mi ngoja nikupe ushuhuda wangu. nilijarib after shaves nyingi bila mafanikio. nikaamua kunyoa kwa magic powder. mwanzon ikaonekana kufeli vibaya. nikagundua makosa makubwa ni mashart kutofuatwa na watu wa salun hasa dakika inazopaswa kukaa kwenye ngoz na kiwango cha kupaka na kutotumia aina yoyote ya kemikali hasa aftershave au shampoo au sabun kuosha ngozi husika. pia kutokuwa na mfumo mmoja wa welekeo wa ukwanguaj wa ndevu wakat wa kuosha. sasa inunue 7000 na nunua vifaa vya kutumia mwenyewe kwa mashart yenyewe. utasahau vipele. vifaa chukua taulo ndogo cotton, brush ya kupakia hasa ya kuchorea maneno, kioo, kibakuri cha kukorogea magic powder, spray ya maji ndogo. ukipaka usizid dk 5-7(na hapa ndo salun weng hupata rushes unapakwa unakaa mda mrefu inakuunguza). na ukishakwangua safisha kwa maji tu sio kemikali yoyote( hapa salun wanakusafisha kwa shampoo ung'ae ndo wanakumalizia). ukinyoa usiku ni bora ili asb uko sawa na kuoga kwa sabun. mi nilpona hivyo kwa miaka 6 sasa. side effects mpaka sasa ninazoona ni kuwa na ndevu baadh zenye mvi. lakin bora mana mapele njia nyingne zote yalishindikana.