Habari wana JF, naliamini sana jukwaa la JF maana huku kuna watu multi professions. Tatizo langu nasumbuliwa sana na mapele yanayotokea baada ya kunyoa ndevu. Nilikuwa natumia hizi mashine za kawaida za salon nikaona kama ndo tatizo, nikaanza kutumia Magic shaving powder, pamoja na after shave moja hv ya mafuta sikumbuki jina lake niliinunua S.H Amon, tatizo likapoa kwa mda ila likajirudia, nikarudi kutumia tu mashine za salon na tatizo bado sijalimanya utatuzi wake. Hebu nisaidieni wadau ni njia gani ya kuzuia haya mapele ama ni after shave gani zinaondoa tatizo hili ama kama kuna dawa yake itakuwa vizuri sana jama, natamani sana kuwa na kidevu soft bila rashes. Msaada wenu wa kitabibu bandugu.