Tatizo la mgawo/kukatika toka hivyo kwa umeme ni aibu sana kwa Serikali ya Tanzania chini ya Chama Cha Mapinduzi!

Kwanza, asante kwa observation yako. Nimepokea na hicho kipengere cha kuingiza siasa kidogo, nimekirekebisha kwa kujiondoa kabisa ili niwakere watu...
Umeandika jambo zuri bahati mbaya ukaja kuharibu baada ya kuingiza vyama, kwani hapo wavivu wa kufikiri watakomea kwenye kujadili vyama badala ya kulizungumzia tatizo husika ulilolitaja, hasa chanzo na nini kifanyike ili kulimaliza.

Mimi kwa upande wangu nitulie hapo ulipozungumzia tatizo wakati wa JPM halikuwa kubwa kama lilivyo wakati huu wa Samia, naamini hapa ndipo penye chimbuko la tatizo, na kutokana na hilo chimbuko, basi tunaweza kuijua solution.
Exactly ndivyo ilivyokuwa
Kwa upande wangu kinachotuumiza ni mindset tofauti za viongozi waliopo madarakani, na wale wanaopewa hiyo wizara kuiendesha, kuna wale wanaopewa na kujiona wamepewa keki hivyo wanajiamulia waanze kuitafuna upande upi[ bahati mbaya hawa ndio wengi zaidi].

Hawa watatengeneza vikwazo vya kila aina ilimradi kuufanya umeme usipatikane wa uhakika, ili waitumie nafasi hiyo kufanya biashara zao za majenereta, ni watu waliotawaliwa na ubinafsi wa hali ya juu, wasiokula wakashiba, ajabu huyo waziri kila siku anakuja na maneno ya uongo kuhusu chanzo cha kukatika umeme.
Ooh, kumbe...

Kwa hiyo ni sahihi kusema tatizo hili ni hujuma ya baadhi ya viongozi dhidi ya wananchi...!
Mfano, alishatudanganya wanafanya maintanance, kwamba wakati ule wa JPM palikuwa hapafanyiki maintanance ndio maana umeme ukawa haukatiki hovyo, sasa ajabu ni kwamba, wakati huu ambapo maintanance imekuwa inafanyika, hali ndio imekuwa mbaya zaidi, kumbe sababu ya maintanance ni uongo.

Akaja na sababu nyingine, mabwawa ya umeme yanakauka maji kutokana na upungufu wa mvua, hii kauli yake ikaja kupingana na meneja anayeendesha moja ya bwawa la kuzalisha umeme [simtaji jina yasijekumkuta] akadai maji yaliyokuwepo yalikuwa yanaweza kuzalisha umeme kwa muda mrefu ujao, huu nao ukawa uongo wa waziri.

Tufanyeje sasa tunapokuwa na viongozi wa dizaini hii wanaohujumu wananchi wao...?
Kwa hiyo mifano michache hapo juu, inaonesha vile wizara ya nishati amepewa mtu asiye na weledi wa kuiongoza, lakini hata sababu anazotoa kuhusu kukatika umeme, nazo zinamfanya apoteze uaminifu kwa jamii.

Lakini bahati mbaya aliyemuweka hana habari, anamuona kijana wake ni mchapakazi, anaonesha vile asivyomfuatiliaji wa wasaidizi wake, au anawafuatilia wale asio na urafiki nao, kwangu wizara ya nishati inamuhitaji mtu mwingine aje kuiongoza, asiyekuwa na makandokando ili kurudisha imani kwa watanzania, sio huyu mfanyabiashara aliyepo sasa.
Kama ndivyo hivi, ni wazi kuwa tatizo ni la mkubwa wake - Rais Samia Suluhu..

Kama ni tiba, tunapaswa kuielekeza dawa mahali hapo...

Huyu Rais anapenda kupokea maneno tu. Hataki kutembea field aone mwenyewe uhalisia wa kile anachoambiwa...

Hili ndilo tatizo hasa ukiachilia mbali changamoto ya mfumo wa kiutawala na kisiasa wa Tanzania kuwa wa hovyo usiosukuma tabia ya uwajibikaji kwa viongozi wa umma wanaoshindwa kutekeleza wajibu wao...
 
Kama kuna eneo ambalo serikali ya JMT inayoongozwa na TANU/ASP kisha CCM tangu uhuru 1961 imefeli spectacularly kisera na kimipango ni la upatikanaji wa huduma bora na ya kuaminika ya nishati ya umeme.

