star health talks
Member
- Apr 28, 2017
- 30
- 73
Tatizo la Presha kuwa juu
Ugonjwa wa presha kuwa juu ni miongoni mwa magonjwa yanayowakumba watu wengi kwa sasa katika jamii.
Kutokuwa na elimu sahihi ya ugonnjwa huu pamoja na kuwa na imani potofu juu ya ugonjwa huu inachangia wingi wa tatizo hili, imani potofu na elimu duni ya ugonnjwa inaanzia kwenye dalili mpaka matibabu yake.
Hii inapelekea watu wengi kushindwa kupata matibabu sahihi na hatimaye kuishia katika matatizo makubwa ya kiafya.
Kitaalamu presha ni mgandamizo wa kitu ,( Pressure =Force/area) huu mgandamizo unaweza ukawa mkubwa au kidogo, hivyo presha inaweza ikawa ya juu/ presha ya kupanda au pressure ya chini/presha ya kushuka.
Kabla ya kuzungumzia pressure hizi za kupanda na kushuka ni muhimu kujikumbusha pressure ya kawaida/normal ni ipi.
Pressure ya kawaida/normal blood pressure ya mwanadamu ilipatikana baada ya kuwapima watu wengi na kupata wastani wa presha za watu wazima wa kawaida ambao hawana magonjwa yoyote. hivyo ikaafikiwa kuwa pressure ya kawaida ya binadamu haitakiwi kufika au kuzidi 140/90 mmHg.
Kama nlivyosema awali hapo juu kuwa normal human blood pressure ilipatikana kwa wastani, hivyo makundi au taasisi mbalimbali za kiafya ulimwenguni zinaweza kutumia namba tofauti kidogo lakini tofauti hizo ni ndogo sana.
Tukianzia na pressure ya kupanda/ shinikizo kubwa la damu, hapa ni pale ambapo ukipima pressure kwa kuzingatia na kutumia vipimo sahihi na mazingira sahihi unapata Presha inayoanzia au kuzidi 140/90 mmHg zaidi ya mara moja.
Kwa kufafanua zaidi, sio lazima zote/ namba ya juu (140) na chini (90) hapo juu ziwe zimezidi, ikitokea moja ipo juu mfano 150/60 mmHg, una shida ya pressure tayari, au ya chini ndo ikawa juu mfano 132/100 mmHg, una shida ya pressure tayari.
Pressure ya kushuka hapa mtu anakuwa na pressure iliyo chini ya wastani wa presha ya watu wengi, wastani huu huwa ni 120/80 mmHg, mara nyingi pressure hii ya kushuka hutokana na mtu kupoteza maji mwilini mfano mtu akiharisha, kutapika sana au kupoteza damu nyingi, hii huambatana moja kwa moja na kupanda kwa mapigo ya moyo.
Cha muhimu kujua hapa ni kuwa watu mbalimbali watakuwa na presha tofauti tofauti, mfano mtu anaweza kuwa na presha ya 98/67 mmHg, kama mtu huyu hana visababishi vya Pressure kushuka maana yake hiyo ndio normal blood pressure yake.
Kwanini mtu anapata shinikizo kubwa la damu/ high blood pressure?
kwa watu wengi ugonjwa huu unakuwa hauna sababu yoyote kwa maana nyingine unatokea tu, kwa watu wachache mtu anakuwa na tatizo jingine ambalo linampelekea apate shinikizo kubwa la damu.
Je dalili za shinikizo kubwa la damu/ high blood pressure ni zipi?
Mtu anaweza asiwe na dalili yoyote ya pressure kuwa juu, yaani mtu anafanya shughuli zake za kila siku bila shida yoyote lakini akipima pressure ipo juu sana, nadhani tumewahi sikia case za watu kuanguka ghafla tu, kupata kiharusi/stroke ghafla, naam hawa wanakuwa na pressure kubwa bila wao kujua, baadhi ya watu huhisi kichwa kuuma, n.k
Yapi ni madhara ya kuwa na shinikizo kubwa la damu/ high blood pressure
mojawapo ya madhara anayoweza kupata mtu ni pamoja na stroke/kiharusi, figo kufeli, moyo kutanuka na matatizo ya macho.
Matibabu yake yapoje?
matibabu ya shinikizo kubwa la damu ni kuanza dawa mara moja, kupunguza au kumantain uzito, kuacha au kupunguza matumizi ya pombe na sigara.