Tatizo la Presha kuwa juu/ shinikizo kubwa la damu

Joined
Apr 28, 2017
Posts
30
Reaction score
73
Tatizo la Presha kuwa juu

Ugonjwa wa presha kuwa juu ni miongoni mwa magonjwa yanayowakumba watu wengi kwa sasa katika jamii.
Kutokuwa na elimu sahihi ya ugonnjwa huu pamoja na kuwa na imani potofu juu ya ugonjwa huu inachangia wingi wa tatizo hili, imani potofu na elimu duni ya ugonnjwa inaanzia kwenye dalili mpaka matibabu yake.

Hii inapelekea watu wengi kushindwa kupata matibabu sahihi na hatimaye kuishia katika matatizo makubwa ya kiafya.

Kitaalamu presha ni mgandamizo wa kitu ,( Pressure =Force/area) huu mgandamizo unaweza ukawa mkubwa au kidogo, hivyo presha inaweza ikawa ya juu/ presha ya kupanda au pressure ya chini/presha ya kushuka.

Kabla ya kuzungumzia pressure hizi za kupanda na kushuka ni muhimu kujikumbusha pressure ya kawaida/normal ni ipi.

Pressure ya kawaida/normal blood pressure ya mwanadamu ilipatikana baada ya kuwapima watu wengi na kupata wastani wa presha za watu wazima wa kawaida ambao hawana magonjwa yoyote. hivyo ikaafikiwa kuwa pressure ya kawaida ya binadamu haitakiwi kufika au kuzidi 140/90 mmHg.

Kama nlivyosema awali hapo juu kuwa normal human blood pressure ilipatikana kwa wastani, hivyo makundi au taasisi mbalimbali za kiafya ulimwenguni zinaweza kutumia namba tofauti kidogo lakini tofauti hizo ni ndogo sana.

Tukianzia na pressure ya kupanda/ shinikizo kubwa la damu, hapa ni pale ambapo ukipima pressure kwa kuzingatia na kutumia vipimo sahihi na mazingira sahihi unapata Presha inayoanzia au kuzidi 140/90 mmHg zaidi ya mara moja.

Kwa kufafanua zaidi, sio lazima zote/ namba ya juu (140) na chini (90) hapo juu ziwe zimezidi, ikitokea moja ipo juu mfano 150/60 mmHg, una shida ya pressure tayari, au ya chini ndo ikawa juu mfano 132/100 mmHg, una shida ya pressure tayari.

Pressure ya kushuka hapa mtu anakuwa na pressure iliyo chini ya wastani wa presha ya watu wengi, wastani huu huwa ni 120/80 mmHg, mara nyingi pressure hii ya kushuka hutokana na mtu kupoteza maji mwilini mfano mtu akiharisha, kutapika sana au kupoteza damu nyingi, hii huambatana moja kwa moja na kupanda kwa mapigo ya moyo.

Cha muhimu kujua hapa ni kuwa watu mbalimbali watakuwa na presha tofauti tofauti, mfano mtu anaweza kuwa na presha ya 98/67 mmHg, kama mtu huyu hana visababishi vya Pressure kushuka maana yake hiyo ndio normal blood pressure yake.

Kwanini mtu anapata shinikizo kubwa la damu/ high blood pressure?
kwa watu wengi ugonjwa huu unakuwa hauna sababu yoyote kwa maana nyingine unatokea tu, kwa watu wachache mtu anakuwa na tatizo jingine ambalo linampelekea apate shinikizo kubwa la damu.

Je dalili za shinikizo kubwa la damu/ high blood pressure ni zipi?

Mtu anaweza asiwe na dalili yoyote ya pressure kuwa juu, yaani mtu anafanya shughuli zake za kila siku bila shida yoyote lakini akipima pressure ipo juu sana, nadhani tumewahi sikia case za watu kuanguka ghafla tu, kupata kiharusi/stroke ghafla, naam hawa wanakuwa na pressure kubwa bila wao kujua, baadhi ya watu huhisi kichwa kuuma, n.k

Yapi ni madhara ya kuwa na shinikizo kubwa la damu/ high blood pressure
mojawapo ya madhara anayoweza kupata mtu ni pamoja na stroke/kiharusi, figo kufeli, moyo kutanuka na matatizo ya macho.

