Tatizo la upele Kidevuni: Chanzo na matibabu yake

na mimi nna tatizo kama lako vipi mdau ulipata ufumbuzi ?
 
kwa kuongezea tumia nyembe halisi halafu usitumie wembe mmoja zaidi ya mara mbili , tumia mswaki au kitambaa kigumu kusugua kidevu chote kila uogapo kisha paka ndimu au limao alternatively tumia electric shaver na fanya na hayo mengine yote
 
Mi nimejaribu njia kibao but tatizo hili haliishi
 
Mi nimejaribu njia kibao but tatizo hili haliishi

Nunua mashine yako ambayo mtakuwa hamchangii na mtu yeyote. Hii inasaidia kupunguza kuota mapele baada ya kunyoa kwa zaidi ya 97%. Hilo nina uhakika nalo kwani iliwahi kunitokea na Mimi miaka iliyopita.
 
Kaka tatizo hilo husababishwa na kujipenyeza kwa vijidudu katika ngozi iliyo chanika. Kwahiyo hakikisha unanawa mikono nasabuni kabla ya kuanza nyoa, kisha safisha kidevu pia.
Nivizuri kuwa na mashine binafsi
 
Tumia magic powder haisababish vipele, inbox nikuelekeze namna ya kuitumia na wapo uinunue.. Inauzwa 7000 hapo mwenge
 
Nunua mashine yako ambayo mtakuwa hamchangii na mtu yeyote. Hii inasaidia kupunguza kuota mapele baada ya kunyoa kwa zaidi ya 97%. Hilo nina uhakika nalo kwani iliwahi kunitokea na Mimi miaka iliyopita.

Okey asante
 
nyoa ndevu kwa Hair remover yaan hautapata michubuko ypoyote itakayokusababisha kutoka vipele!
 
nyoa ndevu kwa Hair remover yaan hautapata michubuko ypoyote itakayokusababisha kutoka vipele!

Kitu chochote utakacho tumia kikatoa ndevu zoooote!! Amini kama ngozi yako ni ya mafuta utaota upele ambao hujawahi upata,, mf. Hair remover,magic shave poda,na zifananazo .
 
Kitu chochote utakacho tumia
kikatoa ndevu zoooote!! Amini kama ngozi yako ni ya mafuta utaota upele
ambao hujawahi upata,, mf. Hair remover,magic shave poda,na zifananazo
.

Hili tatizo limekuwa ugonjwa kama UKIMWI maana dawa zilizopo ni kama kupunguza makali tu kama ARV.Wataalum wajipange upya
 
Hili tatizo limekuwa ugonjwa kama UKIMWI maana dawa zilizopo ni kama kupunguza makali tu kama ARV.Wataalum wajipange upya

Mkuu mimi nakushudia nilikuwa naota mapele baada ya kunyoa mpaka najiogopa. Kuna kipindi mpaka kidevu kilianza kutoa magamba ukijikuna. Ukichukulia na rangi ya ngozi yangu yaani kila MTU anaweza kujua kwamba nimezidiwa.

Nilitumia dawa za kila aina bila mafanikio, scrub sijui ya chumvi inakuwa kama nimekolezea hivi. Niliponunua mashine yangu ya kunyolea kidevu changu kimekuwa safi yaani mpaka najiuliza ni nini kilinitokea. Na mashine yenyewe ni hela ndogo tu! Mi nilinunua 35000tshs
 
Nunua shaving machine utakayotumia peke yako ni bei rahis sana, pale game zipo hadi za sh.13, 000/= hapo hapo nakushauri kama upo dar nenda kariakoo tafuta dawa ya asili inaitwa SHABU uwe unajipaka kwa muda ili kusafisha ngozi yako ya kidevu, na kukausha hayo mapele
 
na mimi nna tatizo kama lako vipi mdau ulipata ufumbuzi ?

Nina tatizo la kutokwa na vipele pia but huja pale tu ninapotumia wembe, ila nikitumia mashine za umeme na only kupaka spirit sina shida kabisa, achana na wembe!
 
Hupaki dawa yeyote baada ya kushave?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…