Ni aibu sana kuwa na umeme usioeleweka na unaokatikakatika hata mara 50 kwa siku. Sababu ambazo hutolewa na serikali za marais wote Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Samia ni zilezile. (lakini JPM alikuja akabidili mambo, akazikataa sababu hizo na mambo yakawa nafuu saaana).

Inashangaza sana kiasi cha mtu kujiuliza hivi hawa viongozi tuliowapa dhamana ya kimaamuzi na ki - raslimali fedha na watu wana akili nzuri za kufikiri kweli au kuna shida fulani vichwani mwao.

Haiwezekani TANESCO watangaze mgawo au kukosekana kwa huduma ya umeme kwa mikoa kadhaa kwa siku nzima kwa madai ya matengenezo ya miundombinu halafu wakirejesha huduma hiyo still tatizo linabaki kuwa palepale.!

Unajiuliza hawa watu walikuwa wanatengeneza nini iwapo tatizo la kukatika na kuwaka la umeme liko palepale.?

Na tatizo hili limekuwepo na kudumu tangu miaka ya u - Rais wa Mkapa, likaja likawa baya zaidi wakati u - Rais wa Jakaya Kikwete na sababu ambazo hutolewa ni zilezile miaka yote.

Lakini, mimi nikiri wazi kabisa kuwa, wakati wa u - Rais wa John P. Magufuli tatizo hili lilikuwepo lakini lilikuwa nafuu sana kwa kiwango cha kuvumilia na kueleweka kwa zaidi ya 90%.

Cha kushangaza ni kuwa tatizo hili limekuwa baya zaidi mara tu baada ya Rais Magufuli kufa na kuingia huyu mama. Watu tunajiuliza kulikoni? Je, ni serikali inafanyia hujuma wananchi wake.?

Na hata hawa wawekezaji hususani wa kutoka mataifa ya kigeni tunapowaalika kuja kuwekeza hapa nchini kwetu wanatuelewa vipi wanapokumbana na shida hizi?

Hivi CCM humuoni aibu ingalau kwenye ishu hii tu? Mimi nadhani sasa ni wakati mwafaka mkubali kuwa kwenye eneo hili sera na mipango yenu imeshindwa then GIVE UP na kama taifa tukae pamoja, tujadili na kutafuta namna kuifanya nchi isonge mbele...

Rais Samia hii hali haivumiliki. Hawa wananchi mnaodhani mnaweza kuwatendea vyovyote mtakavyo eti tu kwa sbb nyie ni "watawala" au "serikali", wana kikomo cha uvumilivu...

Itafika wakati tutasema, ENOUGH is ENOUGH na matokeo ya kauli hii yanaweza kuja kusababisha nyie viongozi mkakiimbia nchi hii bure.!

Shauri lenu. Jirekebisheni. Toeni huduma sahihi kwa wananchi ili mdai TOZO na KODI zingine kwa uhalali na siyo kwa namna hii...!

07 Septemba 2022

Ni kweli kumekuwepo uhaba wa mvua uliojitokeza kwenye maeneo mengi ya nchi yetu kwenye miezi ya hivi karibuni, uhaba huu umesababisha kuwepo kwa upungufu wa kina cha maji kwenye mabwawa ya kufua umeme kwa kutumia maji hivyo kuathiri hali ya uzalishaji wa umeme kwenye baadhi ya vyanzo vinavyotumia maji.

Aidha, ili kuhakikisha kuwa utoaji wa huduma ya umeme inaimarishwa nchini, Shirika limeshachukua hatua mbalimbali za muda mfupi na za muda mrefu kama ifuatavyo;

Mipango ya muda mfupi

[emoji625] Kuanzisha kituo cha kuzalisha umeme kwa njia ya Gesi asilia cha Ubungo III ambacho kimeshakamilika na kuingiza jumla ya Megawati 112 za umeme kwenye Gridi ya Taifa tangu mwanzoni mwa mwaka 2022.

[emoji625]Kuanzisha kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia Gesi asilia cha Kinyerezi I Extension kitakachozalisha jumla ya megawati 185.

Tayari megawati 45 zimeshaingizwa kwenye Gridi ya Taifa na megawati zilizobakia zitaingizwa kwenye Gridi ya Taifa hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka ujao.

