Wakuu,
Tunaomba ushauri wenu, kwa wale ambao specialists wa magonjwa haya ya ngozi. Tunauliza hivi kwa niaba ya watu wengi ambao wamekuwa wanahangaika kupata suluhu ya matatizo haya ya MBA, Fangasi na mabaka (hasa kwenye sehemu za siri, yakiwemo mapaja).
Shukrani
Tafadhari tunaomba ushauri wenu:
A. Kuhusu Fungus za sehemu za siri:
Zinatibiwa vipi au na dawa gani? Mdau anadai amefanya yafuatayo mpaka sasa:
1. Kunyoa muda wote
2. Kukausha vizuri kwa taulo baada ya kuoga
3. Kutumia gentriderm ya kupaka.
Na ameona kuwa akitumia gentriderm zinapona lakini baada kama ya wiki zinarudi.
B. Mabaka:
Je, kuna dawa ya mabaka ya usoni, mgongoni, kifuani na sehemu nyingine za mwili?
C.Mba:
Dawa ya mba please? (Tunafahamu kuna mjadala juu ya MBA tu hapa =>
Ujue ugonjwa wa Mba na Tiba yake
NB:
Kwa kila moja ya dawa utajazo hapo juu tuambie kama mtoto anaweza kutumia, na kama hawezi; ni umri gani unashauriwa?
Je, kwa magonjwa hayo kuna dawa za mitishamba pia, ni zipi, zinatumikaje na dosage yake ikoje.
===========
Similar Cases:
==========
MASWALI MUHIMU:
==========
Walionufaika na ushauri wa wadau: