Tatizo la simu kusumbua chaji ni langu peke yangu?

Oraimo ni chaja zinazofanya kazi ipasavyo ila sio Imara, zina tabia ya sehemu ya kuchomeka usb kuwa loose,

Kwa hizi chaja za bei rahisi kwa experience yangu kuna model flani ya kichina zinajitahidi wanauza 9000 kwenye mall za kichina kama home city

Ina port ya usb ya kawaida na type C.

Pia kuna chaja za Iphone za type C kwenda lightining nazo sio mbaya wanauza kama 10,000. Unachomoa waya wa iphone unaweka wa kwako.

Alternative nunua online, tafuta chaja ya maana, kutegemea na simu ukipata chaja kama YA Xiaomi, Oneplus, Oppo etc OG kabisa ile utakaa nayo hadi utachoka, binafsi sijawahi haribu chaja ya oneplus, moja ninayo toka 2017 hadi leo ipo fresh, ila hai fast charge kila simu, angalia model ya simu yako nunua chaja inayoendana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…