Kuna mtoto ana miaka mitano sasa, mtoto alikuwa mbunifu, mwenye maswali sana, sasa amepata tatizo!
mwanzo alikuwa anasikia vizuri, lakini ametokea kuwa anapoteza uwezo wa kusikia vizuri, ili akusikie lazima awe karibu yako, akiwa mbali hasikii, ingawa masikio hayana usaha.
Nilimpeleka hospitali zetu za kiswahili, akapimwa na akaandikiwa dawa, tena za bei ghali nilizinunua akazitumia wala hazikumpa nafuu yoyote.
Wasamalia wema waliponisikia nikilalama juu ya tatizo hilo walinishauri kumpa amoxiline na dawa ya matone ya kudondoshea, (ingawa siikumbuki jina) ile dawa ilimsaidia akawa anasikia kwa kiasi fulani, lakini baada ya muda mfupi hali ile inarudi.
Naomba msaada wadau, ni dawa gani anatakiwa kupewa mtoto huyo?