimetumia hii dawa sasa nakula kama Farasi, namaanisha kula hasa, sasa hakuna dawa nyingine ya kudailuti hii? maana hii ni hatari sasa.
 
Last edited by a moderator:

Nimerudi wakuu.Kuongezeka kwa hamu ya kula nadhani inatokea kutokana na aina ya minyoo uliyokuwa nayo awali.Nahisi hapo awali kabla hujanywa hii dawa ulikuwa unakula kwa kiwango cha chini sana.Tukumbuke kuna minyoo wasababishao njaa sana na wengine wasababishao shibe na kupoteza hamu ya kula.Sasa usishangae,tuambie kwanza mwanzo ulikuwa unakula vipi.
 
Last edited by a moderator:
Ahsanteni kwa wote mlioitumia dawa na kurudi hapa jamvini kutoa 'feedback'.Naona maswali mengine yanajirudia sana wakati nilishayajibu hapo awali.Kwa yeyote mpya anayetaka kuijaribu hii tiba,naomba ajaribu kusoma majibu yangu yote ndani ya uzi huu kuanzia mwanzo.Ukiona mtu anakuja hapa kubisha kwamba hii dawa haifanyi kazi,jua kwamba hajawahi umwa fangasi huyo,anakuja tu kukebehi watu hapa.Kwahiyo tujaribu kuwapuuza watu wa namna hiyo kwani hawajengi bali wanabomoa.
 
Mkuu BAOSITA uko sahihi kabisa, mwanzoni nilidhani mipombe ndio inanifanya kukosa hamu ya kula na hivyo kupelekea kula kidogo, lakini tangu nimepiga hii dozi nakula kama Farasi hata hapa ninapotype sasa hivi nimetoka Pub kupombeka na nikabeba take away ya chips na kuku nusu na maji makubwa ya Kilimanjaro na nimefuta vyote na maji nimepiga yote lita 1.5. zamani haikuwa hivi friji yangu ilikuwa haikosi viporo vya jana nikirudi nimepombeka nakula kidogo na kuacha.

Ahsanteni kwa wote mlioitumia dawa na kurudi hapa jamvini kutoa 'feedback'.Naona maswali mengine yanajirudia sana wakati nilishayajibu hapo awali.Kwa yeyote mpya anayetaka kuijaribu hii tiba,naomba ajaribu kusoma majibu yangu yote ndani ya uzi huu kuanzia mwanzo.Ukiona mtu anakuja hapa kubisha kwamba hii dawa haifanyi kazi,jua kwamba hajawahi umwa fangasi huyo,anakuja tu kukebehi watu hapa.Kwahiyo tujaribu kuwapuuza watu wa namna hiyo kwani hawajengi bali wanabomoa.
Wajinga wajinga huwa hawakosekani, kwenye kila msafara wa mamba na kenge wamo. Nimeiproval hii dawa ni ya kweli na kwangu nimepata matokeo positive. No more Albendazole, situmii tena madawa ya hospital ambayo most of them ni fake product from India. Ubarikiwe.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Baosita hiyo dawa inatibu hata amoeba nini? Leo hii nimeifakamia dawa asubuhi mapema wakati sijala wala kunywa kitu chochote na nimeshinda kutwa nzima bila kugusa chakula wala kinywaji hadi jioni. Nilipokunywa nilijisikia vibaya kwa dakika chache hivi kisha tumbo liliungurima kwa dakika chache na baada ya hapo niliiza kupata hali njema isiyo ya kawaida. Hivi nimavyoandika, ninaandaa vitunguu vingine ili kesho asubuhi nitwange tena na kunywa. Nachopenda kujua ni je hii dawa inasaidia pia na amoeba? Nauliza hivyo kwa sababu amoeba imenisumbua muda mrefu na dalili zilizokuwepo awali zimetoweka baada ya kunywa vitunguu swaumu.
 
