Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

Habari JF DOCTORS,

Nisaidieni kwa mda sasa nimekuwa nikisumbuliwa na ugonjwa wa fangasi ya makende kiasi kwamba yakianza kuwasha ni shidaa yanawaka ka moto vile.

Nshajaribu sabuni za rungu, protector, na detal ya maji lakn sijapona.

Jamani, msaada kwa anayejua dawa ya hili tatizo manake linanikosesha raha kwakweli.
 
Try gentriderm cream ...paka usiku na asubuhi baada kuoga...inauzwa 3000 famas... but mie sio doctor...
 
Tumia Quandriderm cream, ina combination ya dawa aina 4., ila chunguza chanzo cha hao fungus. Tuliosoma Pugu enzi hizo tunaelewa vizuri what it mean by fungal itching.
 
Tumia Quandriderm cream, ina combination ya dawa aina 4., ila chunguza chanzo cha hao fungus. Tuliosoma Pugu enzi hizo tunaelewa vizuri what it mean by fungal itching.

Nahisi ni joto lilizidi manake hali hii ilinipata miez miwili nyuma nlipotembelea dar kwa mda, tatizo likaanzia hko
 
Hakikisha unavaa chupi za cotton, safi na zinaanikwa juani. Utomvu wa aloe vera unaponyesha haraka sana. Otherwise nenda hospitali, kuna dawa ambazo sio nzuri kutumia maeneo hayo (zina steroids)
 
weka /paka limau kila baada ya kuoga,pia hakikisha unajikausha vizuri kila baada ya kuoga uwe mkavu!
 
Kaka huo ugonjwa ni mbaya sana na hapo Kama una demu utamuambukiza na ni mbaya sana akipata mwanamke.dawa ya kwanza nunua dezor shampoo paka kwa siku 3,alafu anza dozi ya diflu gram 150 na microdox doxycycline nunua amol-G ya kupaka.angalizo chupi badilisha kila siku na ukiweza pasi kabla hujavaa taulo jitaid uwe Nazo hata 3.
 
Kaka huo ugonjwa ni mbaya sana na hapo Kama una demu utamuambukiza na ni mbaya sana akipata mwanamke.dawa ya kwanza nunua dezor shampoo paka kwa siku 3,alafu anza dozi ya diflu gram 150 na microdox doxycycline nunua amol-G ya kupaka.angalizo chupi badilisha kila siku na ukiweza pasi kabla hujavaa taulo jitaid uwe Nazo hata 3.

Nashukuru tena swala la pasi muhimu
 
mimi mwenyew ni victim wa hao fungus kama miaka miwili nyuma, ila nilipona baada kutumia antibiotics jina inaitwa Griseofulvin unatumia kidonge kimoja kwa siku, dozi ni 30 pills, unatakiwa kuwa mvumilivu kidogo coz inalegeza na inaleta njaa sana. Tembelea pharmacy iliokaribu nawe, if symptoms persist see the doctor.
 
Hili suala la "kulamba mikundu" naomba niliruke tafadhali, naona kama halina uhusiano na suala zima la kupambana na magonjwa na waganga wa kutumia viuongo pamoja na hoja yangu kuhusu kusambaziana elimu ya jamii kuhusu germs and diseases.

Siamini superstition, siwezi kuangalia TB Joshua TV!

Babu wa Liliondo ndio hawa waganga wa vitunguu na vikombe vya miujiza! Ni matokeo ya kizazi kilichokosa upeo, kilichonyimwa elimu. Huwezi kuwa na dawa ya kipindupindu wakati unalala hapo hapo unapojisaidia wakati umepanga foleni unasuburi dawa, unakula hapo hapo na vinyesi, huwezi kupona! Wote hawa, vibabu vya imani, waganga wa vitunguu, wachawi, uponyaji kupitia TV ya TB Johua , lazima tuelimishane, tuwapige vita.

Ninajali wabongo wa nchi yangu, ndio maana naeleza ukweli, kwamba, jamani eeh, huwezi kusema kitunguu kinaua bacteria kwa sababu eti baba yako alikunywa akapona, unajuaje kitunguu ndio kilimponya? Unajuaje baba yako alikuwa na bacteria? Bacteria yupi? Madaktari wa kienyeji sasa tunasema mmepitwa na wakati.