[emoji625]Mradi wa kufua umeme wa Rusumo kwa kutumia maji.
Mradi huu unaozihusisha nchi tatu (Tanzania, Rwanda na Burundi) utakapokamilika, unategemewa kufua jumla ya megawati 80 za umeme, ambapo kwa upande wa Tanzania, tutapata megawati 27 za umeme zitakazoingizwa kwenye Gridi ya Taifa.

[emoji625]Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya jua wa Kishapu, Shinyanga.
Mradi huu unategemewa kuanza ujenzi wake Novemba 2022 na kukamilika Disemba 2023, utaingiza jumla ya megawati 150 za umeme kwenye Gridi ya Taifa.

[emoji625]Mradi wa kupeleka Gridi ya Taifa kwenye wilaya za mkoa wa Kigoma.
Tayari umeme wa Gridi ya Taifa umeshapelekwa kwenye wilaya ya Kibondo.
Serikali imeanza kuokoa jumla ya Tsh.9.44 bilioni kwa mwaka zilizokuwa zikitumika kununulia mafuta ya dizeli na kutengeneza mitambo (jenereta).
Mpango uliopo ni kuufikisha umme wa Gridi ya Taifa kwenye Wilaya ya Kasulu hadi Kigoma mjini kabla ya mwisho wa mwaka huu wa 2022 kufika.

Mipango ya muda mrefu

[emoji625]Mradi wa kufua umeme kwa kutumia maji wa bwawa la Julius Nyerere (JNHPP).

[emoji625]Mradi huu umefikia asilimia 71 ya utekelezaji wake.
Mradi utakapokamilika mnamo mwezi Juni 2024, unategemewa kuingiza megawati 2115 za umeme kwenye Gridi ya Taifa.

[emoji625]Kwa hatua hizi Shirika ilizozichuka zimesaidia kuimarisha hali ya upatikanaji umeme nchini na iwapo jitihada hizi zisingechukuliwa, basi ya upatikanaji umeme nchini kwa sasa ingekuwa ipo vibaya zaidi.
 
Sie huku ililitokea shot yaani ni siku ya 8 umeme hamna yaani inakera sana
 
Nyie TANESCO hebu acheni uongo wenu na kwa hakika msiendelee kutufanya sisi wananchi hamnazo na watu tusio na akili...

Hii lugha ya "tuna mipango ya muda mfupi na mrefu hii au ile" haijaanza leo wala jana. Ni lugha ambayo imekuwepo tangu enzi za Rais Mkapa, kisha Jakaya Kikwete na John P. Magufuli na sasa Rais Samia Suluhu anaendeleza ulaghai huu tena ktk namna mbaya sana ya kuumiza wananchi...

Na lugha hii ndugu zangu ni ya zaidi ya miaka 35 sasa na bado haijaweza kutatua tatizo la umeme hapa nchini kwetu...!

Ni lugha tu hii isiyo na substance yoyote...

Na si kosa hata kidogo kusema kuwa, mnachosema hapa ni lugha ya kisiasa ambayo mara nyingi huwa ni uongo kwa zaidi ya 90%...

Mathalani nyie TANESCO mnajua kuwa karibu maeneo yote ya nchi hata umeme huu kidogo uliopo mnaoutoa kwa mgawo unapokuwa unawaka reliability yake ni almost zero kwa sababu ikitokea miji au mitaa fulani ina umeme siku hiyo, basi ni ule unaokatika katika hovyo hata mara 50 kwa siku utadhani ni kibatali kilichotengwa kwenye uwanda wa upepo mkali...!

Sasa hebu tuambieni, hili nalo lina uhusiano gani na sababu ulizozitoa hapa za "uhaba wa umeme" kutokana na "mabwawa kukauka kwa sababu ya uhaba wa mvua...?"

Kwanini hata huu kidogo uliopo usiwe ni wa uhakika kwa nyakati na siku ambazo mitaa au mikoa fulani inapata umeme ili wananchi waendelee na shughuli zao za uzalishaji wa kutumia nishati ya umeme bila shida ...?

TANESCO kumbukeni hili, ya kwamba, hii mnayosema ndiyo mipango yenu ya muda mfupi na mrefu ambayo ndiyo suluhu ya tatizo la nishati ya umeme Tanzania....

Na kwa kuwa tuna kumbukumbu ya kauli kama hizi tangu enzi za Rais Mkapa, kisha Rais Kikwete kiasi cha kuja na mradi mkubwa wa matrilioni ya shilingi wa "Gesi ya Mtwara" tulioambiwa kuwa utakuwa mua arobaini wa umeme Tanzania lakini haikuwa hivyo,

Basi hata hii nayo ni yaleyale. SIASA na UONGO mtupu...

