Street lawyer
New Member
- Apr 13, 2025
- 1
- 0
Habari za wakati huu wana jamvi. Naomba kujua je mtoto huyu ana changamoto gani na ni nini tiba yake? Kuna mtoto wa mjomba wangu kwa sasa ana umri wa miaka miwili na nusu. Mtoto huyu tangu azaliwe amekuwa na changamoto ya kukoroma muda wote na kutoa milio kama vile pua zake zimeziba, kwa kifupi hupumua kwa shida sana.
Vile vile huzungusha macho muda wote. Tumejaribu kwenda hospital mbalimbali kwaajili ya tiba lakini majibu tunayopewa ni kwamba hali hiyo ni kawaida na itaendelea kuisha taratibu.
Chakushangaza hatua za ukuaji kwa huyu mtoto ni za taratibu sana kwa umri alionao wa miaka miwili na nusu anakaa tu na hakuna dalili hata za kutambaa wala kumove, lakini pia hawezi kuongea zaidi ya neno mama kula kwake ni kwa shida sana. Mwili wake ni mnene(Bonge) kwa wastani.