Tatizo la Tanzania ni viongozi wengi hawana uzalendo wa kweli

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Tanzania viongozi wengi wanaenda kwa mazoea na siasa wanaona kama biashara binafsi. Wananchi wengi wanatambua sasa kwamba viongozi wengi badala ya kuangalia nchi kwanza wanaangalia famila zao kwanza na kutafuta jinsi ya kujilimbikizia mali.

Kitendo cha kununua magari ya zaidi ya milioni 300 wakati hakuna gari wa wagojwa tena magari ni kwa viongozi wa wilaya inaonyesha jinsi gani viongozi wanajijali wenyewe zaidi. Mikataba nasikia wameweka mpaka mkuu wa mkoa wao Kilimanjaro ili kuanzia mkuu wa mkoa mpaka waziri wawe watu wanajuana na kufanya rahisi kubinafsisha uwanja wa KIA bila sababu za msingi zaidi ya rushwa. Hakuna sababu yeyote au faida kwa nchi kwa kubinafsisha uwanja ambao una wageni wengi na serikali inatakiwa kuongeza tu runway na majengo!! lakini airport haiko kwao na wanaona watu wa kule sio watu wa chama chao. Hautasikia airport ya zanzibar inabinafsishwa hata siku moja.

Bunge linatunga sheria ambazo hazijulikani zinasaidia nani mfano utatungaje sheria mpya za chaguzi na walalamikiwa tume wote bado ndiyo wafanyakazi kwa chaguzi ambazi zilikuwa mbaya! halafu wananchi wakuone upo serious.

Kibaya zaidi hata wasanii na hata kwenye mitandao kuna watu wengi wanakuwa machawa ili wapate kazi au pesa bila kujali nchi. Nchi hii imekuwa nchi ya kila mtu kujali tumbo lake tu. Hakuna mtu anajali legacy wala nini. Hata wazee wastaafu wa miaka 80 kama Mswekwa bado wanaogopa kuongea!

Hivyo tunawaomba vijana msiige kabisa tabia za watu wazima maana mtu kuwa na nchi mbaya sana huko mbele kama tabia zenu zitakuwa kama za wazazi na hawa viongozi.
 
Mifumo inawalazimisha au kuwapelekea kuwa wapigaji. Watu huwa wanaingia kwenye hizi kazi wakiwa na nia njema kabisa
 
Back
Top Bottom