  • Thanks
Reactions: ARV
Babu wa Loliondo ameingiaje hapa? amekukosea nini?
Usidhihaki waBongo, mbona walikunywa mpaka hao unaowalamba Mikundu?
angalia TB Joshua TV utaona mpaka hao mabwege wenzio wanaenda!
kuna vingine viko beyond human capacity! na usicheze na hisia za watu
waliokwisha kupoteza matumaini kwa sababu yoyote iwayo!
let them be!
By the way what have you???:shut-mouth:

Bora nipate 'sifa za kijinga' lakini zikasaidia kuamsha jamii ya Watanzania wenzangu, kwamba jamani eeeh, tuanze kuondokana na waganga wa vitunguu na matabibu wa kienyeji! Tujijengee uwezo wa kieledi wa karne ya 21.

Hapana, baba yako peke yake hawezi kuwa kigezo cha "ningeona matokeo yake"! Ilibidi uchukue baba yako na wajomba zako na ukoo wenu mzima na majirani na ushee mle "dawa" na wengine wanywe placebo na wengine wawe control group na mpimwe kwa muda unaorekodiwa kieledi. Vinginevyo observation yako ni ya ki "profesa maji marefu"!

Bora mimi niliechelewa kujua kuliko mamilioni ambao mpaka leo hawajui, ndo maana akitokia kibabu kimoja ambacho kuandika jina lake hajui akawaambia amewagundulieni dawa ya kutibu kila ugonjwa basi Watanzania wote rrrrrrrrrr... kwa kibabu!... placebo effect ikiisha mnaanza kukisakama kibabu kiwalipe!.... kizazi kilichonyimwa elimu, a wasted generation!

Jamani, zaidi ya hisabati hakuna somo ambalo kila Mtanzania lazima alisome mpaka Form IV, isipokuwa Biology, lakini watu kwa mamilioni bado hawaelewi the basic fundaments of microbes and diseases.... kizazi cha babu wa Liliondo, mnaenda kupewa dawa ya kipindupindu na minyoo halafu mkiwa kwenye foleni kusubiri dawa mnalala pembeni ya kinyeshi na inzi halafu wagonjwa wote wenye kuhara na kutapika wanakunywa dawa kwenye kikombe hicho hicho! dawa nini? maji ya imani! A primitive generation!
 
Mkuu Baosita hiyo dawa inatibu hata amoeba nini? Leo hii nimeifakamia dawa asubuhi mapema wakati sijala wala kunywa kitu chochote na nimeshinda kutwa nzima bila kugusa chakula wala kinywaji hadi jioni. Nilipokunywa nilijisikia vibaya kwa dakika chache hivi kisha tumbo liliungurima kwa dakika chache na baada ya hapo niliiza kupata hali njema isiyo ya kawaida. Hivi nimavyoandika, ninaandaa vitunguu vingine ili kesho asubuhi nitwange tena na kunywa. Nachopenda kujua ni je hii dawa inasaidia pia na amoeba? Nauliza hivyo kwa sababu amoeba imenisumbua muda mrefu na dalili zilizokuwepo awali zimetoweka baada ya kunywa vitunguu swaumu.
Ahsante.Ndio inatibu mpaka Amoeba mkuu!Pia ukiwa na ulcers ya tumboni inayosababishwa na bacteria nayo huponyesha!Nasema hivi kwasababu kuna watu zaidi ya 4 ninaowafahamu wamepona ulcers na Amoeba pia!
 
unaowalamba Mikundu?
Hili suala la "kulamba mikundu" naomba niliruke tafadhali, naona kama halina uhusiano na suala zima la kupambana na magonjwa na waganga wa kutumia viuongo pamoja na hoja yangu kuhusu kusambaziana elimu ya jamii kuhusu germs and diseases.

angalia TB Joshua TV utaona mpaka hao mabwege wenzio wanaenda!
Siamini superstition, siwezi kuangalia TB Joshua TV!

Babu wa Loliondo ameingiaje hapa? amekukosea nini?
Babu wa Liliondo ndio hawa waganga wa vitunguu na vikombe vya miujiza! Ni matokeo ya kizazi kilichokosa upeo, kilichonyimwa elimu. Huwezi kuwa na dawa ya kipindupindu wakati unalala hapo hapo unapojisaidia wakati umepanga foleni unasuburi dawa, unakula hapo hapo na vinyesi, huwezi kupona! Wote hawa, vibabu vya imani, waganga wa vitunguu, wachawi, uponyaji kupitia TV ya TB Johua , lazima tuelimishane, tuwapige vita.