Ndiyo maana tunasema SERA na MIPANGO ya CCM kuhusu sekta na huduma ya nishati ya uimeshafeli spectacularly na CCM inahitaji misaada wa kutakiwa ikae pembeni tutafute namna ingine kuikwamua nchi hii na adha na matatizo haya yaliyodumu kwa miongo kadhaa sasa bila ufumbuzi wa kudumu...!

Suluhu ya hii siyo KAULI KAMA HIZI TENA bali kama taifa ni lazima tukubali na tuseme kwa pamoja kwamba, TUNA TATIZO na tatizo hili ni la kimfumo zaidi ktk maeneo ya kiutawala na siasa za nchi yetu...

Tukijajua hivi, tukae chini na kufikiri namna sahihi na ya uhakika ya kujikwamua hapa tulipo....

Nyie mliopo huko peke yenu mmeshashindwa na hamuwezi tena. Msisubiri kulazimishwa na mazingira na hasira za wananchi mara zitakaporuhusiwa...!
 
Inauma hapa naandika huku machozi yanabubujika nipo gizani
 
Kama kuna eneo ambalo serikali ya JMT inayoongozwa na TANU/ASP kisha CCM tangu uhuru 1961 imefeli spectacularly kisera na kimipango ni la upatikanaji wa huduma bora na ya kuaminika ya nishati ya umeme.

Ni aibu sana kuwa na umeme usioeleweka na unaokatikakatika hata mara 50 kwa siku. Sababu ambazo hutolewa na serikali za marais wote Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Samia ni zilezile. (lakini JPM alikuja akabidili mambo, akazikataa sababu hizo na mambo yakawa nafuu saaana).

Inashangaza sana kiasi cha mtu kujiuliza hivi hawa viongozi tuliowapa dhamana ya kimaamuzi na ki - raslimali fedha na watu wana akili nzuri za kufikiri kweli au kuna shida fulani vichwani mwao.

Haiwezekani TANESCO watangaze mgawo au kukosekana kwa huduma ya umeme kwa mikoa kadhaa kwa siku nzima kwa madai ya matengenezo ya miundombinu halafu wakirejesha huduma hiyo still tatizo linabaki kuwa palepale.!

Unajiuliza hawa watu walikuwa wanatengeneza nini iwapo tatizo la kukatika na kuwaka la umeme liko palepale.?

Na tatizo hili limekuwepo na kudumu tangu miaka ya u - Rais wa Mkapa, likaja likawa baya zaidi wakati u - Rais wa Jakaya Kikwete na sababu ambazo hutolewa ni zilezile miaka yote.

Lakini, mimi nikiri wazi kabisa kuwa, wakati wa u - Rais wa John P. Magufuli tatizo hili lilikuwepo lakini lilikuwa nafuu sana kwa kiwango cha kuvumilia na kueleweka kwa zaidi ya 90%.

Cha kushangaza ni kuwa tatizo hili limekuwa baya zaidi mara tu baada ya Rais Magufuli kufa na kuingia huyu mama. Watu tunajiuliza kulikoni? Je, ni serikali inafanyia hujuma wananchi wake.?

Na hata hawa wawekezaji hususani wa kutoka mataifa ya kigeni tunapowaalika kuja kuwekeza hapa nchini kwetu wanatuelewa vipi wanapokumbana na shida hizi?

Hivi CCM humuoni aibu ingalau kwenye ishu hii tu? Mimi nadhani sasa ni wakati mwafaka mkubali kuwa kwenye eneo hili sera na mipango yenu imeshindwa then GIVE UP na kama taifa tukae pamoja, tujadili na kutafuta namna kuifanya nchi isonge mbele...

Rais Samia hii hali haivumiliki. Hawa wananchi mnaodhani mnaweza kuwatendea vyovyote mtakavyo eti tu kwa sbb nyie ni "watawala" au "serikali", wana kikomo cha uvumilivu...

Itafika wakati tutasema, ENOUGH is ENOUGH na matokeo ya kauli hii yanaweza kuja kusababisha nyie viongozi mkakiimbia nchi hii bure.!

