habari.
mimi ni daktari wa fiziotherapia.
miguu kuwaka moto na kukosa nguvu ya miguu na kupepesuka.
Hizo dalili mara nyingi hutokana na athari ambazo zimetokea kwenye pingili za uti wa mgongo.hasa pingili za mgongo wa chini (lumber area)
ambapo kuna mishipa ya fahamu midogo(peripheral nerves) ambayo inatoka kwenye mshipa wa fahamu mkubwa (spinal cord) na kupeleka taarifa za hisia(joto ,baridi,maumivu) na command za kukaza au kulegea kwa misuli.
athari ikitokea kwenye mishipa hyo ya fahamu hupelekea taarifa hizo kutofika lwa usahihi au kutofika kabisa kulingana na ukubwa wa tatizo.
hii hupelekea hisia kama ganzi,mguu kuwaka moto,shoti ya umeme kutoka mgongoni hadi miguuni ,sisimizi kutembea kwenye mguu au baridi kali kwenye miguu na kupungua nguvu ya misuli ya mguu au kupooza .
nguvu ya misuli ya mguu ikipungua huleta hali ya mtu kukosa balance akiwa anatembea au kusimama hivyo hupepesuka.
athari hii ikiwa kubwa sana mtu anaweza kupooza mwili kuanzia kwenye kiuno hadi miguu yote miwili.
hivyo basi nakushauri sehemu ulipo nenda kwenye hospitali ya rufaa onana na daktari bingwa wa mifupa (orthopedic) atakufanyia uchunguzi kama kipimo cha MRI ( magnetic reasonance imaging) cha eneo la mgongo ili kufahamu tatizo ulilo nalo.
Baada ya hapo tatizo likionekana atakupa matibabu ya dawa. Na atakuambia ukaanze mazoezi tiba (physiotherapy) katika kitengo cha Fiziotherapia.
Huko utapata msaada mkubwa na hali yako kurudi kama zamani.
Wahi mapema maana matatizo hayo huongezeka siku hadi siku. ukiwahi utaepusha madhara makubwa kutokea.
Habar zenu ndugu znguu,,mwezenu na Kama mwaka sas nasumbuliwa na tatizo la kuwaka Moto miguun na kushika ganzi pia(miguu yote miwil)...na sas imepelekea kukosa nguvu miguun hata nnavyo tembea huwaga napepesuka Kama vle nmelewa.......plz naomba ushauri ndugu znguu Ni ipi tiba au dawa ya kutumia ili npate kuponaaa[emoji120]