goggles
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,415
- 2,358
Alizaliwa nazo.Mwanao ana umri gani?? Ana ndevubtayari??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alizaliwa nazo.Mwanao ana umri gani?? Ana ndevubtayari??
Mh....?Alizaliwa nazo.
Magic inaleta mvi kabla ya uzeeAcha kunyolea wembe. Jaribu kutumia magic kunyolea iwapo unatoka vipele hata baada ya kutumia mashine!
Kwani wewe unaogopa mvi? Zikija si unazipaka Picol au Easy black 😱😱😱Magic inaleta mvi kabla ya uzee
Asante sana kwa Elimu mkuu.......Pole sana mkuu, Dawa ni kutokunyoa ndevu zote. Unaacha ndogo kama zinazoota, usikwangue zikaisha kabisa.
Ngozi na nywele za binadamu zinatofautiana kila mtu. Wewe una Ngozi ngumu, sasa wakati wakati nywele inaota, inakutana na Ngozi ngumu, inashindwa kutoka, halafu inageuka nyuma na kuendelea kuota kwa kuelekea ndani, hapo unaanza uvimbe ambao wewe unaona ni vipele.
Kwa mfano, ukitoboa hicho kipele, utakutana na unywele mlefu uliokuwa umejiviringa kwa ndani.
MUHIMU, PUNGUZA NDEVU WAKATI WA KUNYOA, KUCHONGA IWE MARUFUKU, TATIZO LAKO LITAISHA.
Asante sn nashukuru kwa usahuri!Usinyoe kipara, lkn uctumie magic hautabaki salama baada ya miaka 20 saratani ya ngozi itakuandama
Asante sn mkuuChukua ushauri huu utakusaidia sana na ni very cheap; mi mwenywe nilikuwa kama wewe ila niimepona kabisa..
Hakuna ishu za mashine wala nini, we fanya hivi ukishanyoa makesure unakanda kwa kitaulo chenye maji ya moto 40+C hv, kwa dak kadhaa kama 3&5 hv,
Baada ya hapo paka AFTER SHAVE , utakuwa umemaliza tatizo lako..
Naomba uje unipe mrejesho..
Habari za majukumu wakuu,Nasumbuliwa na tatizo la vipele na baadae natokewa na mabaka meusi hii ni baada ya kunyoa ndevu haijalishi nimenyoa wapi na nimepewa huduma nzuri kiasi gani.
Naomba msaada kwa anayejua dawa au kinga ya hii kitu,mbalikiwe sana
Asante sana na ubarikiweDah, mi sikushauri utumie 'magic' kwasababu kama hiyo dawa ni kali kuweza kupupua ndevu vipi kuhusu ngozi yako, maana ngozi ya binadamu ni laini na nyembamba sana.
Nywele zetu zinatofautiana sana, kuna wale ambao ni nyembamba sana, zikiota zinakuwa zimenyooka, zinatoka nje ya ngozi moja kwa moja. Watu hawa (waasia, wazungu, latino na baadhi ya waafrika) hawana tatizo la kutoka vipele. Sasa kuna wengine ambao nywele zao ni nene, hawa zinaanza kujiviringa wakati bado hazijatoka nje ya ngozi, huendelea kukua huku zikijisokota ndani kwa ndani.
Mwili huhisi kunatatizo, unaanza kujihami ukidhani kuna adui ameingia kwenye ngozi. Mara moja unaanza kutengeneza askari wake (antibodies) kujilinda. kiasi cha askari wanao tengenezwa ndio ukubwa wa kututumka kwa sehemu husika (upele).
Mimi binafsi situmii viwembe ila natumia mashine ya kunyolea pamoja na dawa ya kuzuia vipele. Dawa hii huwa naipata kwenye maduka ya urembo ya wachina au wakati hata amazon.
View attachment 530854