Matibabu yake yapoje?
matibabu ya shinikizo kubwa la damu ni kuanza dawa mara moja, kupunguza au kumantain uzito, kuacha au kupunguza matumizi ya pombe na sigara.
 
Kwenye ugonjwa wowote, Chanzo au vyanzo inatakiwa kujulikana kwanza, ndipo tiba sahihi ifuate.

Na kwa wengine wanaweza kukabiliana na chanzo cha tatizo, Akazingatia taratibu za kiafya, Na akapona pasipo kutumia dawa.

Chanzo cha tatizo ndio kila kitu, wito wangu tusipende kutumia dawa bila kujua chanzo cha tatizo.

---
Kwa hisani ya AI:
Vyanzo vikuu vinavyochangia shinikizo la damu, hasa kwa watu wengi, ni pamoja na:
  1. Mtindo wa maisha usiofaa
    • Lishe isiyofaa: Kula vyakula vyenye chumvi nyingi, mafuta na sukari nyingi.
    • Kutofanya mazoezi: Kukosa shughuli za mwili kunaweza kuongeza hatari ya uzito kupita kiasi.
  2. Uzito kupita kiasi (Obesity)
    • Uzito mkubwa husababisha mzigo zaidi kwa moyo na mishipa, na hivyo kuongeza shinikizo la damu.
  3. Msongo wa mawazo (Stress)
    • Changamoto za kila siku na msongo wa mawazo zinaweza kuchangia kuongezeka kwa shinikizo la damu.
  4. Urithi wa kijeni
    • Ikiwa kuna historia ya shinikizo la damu katika familia, hatari inaweza kuwa kubwa zaidi.
  5. Magonjwa ya msingi (Secondary Hypertension)
    • Magonjwa kama vile matatizo ya figo, matatizo ya viungo vya endocrine (kama hyperthyroidism), au matatizo mengine ya kiafya yanaweza kusababisha shinikizo la damu kupanda.
Kwa ujumla, kwa watu wengi shinikizo la damu hupatikana bila sababu moja iliyo wazi (primary hypertension), lakini vigezo hivi vinaweza kuchangia na kuongeza hatari.
 
Tatizo la Presha kuwa juu

Ugonjwa wa presha kuwa juu ni miongoni mwa magonjwa yanayowakumba watu wengi kwa sasa katika jamii.
Kutokuwa na elimu sahihi ya ugonnjwa huu pamoja na kuwa na imani potofu juu ya ugonjwa huu inachangia wingi wa tatizo hili, imani potofu na elimu duni ya ugonnjwa inaanzia kwenye dalili mpaka matibabu yake.

Hii inapelekea watu wengi kushindwa kupata matibabu sahihi na hatimaye kuishia katika matatizo makubwa ya kiafya.

Kitaalamu presha ni mgandamizo wa kitu ,( Pressure =Force/area) huu mgandamizo unaweza ukawa mkubwa au kidogo, hivyo presha inaweza ikawa ya juu/ presha ya kupanda au pressure ya chini/presha ya kushuka.

Kabla ya kuzungumzia pressure hizi za kupanda na kushuka ni muhimu kujikumbusha pressure ya kawaida/normal ni ipi.

Pressure ya kawaida/normal blood pressure ya mwanadamu ilipatikana baada ya kuwapima watu wengi na kupata wastani wa presha za watu wazima wa kawaida ambao hawana magonjwa yoyote. hivyo ikaafikiwa kuwa pressure ya kawaida ya binadamu haitakiwi kufika au kuzidi 140/90 mmHg.

Kama nlivyosema awali hapo juu kuwa normal human blood pressure ilipatikana kwa wastani, hivyo makundi au taasisi mbalimbali za kiafya ulimwenguni zinaweza kutumia namba tofauti kidogo lakini tofauti hizo ni ndogo sana.

