Habarini.
mshana jr na
MziziMkavu na wataalamu wengine humu ndani naombeni msaada.
Miguu yangu inanisumbua sana, inakuwa kama inaganzi wakati mwingine kama inawaka moto nikienda hospitalini napimwa naambiwa naumwa U.T.I natumia dawa lakini bado.
Sijui tatizo nini, naombeni msaada tafadhali
TATIZO LA MIGUU KUWAKA MOTO MIGUU
Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili
yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu hujulikana kwa jina la Peripheral Neuropathy.
Matatizo haya ya kiafya (miguu/mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) na
hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguuni au mikononi.
Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu ni hizi zifuatazo
1.Mtu kuhisi ganzi
2. kushindwa kushika au kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli na kadhalika.
3.maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni/mikononi,
Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuatayo:
1.Kupungua kwa virutubisho mwilini,hasa mkusanyiko wa vitamini B, (Vitamin B Complex).
2.Matumizi ya dawa, mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya ukimwi
3.Uzito mkubwa wa mwili,
4.Ugonjwa wa kisukari,(diabetic polyneuropathy).
5.Shinikizo la damu,
Nina kuuliza Swali je una uzito wa mwili kilo ngapi? Una miaka mingapi? umeowa au umeolewa?
Unao ugonjwa wa kisukari? unao ugonjwa wa Maradhi ya Presha? Kapime huenda una Ukosefu wa Kupungua kwa virutubisho Mwilini?