Nini kiko beyond human capacity, ku control imani za kichawi na waganga wa vitunguu?

Ndio, mmepoteza matumaini kwa sababu mmekumbatia mawazo ya Zinjanthropus na elimu duni. Sijacheza na hisia za mtu, nimeeleza kwa udhati mkuu, kwamba ni wakati sasa wa kuondokana na imani potofu.

"What have you" ndio nini?

Unaweza kudharau tiba hizo kwa maneno ya kashfa kwa lugha yoyote na matusi ya kila aina lakini mwisho wa siku haitasaidia kitu maana kuumwa ni zaidi ya hayo unayoongea. Zamani nilikuwa na tabia kama yako ya kudharau tiba za asili au tiba mbadala kwa lugha hiyo hiyo kwamba ni kwa sababu ya kukosa elimu tena basi elimu tunayodhani ndiyo elimu ni hiyo iliyoletwa na wazungu; ya biology, chemistry, physics, n.k. Lakini mwisho wa siku yalinikuta na kuhitimisha kwamba tiba mbadala zipo na zinafanya kazi. Nitatoa mifano miwili.

Kwa muda mrefu sana nilikuwa nasumbuliwa na vidonda vya tumbo. Nilipima Akghan Dar es Salaam mara mbili na kwa kutumia vipimo viwili tofauti wakadhihirisha kuwa nilikuwa na ulcers na hali ilikuwa mbaya sana. Nilianza kutumia dawa za kutibu na kkumaliza kila dozi ninayopewa na kuzingatia masharti ya madaktari kuhusu vyakula lakini tatizo liliendelea na mbaya zaidi nilikuwa nahisi maumivu makali zaidi kadri siku zinavyoenda. Ilifika wakati nashindwa hata kufanya kazi ofisini kutokana na maumivu makali ya ulcers. Mwishoni mwa mwaka juzi nilishauriwa niende Nairobi ili nipimwe na ikiwezekana nifanyiwe operation kubwa kwani wakati huo hata nikitembea nilikuwa nahisi natonesha kidonda kilichotokana na kuungua kwa maji ya moto hivi. Nikiwa katika harakati za kujikusanya kufedha ili niende Nairobi, nilishauriwa na rafiki yangu mmoja nijaribu dawa za kimasai.

Pamoja na dharau yangu dhidi ya dawa za kienyeji, ilibidi niwatafute wamasai kwa hali niliyokuwa nayo. Nilienda Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha Ubungo na kukutana na mmasai mmoja ambaye nae alinipeleka kwa rafiki Mwenge nikapata dawa. Ilikuwa ni dawa ya maji kidogo sana na niliambiwa moja ya ingredient zake ni mafuta ya mkia wa kondoo. Nilionywa nisizidishe kipimo kwani ni kali sana. Nilipofika nyumbani nilitulia mpaka nikahisi vidonda vimeanza tena kuuma ndipo nilipokunywa hiyo dawa. Nilitapika sana tena sana mpaka nikahisi labda dawa imenidhuru. Hiyo ilikuwa jioni. Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka takribani mitano, niliamka nikiwa na najisikia mwenye nguvu na mauvimu japo yalikuwepo, yalikuwa kwa umbali sana. Baada ya kunywa chai nusu saa baadaye nilikuwa yena hiyo dawa na sikutapika kabisa. Nilirudia hiyo dawa mara tatu na hivi navyoandika vidonda vya tumbo sina na nimepima mara kadhaa ikadhihirika pasipo shaka kuwa sina ulcers. Siku hizi nakula chochote kilicho mbele yangu bila kupata shida yoyote.