Tukianzia na pressure ya kupanda/ shinikizo kubwa la damu, hapa ni pale ambapo ukipima pressure kwa kuzingatia na kutumia vipimo sahihi na mazingira sahihi unapata Presha inayoanzia au kuzidi 140/90 mmHg zaidi ya mara moja.

Kwa kufafanua zaidi, sio lazima zote/ namba ya juu (140) na chini (90) hapo juu ziwe zimezidi, ikitokea moja ipo juu mfano 150/60 mmHg, una shida ya pressure tayari, au ya chini ndo ikawa juu mfano 132/100 mmHg, una shida ya pressure tayari.

Pressure ya kushuka hapa mtu anakuwa na pressure iliyo chini ya wastani wa presha ya watu wengi, wastani huu huwa ni 120/80 mmHg, mara nyingi pressure hii ya kushuka hutokana na mtu kupoteza maji mwilini mfano mtu akiharisha, kutapika sana au kupoteza damu nyingi, hii huambatana moja kwa moja na kupanda kwa mapigo ya moyo.

Cha muhimu kujua hapa ni kuwa watu mbalimbali watakuwa na presha tofauti tofauti, mfano mtu anaweza kuwa na presha ya 98/67 mmHg, kama mtu huyu hana visababishi vya Pressure kushuka maana yake hiyo ndio normal blood pressure yake.

Kwanini mtu anapata shinikizo kubwa la damu/ high blood pressure?
kwa watu wengi ugonjwa huu unakuwa hauna sababu yoyote kwa maana nyingine unatokea tu, kwa watu wachache mtu anakuwa na tatizo jingine ambalo linampelekea apate shinikizo kubwa la damu.

Je dalili za shinikizo kubwa la damu/ high blood pressure ni zipi?

Mtu anaweza asiwe na dalili yoyote ya pressure kuwa juu, yaani mtu anafanya shughuli zake za kila siku bila shida yoyote lakini akipima pressure ipo juu sana, nadhani tumewahi sikia case za watu kuanguka ghafla tu, kupata kiharusi/stroke ghafla, naam hawa wanakuwa na pressure kubwa bila wao kujua, baadhi ya watu huhisi kichwa kuuma, n.k

Yapi ni madhara ya kuwa na shinikizo kubwa la damu/ high blood pressure
mojawapo ya madhara anayoweza kupata mtu ni pamoja na stroke/kiharusi, figo kufeli, moyo kutanuka na matatizo ya macho.

Matibabu yake yapoje?
matibabu ya shinikizo kubwa la damu ni kuanza dawa mara moja, kupunguza au kumantain uzito, kuacha au kupunguza matumizi ya pombe na sigara.
asante, barikiwa!
 
Elimu nzuri sana , milo mibovu ya wanga , sukari na mafuta kwa wingi hilo ni tatizo kubwa kwa sasa.
 
Pressure kuwa juu sio ugonjwa ni dalili au kiashiria cha ugonjwa fulani.

Medical experts nje na dawa za kizungu ni weupe kichwani hamjui alternative yeyote na haya maradhi huwa hayaishi kwa mtu asipokuwa makini anaweza jikuta anazeeka mapema kwa kubugia vidonge daily
 
naomba kueleweshwa alternatives unazozihubiri wewe
 
Pressure kuwa juu sio ugonjwa ni dalili au kiashiria cha ugonjwa fulani.

Medical experts nje na dawa za kizungu ni weupe kichwani hamjui alternative yeyote na haya maradhi huwa hayaishi kwa mtu asipokuwa makini anaweza jikuta anazeeka mapema kwa kubugia vidonge daily
Fafanua mkuu usiishie hewani tu,,toa elimu watu wanufaike,ndo maana yajukwaa hili,uenda una hoja yenye mashiko,lkn basi tufafanulia ueleweke.
 
Back
Top Bottom