Usidhihaki waBongo, mbona walikunywa mpaka
Ninajali wabongo wa nchi yangu, ndio maana naeleza ukweli, kwamba, jamani eeh, huwezi kusema kitunguu kinaua bacteria kwa sababu eti baba yako alikunywa akapona, unajuaje kitunguu ndio kilimponya? Unajuaje baba yako alikuwa na bacteria? Bacteria yupi? Madaktari wa kienyeji sasa tunasema mmepitwa na wakati.

kuna vingine viko beyond human capacity!
Nini kiko beyond human capacity, ku control imani za kichawi na waganga wa vitunguu?

na usicheze na hisia za watu waliokwisha kupoteza matumaini kwa sababu yoyote iwayo!
let them be!
Ndio, mmepoteza matumaini kwa sababu mmekumbatia mawazo ya Zinjanthropus na elimu duni. Sijacheza na hisia za mtu, nimeeleza kwa udhati mkuu, kwamba ni wakati sasa wa kuondokana na imani potofu.

By the way what have you???:shut-mouth:
"What have you" ndio nini?
 
Hili suala la "kulamba mikundu" naomba niliruke tafadhali, naona kama halina uhusiano na suala zima la kupambana na magonjwa na waganga wa kutumia viuongo pamoja na hoja yangu kuhusu kusambaziana elimu ya jamii kuhusu germs and diseases.

Siamini superstition, siwezi kuangalia TB Joshua TV!

Babu wa Liliondo ndio hawa waganga wa vitunguu na vikombe vya miujiza! Ni matokeo ya kizazi kilichokosa upeo, kilichonyimwa elimu. Huwezi kuwa na dawa ya kipindupindu wakati unalala hapo hapo unapojisaidia wakati umepanga foleni unasuburi dawa, unakula hapo hapo na vinyesi, huwezi kupona! Wote hawa, vibabu vya imani, waganga wa vitunguu, wachawi, uponyaji kupitia TV ya TB Johua , lazima tuelimishane, tuwapige vita.

Ninajali wabongo wa nchi yangu, ndio maana naeleza ukweli, kwamba, jamani eeh, huwezi kusema kitunguu kinaua bacteria kwa sababu eti baba yako alikunywa akapona, unajuaje kitunguu ndio kilimponya? Unajuaje baba yako alikuwa na bacteria? Bacteria yupi? Madaktari wa kienyeji sasa tunasema mmepitwa na wakati.

Nini kiko beyond human capacity, ku control imani za kichawi na waganga wa vitunguu?

Ndio, mmepoteza matumaini kwa sababu mmekumbatia mawazo ya Zinjanthropus na elimu duni. Sijacheza na hisia za mtu, nimeeleza kwa udhati mkuu, kwamba ni wakati sasa wa kuondokana na imani potofu.

"What have you" ndio nini?
Unaweza kudharau tiba hizo kwa maneno ya kashfa kwa lugha yoyote na matusi ya kila aina lakini mwisho wa siku haitasaidia kitu maana kuumwa ni zaidi ya hayo unayoongea. Zamani nilikuwa na tabia kama yako ya kudharau tiba za asili au tiba mbadala kwa lugha hiyo hiyo kwamba ni kwa sababu ya kukosa elimu tena basi elimu tunayodhani ndiyo elimu ni hiyo iliyoletwa na wazungu; ya biology, chemistry, physics, n.k. Lakini mwisho wa siku yalinikuta na kuhitimisha kwamba tiba mbadala zipo na zinafanya kazi. Nitatoa mifano miwili.

