Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

futurestar hebu kuja hapa eleza vizuri gonjwa yako pia jinsia yako.

Je wewe ni Mke au Mme?

Hao fangus ni wa nje?

Au ikiwa wewe Mke, Je, hao fangus ni wa ndani au nje?

Unataka kusaidiwa basi jitahidi kujieleza watu wakuelewe vyema vinginevyo utaishia kupata majibu ya juu juu tu na hautafanikiwa kuitibu.

USHAURI.

Ikiwa fangus wanaosumbua ni wa nje bila kujali wewe ni Mke au Mme, fanya yafuatayo

1. Hakikisha haufugi nywele sehemu za siri kwani zinatunza uchafu na majimaji
2. Hakikisha sehemu za siri ni safi muda wote.
3. Hakikisha sehemu za siri ni kavu muda wote.
4. Hakikisha unaoga asubuhi na jioni na kisha kausha na paka dawa sehemu hizo za siri. Nashauri utumie FUNGIFENG
5. Kama wewe ni Mme acha tabia ya kuparamia wanawake ovyo leo huyu kesho yule unaokoteza fangus
6. Kama wewe ni Mke acha tabia ya kuparamia wanaume ovyo kwani unaokoteza fangus
7. Hakikisha chupi unazovyaa ni kavu na safi muda wote, ikiwa wewe ni Mke unaweza badilisha mara 2 kwa siku
8. Usiku unaweza usivae chupi ukavaa bukta au nguo za kulalia pekee, hii utaruhusu maeneo nyeti kupata hewa
9. Chup ikivaliwa mara moja ifuliwe, usirudie. haijalishi wewe ni mwanaume au mwanamke.

Kwa uchache ni hayo tu.

Kama ni fangus za ndani, mimi sina majibu.

Asante kk.
Hawa fangas wapo nje
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Bill hiyo FUNGIFENG inapatikana wapi na ikoje mkuu??? Msaada tafadhali
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Bill hiyo FUNGIFENG inapatikana wapi na ikoje mkuu??? Msaada tafadhali

GlorytoGod FUNGIFEN ina cover la blue na maandishi ya njano kama sikosei. Inauzwa kati ya shs 1,500 hadi 2,000. Tube yake pia ni ya blue na maandishi ya njano au meupe hivi.

Nenda famas yoyote uulize watakupatia.
 
Last edited by a moderator:
Jamani msaada mimi nasumbuliwa na punye kwnye mkono yaani linaweka shilingi natumia dawa ya kupaka linaisha then linarudi.
Naomba msaada wenu pls
 
usafi ni muhimu sana. hasa kunawishi mwili wako kwa maji safi na medicated soap. nguo pia zifuliwe zingae na zianikwe juani pia kama inawezekana piga pasi na usivae nguo moja kwa mda mrefu kwan inahitaj nayo kupumzika. maeneo ya siri yaache ya pumue na usivae nguo zenye kubana. jitahipi upepo upite. nguo zetu za ndani, machupi hakikishen zinakua saf za ziko za kutosha ikishindikana hapo. tumia cosmetics, nenda hospitalini. utapewa dawa
 
Jamani kuna mtu anajua dawa ya Fangasi yaani Pumbu zinauma na zimekua nyekundu kama nyanya msaada please!

Mwanzo nilikua natumia sabuni ambazo ni Medicated sana kama Protex na Detol baada ya kuacha naona hali ni mbaya nahitaji tiba ambayo itanisaidia kutibu niweze kutumia hata sabuni za Kawaida ambazo siyo medicated Suala la kuacha sabuni na Ugonjwa kurudi nimegundua kuwa sijapona.

Nahitaji tiba.

Naoamba Kuwasilisha.
 
Umenikumbusha mbali sana. Wakati nipo form 4 kuna dogo alikuwa form 3..huyo dogo alikuwa hajipendi sana haswa kwenye swala la usafi. Kuoga na kufua nguo kwake ilikuwa ni shida kubwa sana.

Matokeo ya uchafu wake yali pelekea huyo dogo kupata huo ugonjwa wa " PUMPU JERO".

Nakushauri, wekeza nguvu nyingi kwenye usafi wa mwili. Boxer moja usizae zaidi ya siku mbili.
 
Jamani kuna Mtu anajua dawa ya Fangasi yaani Pumbu zinauma na Zimekua nyekundu kama nyanya msaada please! Mwazo nilikua natumia Sabuni ambazo ni Medicated sana kama Protex na Detol baada ya Kuacha Naona hali ni mbaya nahitaji tiba ambayo itanisaidia kutibu niweze kutumia hata sabuni za Kawaida ambazo siyo medicated Suala la kuacha sabuni na Ugonjwa kurudi nimegundua kua sijapona.........na nahitaji tiba.

Naoamba Kuwasilisha.

Unapatikana mkoa gani nikuelekeze hospitali ya kwenda kuchekiwa na kupatiwa matibabu.
 
Umenikumbusha mbali sana. Wakati nipo form 4 kuna dogo alikuwa form 3..huyo dogo alikuwa hajipendi sana haswa kwenye swala la usafi. Kuoga na kufua nguo kwake ilikuwa ni shida kubwa sana.
Matokeo ya uchafu wake yali pelekea huyo dogo kupata huo ugonjwa wa " PUMPU JERO".

Nakushauri, wekeza nguvu nyingi kwenye usafi wa mwili. Boxer moja usizae zaidi ya siku mbili.

Usafi mbona ninao kadri inavyotakiwa.
 
Jamani kuna Mtu anajua dawa ya Fangasi yaani Pumbu zinauma na Zimekua nyekundu kama nyanya msaada please! Mwazo nilikua natumia Sabuni ambazo ni Medicated sana kama Protex na Detol baada ya Kuacha Naona hali ni mbaya nahitaji tiba ambayo itanisaidia kutibu niweze kutumia hata sabuni za Kawaida ambazo siyo medicated Suala la kuacha sabuni na Ugonjwa kurudi nimegundua kua sijapona.........na nahitaji tiba.

Naoamba Kuwasilisha.

Mkuu, humu kuna uzi unaoelezea matumizi ya vitunguu saumu kama tiba ya fangasi, tafadhali u-"search". Mimi nimefaidika nao saana.
 
Pole sana ww usumbuliwae na fungus, dawa sahii itakayokusaidia ni NYSTATIN ,GRISEOFULVIN or AMPHOTELICIN, njisi ya kutumia dawa na muda gan utatumia dawa hyo, utapewa maelezo ktk pharmac utayoenda kununua dawa, ama piga 0758152000 my no. to get more infor free.
 
Back
Top Bottom