Nilianza kuota ndevu takribani miaka 7 iliyopita, katika miaka 2 ya mwanzo nilifurahia kua na ndevu na nilinyoa ndevu kwa staili yoyote ile niipendayo.
Baada ya muda huo nilianza kusumbuliwa na tatizo la kutokwa na vipele kila baada ya kunyoa/kuchonga ndevu zangu.
Kukabiliana na tatizo hili niliamua kutumia njia 3 kwa nyakati tofauti lakini zote zimegonga mwamba na mpaka sasa vipele vya ndevu vinanitoka sana mpaka kutishia kuharibu unadhifu wa ngozi yangu...
Njia ambazo nilitumia kuondoa vipele zimekua zinanisaidia mwanzoni tu lakini baada ya muda vipele huendelea na kutotibiwa na njia/dawa husika! Njia/dawa hizo ni kama ifuatavyo;
√Kubadili vivyozi/barber shop
√Split na after shave aina nyingi
√Eskinol
√Gentlemen pride(product ya forever)
√Gentrose
√Persol gel
√Kukanda maji ya moto
√Kupaka mawe flani meupe
√Kupaka utomvu wa alovera
√Kubadili lotion nazotumia mfano Nivea, cocopulp, kupakaa mafuta mfano zawadi zanzibar, babycare
√Shaving cream
√Kunyoa kwa kutumia magic powder
√Kushave mwenyewe kwa kutumia povu la gillete etc
Pamoja na kutumia njia/dawa hizo katika vipindi tofauti tofauti zoote zimeshindwa kutatua tatizo langu. Kwa waliowahi kuona tatizo kama hili tushirikiane kupata ufumbuzi wake