Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

nimewahi kuwa na tatizo kama lako,nimeenda kwa waganga na waganguzi lakini wapi,tatizo lako laweza kuwa UTI na minyoo ambayo waweza kuwa sababu ya gonjwa lako,tibu haya matatizo hakika utapona
 
Tumia tiba hii ya kitunguu saumu na ndimu loweka miguu kwenye beseni la maji vuguvugu yenye mchanganyiko wa kitunguu saumu kilichopondwa na ndimu iliyokamuliwa
Asante sana Mshana Jr kwa misaada wako Mungu akujalie zaidi ya hapa. Ngoja nijaribu nitakupa mrejesho
 
Habarini.
mshana jr na MziziMkavu na wataalamu wengine humu ndani naombeni msaada.
Miguu yangu inanisumbua sana, inakuwa kama inaganzi wakati mwingine kama inawaka moto nikienda hospitalini napimwa naambiwa naumwa U.T.I natumia dawa lakini bado.
Sijui tatizo nini, naombeni msaada tafadhali

TATIZO LA MIGUU KUWAKA MOTO MIGUU

Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili

yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu hujulikana kwa jina la Peripheral Neuropathy.
Matatizo haya ya kiafya (miguu/mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) na

hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguuni au mikononi.
Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu ni hizi zifuatazo

1.Mtu kuhisi ganzi

2. kushindwa kushika au kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli na kadhalika.

3.maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni/mikononi,
Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuatayo:

1.Kupungua kwa virutubisho mwilini,hasa mkusanyiko wa vitamini B, (Vitamin B Complex).

2.Matumizi ya dawa, mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya ukimwi

3.Uzito mkubwa wa mwili,

4.Ugonjwa wa kisukari,(diabetic polyneuropathy).

5.Shinikizo la damu,

Nina kuuliza Swali je una uzito wa mwili kilo ngapi? Una miaka mingapi? umeowa au umeolewa?

Unao ugonjwa wa kisukari? unao ugonjwa wa Maradhi ya Presha? Kapime huenda una Ukosefu wa Kupungua kwa virutubisho Mwilini?
 
Heshima kwenu wana JF,
Kuna hii tatizo la viganja vya miguu kuwaka moto na haswa tatizo linakuwa kubwa nyakati za usiku wakati wa kulala mpaka unashindwa kupata usingizi kwa wakati.

Tatizo lenyewe ilianza hivi; Mwaka 2007 wakati naenda kuanza kidato cha tano nilianza kuhisi miguu kuwa moto wakati nikiwa kwa gari na safari ilikuwa ndefu sana ilibidi nivue viatu ili nipate ahueni. Hiyo ilikuwa safari ya kutoka babato to tanga.

Hali hii iliendelea kwa muda wote huo nikiwa tanga na hasa nikiwa class either tunafundishwa au najisomea huwa navua viatu na soksi ili viganja viguse sakafu ndo angalau vinapoa
Sasa tatizo lilianza kuwa kubwa 2009 nikiwa morogoro na kila nikienda hospital inaonekana uelewa wa madaktari ni mdogo kuhusu tatizo langu.

Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu bila muafaka wa tatizo nilijaribu kuwashirikisha baadhi ya ndugu zangu ndo wakaniambia kuwa utakuwa umefanyiwa mambo ya kishirikina na nilielekezwa kwenda kwa mtumishi moja wa mungu hapo DAR.

Mwaka 2010 nilienda kwa mtumishi huyu anayepatina kivule na akaniombea akasema niwekewa vitu vingi sana mwilin na wachawi na akatoa midude mingi ya ajabu na nikaacha sadaka ya20,000/- angalau nilipata nafuu nikarudi moro kuendelea na masomo. Baada ya muda tatizo lilirudi ikabidi nirudi tena kwenye huduma kama mbili na nilikuwa na acha kiasi hicho hicho cha sadaka.

Sasa nikiwa kazin mwaka 2014 niliamua kwenda DAR maana tatizo ndo limeongezeka nilipofika niliambiwa sadaka ya huduma ya maombezi imepanda mpaka 60,000/-Tsh na mazaga mengine ya maombi pia lazima ninunue.

