Tatizo la mtu kuongea peke yake: Fahamu visababishi na namna ya kutatua shida hii

Tatizo la mtu kuongea peke yake: Fahamu visababishi na namna ya kutatua shida hii

Mkuu yaani mimi najikuta naongea mwenyewe kama najibishana na mtu nishachunguza kwetu tupo hivyo hasa kwa upande wa mama ila naona ni genetic

Nikija moshi ntakutafuta mkuu maana ulishawahi kusema huku jf unakaa KCMC

Sio kila mara niko hapo sasa niko Kibiti
 
Nenda kwa wataalamu mku kwanza una umri gani, neurotransmitters zikianza kupungua unakuwa matatizo.

Nina miaka 26 ila nimejitadhimini sana maana najiona sio wa kawaida. Nilipochunguza nikagundua mama yangu anaongea mwenyewe kama ... (nimtunzie siri mama yangu) nilipoendaga kwa ndugu zangu upande wa mama nao ni hivyo hivyo nika hitimisha hii itakuwa genetic disorder.

Sasa najiuliza kuna njia ya kutibu maana mimi najitahidi kuwa social sana ila haiba yangu inakataa maana nikitaka kuongea na mtu stranger najitutumua sana ila naona nashindwa. Na kama nikishapishana naye nikifika home naanza kuongea mwenyewe mpaka najishangaa.

Kama kuna tiba naomba msaada
 
@Aleppo,
aone wataalamu watakufanyia unchunguzi lakini inaonekana ni genetic issue pia imechangia
 
Sio kila mara niko hapo sasa niko Kibiti

Hahahaha sawa mkuu ila ukiwa huku usije ukajisahau kusema ulipo maana ulisemaga mwaka jana kwenye uzi mmoja ambao mmoja alianzisha kuhusu watu wa kilimanjaro na wewe ukasema vile.

Anyway naomba msaada wako maana hapa kwetu workmate wangu wanasema kila kitu hawana ile confidentiality

Nisaidie mawazo nafanyaje
 
-Una mambo mengi kichwani ila huna wa kumshirikisha, jitahidi kuwa na partner wa kujadiliana nae mambo kadha wa kadha.
-Pia kuna baadhi ya watu huongea mambo yao kwa sauti ili iwe rahisi zaidi kuyakumbuka hasa kwa wale watu wasahaulifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni pure genetic haswa sasa najitutumuaje nayo maana sasa ntauwa kichaa aisehh
Ukienda hospitali wataalamu wanajua jinsi ya kulisolve utapewa vidonge lakini Nikita arudi tu matibabu yake ni ya muda mrefu na wala isifike Mshana ukajiona imepona ua he kutumia dawa hapana.
 
Hahahaha sawa mkuu ila ukiwa huku usije ukajisahau kusema ulipo maana ulisemaga mwaka jana kwenye uzi mmoja ambao mmoja alianzisha kuhusu watu wa kilimanjaro na wewe ukasema vile.

Anyway naomba msaada wako maana hapa kwetu workmate wangu wanasema kila kitu hawana ile confidentiality

Nisaidie mawazo nafanyaje
Ni sawa mkuu, sisi vijana kuzunguka ni kawaida. Ntakuwa Mbagala alhamis mchana nikuone two hours.
 
Dah mi nna tatizo la kuongea kingereza mda wote najikuta kiswahili kinanishinda sijui tatizo nini hata nikitaka niongee kiswahili maneno yanakosa

blame no body
 
Wengi ni wenye kigugumizi ndiyo mara nyingi huongea pekeyao, mie ndugu zangu upande wa baba ndiyo huongea wenyewe kama wanapiga stata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mdau hapo juu kahusisha hali yako ya kiafya na matumizi ya canabis, watu hawana huruma, hilo tatizo lako liko sana mjini tangu Magu aingie madarakani, watu wamekua wanaongea wenyewe barabarani, wakifanya alama za mikono na kuvuka barabara bila ata ya kuanglia magari, hii ni shida kubwa sana. Kuna shida kubwa sana kwenye afya ya akili hapa nchin kwetu, ni jambo lakufanyia kazi.
 
Back
Top Bottom