Mkuu, Mimi pia Nina hali hiyo ila siioni hata kama ni tatizo.
Mfano, naenda kukutana na mtu Fulani au naenda katika kongamano Fulani, ama naenda sehemu mpya ambayo itanipasa kujitambulisha.
Naanza kupanga maneno na mistari jinsi ya kuanza kuzungumza. Naongea kwa sauti lakini siyo kubwa.
Na nikifika, nashusha maneno yote kama ambavyo nilikuwa nikizungumza mwenyewe.
Na najisikia vema Sana kwani maneno yangu yanakuwa yamepangika katika mtiririko mzuri na kuniongezea ari ya kujiamini vema.
Kuna siku nilikuwa naenda kwenye interview. Kabla sijafika, nikiwa njiani nilikuwa najiuliza maswali na njia ya kujibu.
Cha kushangaza, nimefika kwenye interview maswali yote ambayo nilikuwa najiuliza na kutoa majibu ndiyo hayo hayo niliyoulizwa na interview Pannel.
Naomba madaktari wanieleze, huu pia ni ugonjwa?