Na wakati wa maombi huwa nabaki na boksa ninapakwa mafuta na kunyiziwa mapafyum ndo anaanza kuomba na kunitoa hayo madude.

Sasa wakuu nikisharudi maskani tatizo lile lile huku nikiwa nimetumia garama kubwa ya nauli Babati to Dar and Dar to Babat, garama za logde, sadaka, chakula lakin hakuna mafanikio. Sasa wadau naombeni msaada kwa wenye ufaham wa tatizo hii.

NAWASILISHA
 
Mkuu, ukiacha tatizo hilo la ganzi na miguu kuwaka moto una tatizo lingine kiafya?
 
Mkuu, ukiacha tatizo hilo la ganzi na miguu kuwaka moto una tatizo lingine kiafya?
Lipo ni kitambo kidogo nilikiwa naweza kuacha nywele zirefuke bila tatizo lakin sasa zikikuwa kidogo tu huwa zinawasha sana.

Na kingine ni kwamba kila nikiwa naswaki huwa nahidi kutapika na pia huwa nipanda gari huwa natapika sana hata kama sijala huwa pumzi inakata
 
Lipo ni kitambo kidogo nilikiwa naweza kuacha nywele zirefuke bila tatizo lakin sasa zikikuwa kidogo tu huwa zinawasha sana. Na kingine ni kwamba kila nikiwa naswaki huwa nahidi kutapika na pia huwa nipanda gari huwa natapika sana hata kama sijala huwa pumzi inakata
Mkuu mimi sio daktari kwahiyo nakushauri umuone daktari mzoefu hasa wale wazee.

Miguu kupata ganzi na kuwaka moto wakati mwingine husababishwa na msongo wa mawazo/stress au kukosa kulala kwa muda unaopendekezwa, na zaidi sana upunguvu wa vitamin fulani huchangia kupata tatizo hilo.

Hivyo wakati unatafuta matibabu jaribu kubadili style yako ya maisha kuanzia namna unavyofikiri(usiwe na mawazo sana/stess, lala masaa saba hadi nane, pata chakula kizuri fanya mazoezi kila siku na uwe na muda wa kupumzika.

Madaktari wengi ukienda kuonana nao ukishawaambia miguu inawaka moto basi haraka haraka watakuambia upime kisukari. Kama unatumia pombe acha kabisa.
 
Mkuu mimi sio daktari kwahiyo nakushauri umuone daktari mzoefu hasa wale wazee. Miguu kupata ganzi na kuwaka moto wakati mwingine husababishwa na msongo wa mawazo/stress au kukosa kulala kwa muda unaopendekezwa, na zaidi sana upunguvu wa vitamin fulani huchangia kupata tatizo hilo. Hivyo wakati unatafuta matibabu jaribu kubadili style yako ya maisha kuanzia namna unavyofikiri(lndoa mawazo/stess, lala masaa saba hadi nane, pata chakula kizuri fanya mazoezi kila siku na uwe na muda wa kupumzika. Madaktari wengi ukienda kuonana nao ukishawaambia miguu inawaka moto basi haraka haraka watakuambia upime kisukari. Kama unatumia pombe acha kabisa.
Kwanza mi bado kijana ndo niko early 30s wala si mnyuaji tena maana nilitumia pombe kidogo nikiwa chuo. Huwa sinaga stress kivile na kwenda madactari nilishaenda lakin hamna muafaka.
 
Kwanza mi bado kijana ndo niko early 30s wala si mnyuaji tena maana nilitumia pombe kidogo nikiwa chuo. Huwa sinaga stress kivile na kwenda madactari nilishaenda lakin hamna muafaka.
Madaktari wanatofautiana na ndo maana nikakuambia utafute daktari mzoefu.
 
Hii ya kuombewa na kutolewa matakataka mengi ya kichwi mwilin mnalionaje? na baada ya muda tatizo linabaki pale pale sasa naombeni mnipatie njia mbadala jamani
 
Back
Top Bottom