Tatizo la upele Kidevuni: Chanzo na matibabu yake

Tatizo la upele Kidevuni: Chanzo na matibabu yake

mi ngoja nikupe ushuhuda wangu. nilijarib after shaves nyingi bila mafanikio. nikaamua kunyoa kwa magic powder. mwanzon ikaonekana kufeli vibaya. nikagundua makosa makubwa ni mashart kutofuatwa na watu wa salun hasa dakika inazopaswa kukaa kwenye ngoz na kiwango cha kupaka na kutotumia aina yoyote ya kemikali hasa aftershave au shampoo au sabun kuosha ngozi husika. pia kutokuwa na mfumo mmoja wa welekeo wa ukwanguaj wa ndevu wakat wa kuosha. sasa inunue 7000 na nunua vifaa vya kutumia mwenyewe kwa mashart yenyewe. utasahau vipele. vifaa chukua taulo ndogo cotton, brush ya kupakia hasa ya kuchorea maneno, kioo, kibakuri cha kukorogea magic powder, spray ya maji ndogo. ukipaka usizid dk 5-7(na hapa ndo salun weng hupata rushes unapakwa unakaa mda mrefu inakuunguza). na ukishakwangua safisha kwa maji tu sio kemikali yoyote( hapa salun wanakusafisha kwa shampoo ung'ae ndo wanakumalizia). ukinyoa usiku ni bora ili asb uko sawa na kuoga kwa sabun. mi nilpona hivyo kwa miaka 6 sasa. side effects mpaka sasa ninazoona ni kuwa na ndevu baadh zenye mvi. lakin bora mana mapele njia nyingne zote yalishindikana.
 
njia pekee ni hii hapa usinyoe ndevu zote punguza tu mi nimetumia dawa nyingi pamoja na hizo ulizotaja sikufanikiwa/
 
Ni nmecontrol mapele kwa kutomaliza ndev wakati nanyoa..zinabaki kwa mbali sana
 
Unaweza kunyoa zote Ila Ukimaliza OSHA vizuri na maji ya uvuguvugu na sabun na hakikisha umejisugua vizuri sana kwa nguvu kiasi kumake sure hujabaki na uchafu wowote na kimsingi ndo unaleta infections, maliza kwa kupaka cream ambayo ni antifungal mf acrason zinapatikana duka LA dawa 3500/-
 
Habari wapendwa.

Naomba msaada kwa anayefahamu dawa ya mapele ya ndevu.

Msaada tafadhali.
 
Habari wapendwa. Naomba msaada kwa anayefahamu dawa ya mapele ya ndevu. msaada tafadhari.

Me nilikuwa muathirika wa vipele vya ndevu.....
Nilichofanya na mpaka leo namaliza mwaka wa pili sina vipele
1. Natumia machine yangu ninapoenda kunyoa 'home cutting'
2. Nina kinyozi wangu . Ye ndiyo peekee anaeninyoa
3. Ukimaliza kunyoa penda kypaka mafuta ya asili kama ya nazi kwa kidevu chako
 
Kwenye kidevu kuna aina mbili za nywele.

Nywele ngumu- hizi nywele ukikata kwa wembe probability kubwa vipele vitaota. Kwa sababu zikiota huwa zinachoma ngozi na hivyo kusababisha uvimbe au kipele.

Chakufanya- nyolea mashine ya kawaida. Hutapata vipele. Japo chemicals zipo kwa kuzuia vipele

Pili nywele laini- hizi hata unyoe kwa wembe vipele havitoki. Kama waarabu na wazungu.

Tadhamini upo kundi lipi
 
Tumia mkasi zibaki zile za chini chini sana kama Dr.Shein anavyonyoa hutopata kipele na bado utaonekana smart kukwangua ngozi ya kidevu unaikomaza sana mwishowe inaanza kuonekana kama goti la mlemavu wa miguu
 
Nilianza kuota ndevu takribani miaka 7 iliyopita, katika miaka 2 ya mwanzo nilifurahia kua na ndevu na nilinyoa ndevu kwa staili yoyote ile niipendayo.
Baada ya muda huo nilianza kusumbuliwa na tatizo la kutokwa na vipele kila baada ya kunyoa/kuchonga ndevu zangu.
Kukabiliana na tatizo hili niliamua kutumia njia 3 kwa nyakati tofauti lakini zote zimegonga mwamba na mpaka sasa vipele vya ndevu vinanitoka sana mpaka kutishia kuharibu unadhifu wa ngozi yangu...
Njia ambazo nilitumia kuondoa vipele zimekua zinanisaidia mwanzoni tu lakini baada ya muda vipele huendelea na kutotibiwa na njia/dawa husika! Njia/dawa hizo ni kama ifuatavyo;
√Kubadili vivyozi/barber shop
√Split na after shave aina nyingi
√Eskinol
√Gentlemen pride(product ya forever)
√Gentrose
√Persol gel
√Kukanda maji ya moto
√Kupaka mawe flani meupe
√Kupaka utomvu wa alovera
√Kubadili lotion nazotumia mfano Nivea, cocopulp, kupakaa mafuta mfano zawadi zanzibar, babycare
√Shaving cream
√Kunyoa kwa kutumia magic powder
√Kushave mwenyewe kwa kutumia povu la gillete etc
Pamoja na kutumia njia/dawa hizo katika vipindi tofauti tofauti zoote zimeshindwa kutatua tatizo langu. Kwa waliowahi kuona tatizo kama hili tushirikiane kupata ufumbuzi wake
 
Back
Top Bottom