Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Tatizo la umeme nchi hii haijaanza leo, huku chanzo kikubwa cha tatizo miaka yote kikiwa ni kile kile. Hivyo? hakuna sababu mpya na ilio nje ya uwezo wao zaidi ya hizi serikali za CCM miaka yote kushindwa kuja na suluhu ya Kudumu ya hili tatizo.
Serikali ya Magufuli ambayo Mama Samia alikuwa Makama wa Raisi, haikuwa na kipaumbele kwenye chanzo mbadala cha umeme zaidi ya kuwaza umeme wa maji kupitia mto Rufiji. Kama waliwaza vyanzo vingine, basi ilikuwa ni geresha tu.
Halikadhalika, Waziri Mkuu na Waziri wa sasa wa Nishati na aliepita, wote walikuwa katika serikali ya Magufuli na walihusika kupitisha mipango na hata Bajeti za serikali Bungeni bila kuona umuhimu wa kutoa kipaumbele kwa vyanzo mbadala vya nishati ya umeme.
Hivyo, kabla hawajafikiria kuchukua hatua yotote kutatatua tatizo hili zikiwemo hatua za kuwajibisha walio chini yao( in case wanapanga hivyo) nashauri wote wajiuzulu turudi kwenye uchaguzi tutafute watu wengine wa kuongoza hii nchi.
Ukiacha serikali ya Nyerere, zingine zote zimeshindwa kuwekeza vya kutosha katika vyanzo mbdala vya umeme na haya ndio matokeo yake.
Utawala wa Kikwete ulijitahidi kwa kiasi chake kuwekeza katika vyanzo mbadala ingawa si kwa kiasi cha kutosha huku wakituacha kwenye sintafahamu kuhusu swala zima la gesi.
Baba wa Taifa tunaweza kumsamehe kwasababu kwa nyakati zake, ilikuwa ni sahihi kwa nchi kuwekeza zaidi katika chanzo cha umeme wa maji ukizingatia mazingira ya wakati huo na uchanga wa nchi yetu bila kusahau uwezo wetu kama nchi nyakati hizo.
Hivyo, CCM na viongozi wake ndio wanapaswa kuwajibika kwa sasa kabla ya mtu mwingine yoyote kuwajibika au kuwajibishwa.
Tumechoka na tumewachoka.