Kwa muda mrefu sana nilikuwa nasumbuliwa na vidonda vya tumbo. Nilipima Akghan Dar es Salaam mara mbili na kwa kutumia vipimo viwili tofauti wakadhihirisha kuwa nilikuwa na ulcers na hali ilikuwa mbaya sana. Nilianza kutumia dawa za kutibu na kkumaliza kila dozi ninayopewa na kuzingatia masharti ya madaktari kuhusu vyakula lakini tatizo liliendelea na mbaya zaidi nilikuwa nahisi maumivu makali zaidi kadri siku zinavyoenda. Ilifika wakati nashindwa hata kufanya kazi ofisini kutokana na maumivu makali ya ulcers. Mwishoni mwa mwaka juzi nilishauriwa niende Nairobi ili nipimwe na ikiwezekana nifanyiwe operation kubwa kwani wakati huo hata nikitembea nilikuwa nahisi natonesha kidonda kilichotokana na kuungua kwa maji ya moto hivi. Nikiwa katika harakati za kujikusanya kufedha ili niende Nairobi, nilishauriwa na rafiki yangu mmoja nijaribu dawa za kimasai.

Pamoja na dharau yangu dhidi ya dawa za kienyeji, ilibidi niwatafute wamasai kwa hali niliyokuwa nayo. Nilienda Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha Ubungo na kukutana na mmasai mmoja ambaye nae alinipeleka kwa rafiki Mwenge nikapata dawa. Ilikuwa ni dawa ya maji kidogo sana na niliambiwa moja ya ingredient zake ni mafuta ya mkia wa kondoo. Nilionywa nisizidishe kipimo kwani ni kali sana. Nilipofika nyumbani nilitulia mpaka nikahisi vidonda vimeanza tena kuuma ndipo nilipokunywa hiyo dawa. Nilitapika sana tena sana mpaka nikahisi labda dawa imenidhuru. Hiyo ilikuwa jioni. Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka takribani mitano, niliamka nikiwa na najisikia mwenye nguvu na mauvimu japo yalikuwepo, yalikuwa kwa umbali sana. Baada ya kunywa chai nusu saa baadaye nilikuwa yena hiyo dawa na sikutapika kabisa. Nilirudia hiyo dawa mara tatu na hivi navyoandika vidonda vya tumbo sina na nimepima mara kadhaa ikadhihirika pasipo shaka kuwa sina ulcers. Siku hizi nakula chochote kilicho mbele yangu bila kupata shida yoyote.

Mfano wa pili ni pumu. Kwa muda mrefu sana shemeji yangu mke wa kaka yangu alikuwa anasumbulikuwa sana na pumu kiasi cha sisi ndugu zake kukata tamaa. Ilifika wakati shemeji yangu popote aendapo lazima atembee na mtu akiwa na dawa ya kushusha pumu ikiwa ni pamoja na bomba za sindano. Shemeji alikuwa akitembea inakuwa kama mnywa gongo kwa jinsi anavyonyanyua mabega juu. Maisha yalikuwa ya kukata tamaa kwani pamoja na uwezo mkubwa wa kaka yangu kifedha uliomsaidia kutafuta za kila aina kwenye mahospitali mbalmbali, bado haikusaidia. Siku moja nikiwa ofisini nilikuwa nasimulia watu muujiza ulioniwezesha kupona ulcers na kuwaeleza kwamba kamwe sitasharau tena tiba mbadala, mama mmoja akaniambia kwamba na yeye alikuwa na pumu lakini alipona kimiujiza hivyo hivyo. Nilipopata taarifa hiyo nilimwomba anielekeze alikopata hiyo tiba na gharama zake. Aliniambia eti ni mbali itabidi nisubiri mpaka ndugu zake watakapopata fursa ya kutoka huko kuja Dar. Mahali kwenyewe ni Urambo Tabora.