Mfano wa pili ni pumu. Kwa muda mrefu sana shemeji yangu mke wa kaka yangu alikuwa anasumbulikuwa sana na pumu kiasi cha sisi ndugu zake kukata tamaa. Ilifika wakati shemeji yangu popote aendapo lazima atembee na mtu akiwa na dawa ya kushusha pumu ikiwa ni pamoja na bomba za sindano. Shemeji alikuwa akitembea inakuwa kama mnywa gongo kwa jinsi anavyonyanyua mabega juu. Maisha yalikuwa ya kukata tamaa kwani pamoja na uwezo mkubwa wa kaka yangu kifedha uliomsaidia kutafuta za kila aina kwenye mahospitali mbalmbali, bado haikusaidia. Siku moja nikiwa ofisini nilikuwa nasimulia watu muujiza ulioniwezesha kupona ulcers na kuwaeleza kwamba kamwe sitasharau tena tiba mbadala, mama mmoja akaniambia kwamba na yeye alikuwa na pumu lakini alipona kimiujiza hivyo hivyo. Nilipopata taarifa hiyo nilimwomba anielekeze alikopata hiyo tiba na gharama zake. Aliniambia eti ni mbali itabidi nisubiri mpaka ndugu zake watakapopata fursa ya kutoka huko kuja Dar. Mahali kwenyewe ni Urambo Tabora.

Sikutaka kusubiri. Nikamwambia yule mama kwamba akinielekeza hata kesho yake ningeanza safari ya kwenda Urambo kutafuta hiyo dawa. Bahati nzuri katika fukuafukua yake, yule mama alibahatika kusikia kwamba kuna mtu anayemfahamu alikuwa ana safari ya kuja Dar. Kwa hiyo, tulimtumia hela kwa mtandao na akaenda kwa jamaa anayeandaa dawa na akaja nayo Dar. Bei yenyewe ilikuwa Sh. 15,000 tu! Kama ilivyotokea kwangu, shemeji alipokunywa hiyo dawa jwa mara ya kwanza alitapika sana kiasi cha kuishiwa nguvu. Ilibidi tumpeleke hospitali awekewe drip la dawa ya kumpatia nguvu. Kumbe tulikuwa tumekosea masharti. Ilitakiwa kabla ya kuinywa dawa ale chakula na kushiba masaa matatu kabla. Sisi hatukuzingatia hilo. Kesho yake alikunywa tena na hakutapika. Aliendelea kunywa kwa muda wa wiki moja. Hivi navyoandika, unakaribia mwaka sasa shemeji yangu ni mzima wa afya na tangu wakati huo pumu haijamshka tena na kwa kudhihirisha hilo hata mafuta ya kupakaa, pyafumu na vitu vingi ambavyo alikuwa hadiriki hata kuvisogelea, sasa hivi anavitumia. Madawa yote ya kisasa aliamua kutupa jalalani.

Kutokana na mifano hiyo miwili, siwezi kubeza hata kidogo tiba mbadala. Waache watu wanaoteseka wajaribu bahati yao maana uzima au uhai ni kitu muhimu sana. Siyo rahisi mtu kubeza na kudharau tiba mbadala kama tiba zinazoaminika za kisasa zimeshindwa kumwondolea tatizo.
Mwachieni huyu Anheuser pumzi zake za uzima ndizo zinazo mdanganya uzima wake ndio unaomfanya awe jeuri atavuna kile alicho kipanda .

Inaonekana hujawahi kuugua kisawasawa au hujauguliwa kisawasawa. Hongera sana.
Tunamngojea huyu mkuu Anheuser aje siku moja akiumwa dawa za hospitali zimeshindikana aje kuomba ushauri wetu tutampa ushauri wetu wa Negative badala ya Positive tunakusubiri kwa hamu wewe lete jeuri yako kwa watu wanaotumia dawa za asili Tiba mbadala utakuja kututafuta siku moja.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mwenye fungus wa hayo maeneo ni wewe au? Natanguliza pole
 
Jamani, mwenzio kauliza dawa...

Hahahaha...haya mkuu. Twende kaaz....

dawa.jpg
 
Ahsanteni kwa elimu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Watanzania fungus za sehem za Siri si rahisi kuzitibu kwa kupaka ant fungal lazima umeze dawa tafadhali Kama unataka kupona nunua dawa hizi doxicisiline pamoja na fluconazole ya gram 150 zote ziko kwenye blista utapona kabisa
 
Back
Top Bottom