Shauri lenu. Jirekebisheni. Toeni huduma sahihi kwa wananchi ili mdai TOZO na KODI zingine kwa uhalali na siyo kwa namna hii...!
Muhimu kontenti, waache wazibe maskio mpaka madili yao ya wizi wa gesi yatimie,ila iko siku mbeleni watajuta,muhimu ni uhai tu
 
Nimeshuhudia kwenye misafara yake kila anapokanyaga sehemu swali ni hilohilo.

Anajisikia burudani au huzuni kama Mimi Makinikia?
 
Kwani kwenye ziara wapo na January?
 
Nyie TANESCO hebu acheni uongo wenu na kwa hakika msiendelee kutufanya sisi wananchi hamnazo na watu tusio na akili...

Hii lugha ya "tuna mipango ya muda mfupi na mrefu hii au ile" haijaanza leo wala jana. Ni lugha ambayo imekuwepo tangu enzi za Rais Mkapa, kisha Jakaya Kikwete na John P. Magufuli na sasa Rais Samia Suluhu anaendeleza ulaghai huu tena ktk namna mbaya sana ya kuumiza wananchi...

Na lugha hii ndugu zangu ni ya zaidi ya miaka 35 sasa na bado haijaweza kutatua tatizo la umeme hapa nchini kwetu...!

Ni lugha tu hii isiyo na substance yoyote...

Na si kosa hata kidogo kusema kuwa, mnachosema hapa ni lugha ya kisiasa ambayo mara nyingi huwa ni uongo kwa zaidi ya 90%...

Mathalani nyie TANESCO mnajua kuwa karibu maeneo yote ya nchi hata umeme huu kidogo uliopo mnaoutoa kwa mgawo unapokuwa unawaka reliability yake ni almost zero kwa sababu ikitokea miji au mitaa fulani ina umeme siku hiyo, basi ni ule unaokatika katika hovyo hata mara 50 kwa siku utadhani ni kibatali kilichotengwa kwenye uwanda wa upepo mkali...!

Sasa hebu tuambieni, hili nalo lina uhusiano gani na sababu ulizozitoa hapa za "uhaba wa umeme" kutokana na "mabwawa kukauka kwa sababu ya uhaba wa mvua...?"

Kwanini hata huu kidogo uliopo usiwe ni wa uhakika kwa nyakati na siku ambazo mitaa au mikoa fulani inapata umeme ili wananchi waendelee na shughuli zao za uzalishaji wa kutumia nishati ya umeme bila shida ...?

TANESCO kumbukeni hili, ya kwamba, hii mnayosema ndiyo mipango yenu ya muda mfupi na mrefu ambayo ndiyo suluhu ya tatizo la nishati ya umeme Tanzania....

Na kwa kuwa tuna kumbukumbu ya kauli kama hizi tangu enzi za Rais Mkapa, kisha Rais Kikwete kiasi cha kuja na mradi mkubwa wa matrilioni ya shilingi wa "Gesi ya Mtwara" tulioambiwa kuwa utakuwa mua arobaini wa umeme Tanzania lakini haikuwa hivyo,

Basi hata hii nayo ni yaleyale. SIASA na UONGO mtupu...

Ndiyo maana tunasema SERA na MIPANGO ya CCM kuhusu sekta na huduma ya nishati ya uimeshafeli spectacularly na CCM inahitaji misaada wa kutakiwa ikae pembeni tutafute namna ingine kuikwamua nchi hii na adha na matatizo haya yaliyodumu kwa miongo kadhaa sasa bila ufumbuzi wa kudumu...!

Suluhu ya hii siyo KAULI KAMA HIZI TENA bali kama taifa ni lazima tukubali na tuseme kwa pamoja kwamba, TUNA TATIZO na tatizo hili ni la kimfumo zaidi ktk maeneo ya kiutawala na siasa za nchi yetu...

Tukijajua hivi, tukae chini na kufikiri namna sahihi na ya uhakika ya kujikwamua hapa tulipo....

Nyie mliopo huko peke yenu mmeshashindwa na hamuwezi tena. Msisubiri kulazimishwa na mazingira na hasira za wananchi mara zitakaporuhusiwa...!
Siasa imetawala vichwa vya viongozi wetu matokeo yake hata jambo la kiufundi wanaingiza siasa, ndio maana kila siku matatizo hayaishi, wanaona raha kutudanganya maisha yaende hawajui uwajibikaji wala chochote, ni kama vile wameona wanaongoza kondoo.
 
Back
Top Bottom