Sikutaka kusubiri. Nikamwambia yule mama kwamba akinielekeza hata kesho yake ningeanza safari ya kwenda Urambo kutafuta hiyo dawa. Bahati nzuri katika fukuafukua yake, yule mama alibahatika kusikia kwamba kuna mtu anayemfahamu alikuwa ana safari ya kuja Dar. Kwa hiyo, tulimtumia hela kwa mtandao na akaenda kwa jamaa anayeandaa dawa na akaja nayo Dar. Bei yenyewe ilikuwa Sh. 15,000 tu! Kama ilivyotokea kwangu, shemeji alipokunywa hiyo dawa jwa mara ya kwanza alitapika sana kiasi cha kuishiwa nguvu. Ilibidi tumpeleke hospitali awekewe drip la dawa ya kumpatia nguvu. Kumbe tulikuwa tumekosea masharti. Ilitakiwa kabla ya kuinywa dawa ale chakula na kushiba masaa matatu kabla. Sisi hatukuzingatia hilo. Kesho yake alikunywa tena na hakutapika. Aliendelea kunywa kwa muda wa wiki moja. Hivi navyoandika, unakaribia mwaka sasa shemeji yangu ni mzima wa afya na tangu wakati huo pumu haijamshka tena na kwa kudhihirisha hilo hata mafuta ya kupakaa, pyafumu na vitu vingi ambavyo alikuwa hadiriki hata kuvisogelea, sasa hivi anavitumia. Madawa yote ya kisasa aliamua kutupa jalalani.

Kutokana na mifano hiyo miwili, siwezi kubeza hata kidogo tiba mbadala. Waache watu wanaoteseka wajaribu bahati yao maana uzima au uhai ni kitu muhimu sana. Siyo rahisi mtu kubeza na kudharau tiba mbadala kama tiba zinazoaminika za kisasa zimeshindwa kumwondolea tatizo.
 
Hili suala la "kulamba mikundu" naomba niliruke tafadhali, naona kama halina uhusiano na suala zima la kupambana na magonjwa na waganga wa kutumia viuongo pamoja na hoja yangu kuhusu kusambaziana elimu ya jamii kuhusu germs and diseases.

Siamini superstition, siwezi kuangalia TB Joshua TV!

Babu wa Liliondo ndio hawa waganga wa vitunguu na vikombe vya miujiza! Ni matokeo ya kizazi kilichokosa upeo, kilichonyimwa elimu. Huwezi kuwa na dawa ya kipindupindu wakati unalala hapo hapo unapojisaidia wakati umepanga foleni unasuburi dawa, unakula hapo hapo na vinyesi, huwezi kupona! Wote hawa, vibabu vya imani, waganga wa vitunguu, wachawi, uponyaji kupitia TV ya TB Johua , lazima tuelimishane, tuwapige vita.

Ninajali wabongo wa nchi yangu, ndio maana naeleza ukweli, kwamba, jamani eeh, huwezi kusema kitunguu kinaua bacteria kwa sababu eti baba yako alikunywa akapona, unajuaje kitunguu ndio kilimponya? Unajuaje baba yako alikuwa na bacteria? Bacteria yupi? Madaktari wa kienyeji sasa tunasema mmepitwa na wakati.

Nini kiko beyond human capacity, ku control imani za kichawi na waganga wa vitunguu?

Ndio, mmepoteza matumaini kwa sababu mmekumbatia mawazo ya Zinjanthropus na elimu duni. Sijacheza na hisia za mtu, nimeeleza kwa udhati mkuu, kwamba ni wakati sasa wa kuondokana na imani potofu.

"What have you" ndio nini?
Inaonekana hujawahi kuugua kisawasawa au hujauguliwa kisawasawa. Hongera sana.
 
Nashukuru sana mtoa maada umenisaidia maana nilikuwa na fungus wa miguu mpaka nashindwa kuvaa viatu ila baada ya kutumia tu 5 days naona maendeleo makumba

Ubarikiwe sana kwa msaada wako
 
Nimekula ila nackia kufa kufa!!daah!mpk nimeshindwa kuimalizia yote
Pole sana mkuu.Kama nilivyoeleza,inabidi kuimeza yote mara moja kwa haraka bila kusikilizia ladha!Ukimeza kwa kubeep itakushinda tu.
 
Nashukuru sana mtoa maada umenisaidia maana nilikuwa na fungus wa miguu mpaka nashindwa kuvaa viatu ila baada ya kutumia tu 5 days naona maendeleo makumba

Ubarikiwe sana kwa msaada wako
Ahsante sana,na wewe ubarikiwe kwa kupona kabisa!
 
nameza pamoja na yale sijui ndio machicha yake au naweza isaga tu alaf nikanywa mchuzi wake tu
 
Back
Top Bottom