Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

Wakuu

Habari zenu ,nilikuwa naomba kujua mwenye kujua dawa ya fangus, huku chini, kwenye korodani aisee kuna washa sana, hadi kuna unga unatoka kabisa, nilikuwa nasikia watu wanaita korodani erosion sasa naona hali si hali.

Mwenye kujua dawa nzuri kabisa ya kutumia iwe kupaka au ya kunywa, naomba kujua.

Uzi tayari
 
Pole sana mkuu, tumia dawa inaitwa (Clotrimazole+Gentamycin +Betamethasone ) ,wengine huiita Gentrisone cream na Vidonge FluconazoleTabs 150mg everyday for 14 days
 
Kabla ya tiba fanya mabadiliko ya tabia.
Ukitoka kuoga kausha sehemu yote vizuri na taulo. Taulo ulifue mara kwa kwa mara na sabuni na ulianike juani. Kama utaweza uwe na taulo la sehemu yenye ugonjwa tu.

Vaa pichu/boxer za cotton na ufue na sabuni usirudie pichu/boxer siku mbili.

Muone daktari na udumu kwenye matibabu kwa muda mrefu. Ikiwezekana hata miezi sita.
 
TAFUTA TERBINAFINE CREAM hii hatarii sanaa..!! Hutaitaji hata dawa za vidonge lakini cha muhimu Ukiogaa futaaa hukoo mzeee...boxer sio unavaa siku nne...!!
 
Pole sana mkuu, tumia dawa inaitwa (Clotrimazole+Gentamycin +Betamethasone ) ,wengine huiita Gentrisone cream na Vidonge FluconazoleTabs 150mg everyday for 14 days
Asante mkuu

Nimenunua candistat

Naanza nayo nione Kama itasaidia
 
hello, za jumapili na za ibaada kwa ujumla.
naombe nieleze kwa kifupi dawa iliyonisaidiakupona fagasi baada ya kuteseka nazo kwa zaidi ya miezi sita na kutumia dawa nyingi bila mafanikio...
pamoja na kwamba dawa hii inatibu mmba na fagasi zote ila mimi nijikite kwenye sehemu za siri za mwanaume kwa maana ya makorodani na maumbile yake...
habari nzuri ni kwamba dawa hii inagharim haizidi 1500tsh ya kitanzania,
iko hivi, lotion ya vestline alovera 70g ambayo inauzwa sh. 500, sijajua eneo ulilopo.. halafu chukua dawa ya septline vidonge viwili vipondeponde au visage halafu changanya unga wa hiyo dawa kwenye lotion koroga hadi ujilidhishe kuwa imechanganyikana vizuri, halafu...hapo dawa yako tayari imekamilika unaweza kuwa unapaka mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni, na utapata matokeo
nb, pia unaweza tumia mafuta ya mawese ukawa unapaka sehemu iliyoathirika nayo pia utapata matokeo..
kwa mimi nilitumia vyoyte viwili yaani mafuta ya mawese na huo mchanganyiko wa lotion, ingawa mawese na lotion sikuchanganya nilikuwa napaka tofauti kwa mda mmoja.....
 
Sasa ni kipi kilikuponyesha hapo ni huo Mchanganyiko wa Lotion au mawese? au ni vyote kwa pamoja?
 
Msaada wa hiyo picha ya vestline alovera 70g tafadhali kiongozi.
 
Back
Top Bottom