Tatizo la upele Kidevuni: Chanzo na matibabu yake

Tatizo la upele Kidevuni: Chanzo na matibabu yake

Hili ni tatizo ambalo hata nami nimekutana nayo sana miaka kadha iliyopita

Elimu aliyotoa mhalisi ni nzuri lakini Mi naona bado haimalizi tatizo tajwa.

Fanya hivi,Acha ndevu ziote usiogope kabisa, hata unaweza acha kama mwezi moja hivi
Maana ukiacha ndevu hivyo yale maupele yanapungua ama kwisha kbs.
Sasa siku ya kwenda kunyoa hakikisha kabisa una kangua yote na ikiwezekana tumia wembe na hakikisha kbs una LIMAO moja hata mbili mkononi.

Ukimaliza tu kunyoa kata limao ktkt na pakaa kote kwenye usawa wa ndevu!
Hata kesho yake pakaa tena!
Halafu kama unatumia wembe sasa hakikisha baada ya siku tatu tena pitisha wembe tena na pakaa limao na hapo mwenyewe utaleta majibu hapa kwamba Jamiiforums kuna kila aina ya mtu.

Pole sana Kamanda!

kwa kuongezea tumia nyembe halisi halafu usitumie wembe mmoja zaidi ya mara mbili , tumia mswaki au kitambaa kigumu kusugua kidevu chote kila uogapo kisha paka ndimu au limao alternatively tumia electric shaver na fanya na hayo mengine yote
 
Mi nimejaribu njia kibao but tatizo hili haliishi
 
Mi nimejaribu njia kibao but tatizo hili haliishi

Nunua mashine yako ambayo mtakuwa hamchangii na mtu yeyote. Hii inasaidia kupunguza kuota mapele baada ya kunyoa kwa zaidi ya 97%. Hilo nina uhakika nalo kwani iliwahi kunitokea na Mimi miaka iliyopita.
 
Kaka tatizo hilo husababishwa na kujipenyeza kwa vijidudu katika ngozi iliyo chanika. Kwahiyo hakikisha unanawa mikono nasabuni kabla ya kuanza nyoa, kisha safisha kidevu pia.
Nivizuri kuwa na mashine binafsi
 
Kwa muda mrefu now ninasumbiliwa na tatizo la kutoka vipele baada ya kunyoa ndevu,nimetafuta tiba sana lkn hakuna nafuu yani mpk nw sijui tiba nitaipata lini,mara ya mwisho dactari aliniambia vipele vinatokea bse ndevu zinapoota zinashindwa kupenyeza kwenye ngozi hivyo kujisokota kwa ndani na kusababisha vipele,plz anayefahamu tiba yake anipe taarifa.PLZ TUKAWA SERIOUS MTU ANAPOOMBA USHAURI AU MSAADA KWA MAMBO YANAYOGUSA AFYA NA SI KUANZA KUKEJELI.

Tumia magic powder haisababish vipele, inbox nikuelekeze namna ya kuitumia na wapo uinunue.. Inauzwa 7000 hapo mwenge
 
Nunua mashine yako ambayo mtakuwa hamchangii na mtu yeyote. Hii inasaidia kupunguza kuota mapele baada ya kunyoa kwa zaidi ya 97%. Hilo nina uhakika nalo kwani iliwahi kunitokea na Mimi miaka iliyopita.

Okey asante
 
nyoa ndevu kwa Hair remover yaan hautapata michubuko ypoyote itakayokusababisha kutoka vipele!
 
nyoa ndevu kwa Hair remover yaan hautapata michubuko ypoyote itakayokusababisha kutoka vipele!

Kitu chochote utakacho tumia kikatoa ndevu zoooote!! Amini kama ngozi yako ni ya mafuta utaota upele ambao hujawahi upata,, mf. Hair remover,magic shave poda,na zifananazo .
 
Kitu chochote utakacho tumia
kikatoa ndevu zoooote!! Amini kama ngozi yako ni ya mafuta utaota upele
ambao hujawahi upata,, mf. Hair remover,magic shave poda,na zifananazo
.

Hili tatizo limekuwa ugonjwa kama UKIMWI maana dawa zilizopo ni kama kupunguza makali tu kama ARV.Wataalum wajipange upya
 
Hili tatizo limekuwa ugonjwa kama UKIMWI maana dawa zilizopo ni kama kupunguza makali tu kama ARV.Wataalum wajipange upya

Mkuu mimi nakushudia nilikuwa naota mapele baada ya kunyoa mpaka najiogopa. Kuna kipindi mpaka kidevu kilianza kutoa magamba ukijikuna. Ukichukulia na rangi ya ngozi yangu yaani kila MTU anaweza kujua kwamba nimezidiwa.

Nilitumia dawa za kila aina bila mafanikio, scrub sijui ya chumvi inakuwa kama nimekolezea hivi. Niliponunua mashine yangu ya kunyolea kidevu changu kimekuwa safi yaani mpaka najiuliza ni nini kilinitokea. Na mashine yenyewe ni hela ndogo tu! Mi nilinunua 35000tshs
 
Nunua shaving machine utakayotumia peke yako ni bei rahis sana, pale game zipo hadi za sh.13, 000/= hapo hapo nakushauri kama upo dar nenda kariakoo tafuta dawa ya asili inaitwa SHABU uwe unajipaka kwa muda ili kusafisha ngozi yako ya kidevu, na kukausha hayo mapele
 
na mimi nna tatizo kama lako vipi mdau ulipata ufumbuzi ?

Nina tatizo la kutokwa na vipele pia but huja pale tu ninapotumia wembe, ila nikitumia mashine za umeme na only kupaka spirit sina shida kabisa, achana na wembe!
 
Mkuu mimi nakushudia
nilikuwa naota mapele baada ya kunyoa mpaka najiogopa. Kuna kipindi
mpaka kidevu kilianza kutoa magamba ukijikuna. Ukichukulia na rangi ya
ngozi yangu yaani kila MTU anaweza kujua kwamba nimezidiwa. Nilitumia
dawa za kila aina bila mafanikio, scrub sijui ya chumvi inakuwa kama
nimekolezea hivi. Niliponunua mashine yangu ya kunyolea kidevu changu
kimekuwa safi yaani mpaka najiuliza ni nini kilinitokea. Na mashine
yenyewe ni hela ndogo tu! Mi nilinunua 35000tshs

Hupaki dawa yeyote baada ya kushave?
 
Back
Top Bottom