Nchi hii kuna mambo ya ajabu sana,katika moja ya kampeni za mh. Samia rais wa JMT katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo,moja ya kauli mbiu yake katika miradi ya maji ni kumtua mama ndoo kichwanai.
Lakini ajabu na kweli kwenye miji iliyo pembezoni mwa vyanzo vya maji ndiyo inayo ongoza kwa ukosefu wa maji,tatizo nini au kampeni ya utekelezaji mradi huu unapigwa zengwe kwa sababu za kisiasa!!!
Ukitaka leo huduma ya kuunganishiwa maji inakulazimu kusubiri takribani zaidi ya mwaka mzima ndiyo surveys wakutembelee,then mwaka mmoja zaidi kwa ajili ya kuunganishiwa huduma hii,shida ni miundo mbinu,mkakati wa kumfelisha mama au kauli ya mama ni ya kisiasa zaidi haiendani na uhalisia wa tatizo lenyewe?

Kwanza kabisa hizi habari za hujuma za makusudi dhidi ya rais si kweli.
Matatizo ya maji kwa kiasi kikubwa yanayokana na sababu hizi.
1.Nchi inaongeza watu sana lakini uwezo wa mitambo na miundombinu hauongezwi kwa uwiano sawa na uongezekaji wa watu. Tena watu wanapoongezeka na uchumi kukua ndipo matumizi ya maji yanaongezeka kwenye shughuli kama kuosha magari, kumwagilia bustani za maua, kwenye swimming pools, etc. Pamoja na matumizi ya viwandani ambapo Dar es salaam inakadiriwa kuwa na shughuli za viwandani takriban 80% ya shughuli za nchi nzima.
Mfano, Dar es salaam ni mji mkubwa sana na kati ya miji inayokua kwa kasi sana duniani, inakadiriwa kuwa na watu zaidi ya milioni 6. Lakini mpaka leo Dar es salaam haina reservoir (bwawa) ya maji. Inategemea maji ya mto Ruvu. Maji ya mto Ruvu yanatoa lita milioni 300 kwa siku, mji wa Dar unahitaji lita milioni 450 kwa siku. Kuna upungufu wa lita milioni 150. Na hizo lita milioni 300, kwa makadirio ya DAWASA wenyewe, karibu nusu zinapotea njiani kabla ya kufikia mlengwa.
Mto Ruvu ulikuwa ukitoa lita mpaka milioni 520 kwa siku siku za nyuma, hilo linamaanisha umepunguza maji yanayoingia Dar kwa lita milioni 220 kwa siku. Huo ni upungufu wa 42%.
Climate change inachangia, lakini pia watu wameongezeka na kuharibu vyanzo vya maji.
Nchi kama Botswana, ambayo haina maji sana na sehemu yake kubwa tu ni jangwa la Kalahari, wameweza kuweka bwawa (Gaborone Dam) kuhudumia maji mji mkuu wao Gaborone.
2. Hatufanyii ukarabati mitambo na miundombinu inavyotakiwa.
3. Hatutumii vyanzo vya maji na kuvitunza vizuri.
4.Maji mengi yanapotea njiani.
5.Mashirika yetu ya umeme na maji hayaendeshwi kibiashara, yanaendeshwa kama ya public goods, which is not necessarily a bad thing, lakini yanashindwa kujiendesha inavyotakiwa na kuishia kutegemea ruzuku za serikali sana. Hatulipi gharama za umeme na maji at market price, mostly.
Haya ndiyo matatizo, na yanajulikana siku nyingi kabla Samia hajajulikana.
Haya ndiyo matatizo.
Zamani Upanga miaka ya mwanzo ya 80 tulikuwa tunapata maji bwerere mpaka juu ghorofani. Kufikia miaka ya mwisho ya 90 ikabidi kuweka pump kupandisha maji ghorofani.
Kwa nini?
Mji umeongeza watu wanaotumia maji sana, lakini mabomba ni yale yale.
Lakini, hata kama ni hujuma za makusudi dhidi ya huyu rais, rais wa Tanzania akiweza kuhujumiwa tu katika kitu cha msingi kama hiki, kashindwa kazi.
Yani rais wa Tanzania anatakiwa kuanza kazi siku ya kwanza kwa kujua kwamba kuna watu watataka kunihujumu, na kuweka mkakati wa kupambana nao.
Akishindwa hilo, kashindwa kuwa rais mwenye mkakati wa kufanya kazi yake.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.